WAY

Wednesday, February 6, 2013

TWANGA KUMFANYIA LUIZER MBUTU BIRTHDAY jumamosi

 


MWIMBAJI na Kiongozi wa Bendi ya African Stars “Twanga Pepeta” Luizer Mbutu anataraji kufanyiwa sherehe ya siku yake ya kuzaliwa (Birthday Party) siku ya Jumamosi tarehe 09-02-2013 katika ukumbi wa Mango Garden uliopo maeneo ya Kinondoni jijini Dar es salaam.

Luizer Mbutu hii ni mara ya pili kufanyiwa sherehe hiyo huku kwa mara ya kwanza ilikuwa ni mwaka jana, sherehe ilifanyika katika Club ya Maisha iliyopo Oysterbay.

Ikumbukwe ASET Imeamua kumfanyia Luizer Mbutu sherehe hiyo kwa mara yapili mfululizo kwa kutambua mchango wake mkubwa alioutoa katika bendi ya Twanga Pepeta kwa kudumu kwa muda mrefu bila kuhama na kwa kufanya kazi kwa kujituma bila ya kuchoka toka aanze kazi rasmi ndani ya Bendi mpaka leo.

Sambamba na sherehe hiyo Twanga Pepeta kama ilivyo kawaida yao watainogesha sherehe hiyo ya Kiongozi wao kwa masebene matamu yatayoendana na nyimbo nzuri zilizo na meseji zilizojitosheleza kutoka kwa wanamuziki wenye vipaji vya viwango vya hali ya juu kabisa.

Wadau mbalimbali wamealikwa kuhudhuria sherehe hiyo ili kutoa sapoti kwa Kiongozi huyo wa Bendi katika siku yake ya kuzaliwa kwa kuwa utatumika utaratibu kama wa mwaka jana wa kulishwa keki kwa wadau na marafiki walio karibu na bendi ya Twanga Pepeta.

0 comments:

Post a Comment

.

.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...