KIMYA kingi na stori kibao mtaani juu ya kuingia mitini
na ‘mkwanja’ wa waigizaji wapya, hatimaye staa
kutoka tasnia ya filamu Bongo, Rose Ndauka kwa mara
nyingine ameibuka na kutupilia mbali taarifa kuwa
amekuwa akiitisha usahili kwa wasanii chipukizi na kuwachukulia fedha
kisha kutokomea kizani bila kuwashirikisha katika filamu zake.
Akizungumza na na cloudsfm.co mapema leo kufuatia uwepo wa habari kuwa kuna kundi la wasanii wamefika kwenye ofisi zake zilipo maeneo ya Kinondoni Jijini Dar kudai fedha zao baada ya kushinda usaili uliofanywa na Rose na kuambulia patupu pasipo kushirikishwa katika filamu yoyote ya msanii huyo.
“Sijawahi kuchukua fedha ya mtu na kumnyima nafasi, kinachotokea ni tatizo la wasanii kukosa uvumilivu kwani si rahisi kumchukua kila mtu aliyeshiriki na kushinda usahili na kumuweka kwenye filamu, tunachokifanya ni kutoa nafasi moja kutokana na kipaji halisi kisha wengine wanafuata, lakini ajabu naona wengine wanalalamika bila kuelewa lakini sijawahi kula hela ya mtu” alisema Rose.

0 comments:
Post a Comment