WAY

Monday, February 18, 2013

RAMA PENTAGONE AELEZEA KILICHOMTOA EXTRA BONGO NA KUHAMIA TWANGA PEPETA

Msanii wa siku nyingi katika kundi la extra bongo ambae kwa siku ya jumamosi alitambulishwa rasmi katika band ta twanga pepeta ameweka bayana kile kilichomtoa katika band hiyo na kuhamia twanga pepeta.
RAMA PENTAGON ambaye ameshiriki vyema katika albuma mbili za extra bongo kiwemo mjini mipango na mtenda akitendewa amesema kuwa ameondoka extra bongo kwa sababu ya kimaslahi kwa kuwa ameweza kukaa muda mrefu katika bannd hiyo ambapo alikua akilipwa kidogo lakini kutokana na mwenendo wa band inavyokwenda ndipo alipoamuia kumuomba mkurugenzi amuongezee kipato lakini majibu aliyoyapata hayakumridhisha ndipo  mkataba wake ulipoisha akaamua kujiunga na twanga pepeta ambapo alikua na mazungumzo nao kwa muda mrefu na kusema wamekubaliana vya kutosha na rasmi ataanza kazi na twanga hivi karibuni.

0 comments:

Post a Comment

.

.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...