Mkurugenzi LHRC, Dkt Hellen Kijo- Bisimba
Asilimia
35 ya watoto chini ya miaka 18 nchini Tanzania wamefanyiwa vitendo
vya ukatili wa kijinsia ikiwa ni pamoja na kuolewa wakiwa na umri
mdogo hali inayochangia kushindwa kumu kutunza familia.
Akizungumza
jijini Dar es salaam,Mkurugenzi wa kituo cha Sheria na Haki za
Bianadamu,Dkt. Hellen Kijo-Bisimba amesema mkoa wa shinyanga
unaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya ndoa za utotoni kutokana na
baadhi ya mila na desturi za wakazi wa mkoa huo.
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa Mtandao wa Kupinga ndoa za utotoni TCEMN,
Justa Mwaituke amesema tatizo la ndoa za utotoni ni kubwa na
linaathiri maendeleo kwa watoto wanaoolewa wakiwa na umri mdogo.
0 comments:
Post a Comment