Mashirika
na Taasisi zisizo za kiserikali zinayohusika na masuala ya Ukimwi
yametakiwa kuimarisha ushirikiano ili kuweza kuleta mafanikio ya
kuhakikisha wanaufuta kabisa ukimwi Afrika mashariki.
Akizungumza
na wadau wanaowakilisha asasi zinazounda Mitandao inayojihusisha na
VVU na Ukimwi Kaimu Mratibu wa Tume ya Taifa yakudhibiti Ukimwi
Visiwani Zanzibar ALLY Mbrarouk Omary amesema kamwe vita dhidi ya
Ukimwi haitaisha kama hakuta kuwa na ushirikiano baina yao.
Kwa
upande wake Mwakilishi kutoka Mtandao wa mashirika yasiyo ya
kiserikali kutoka nchini Uganda yanayojishughulisha na masula ya
UKIMWI, Namanya Baram amesema mtandao wao wenye zaidi ya mika 18 sasa
una imani na Tanzania kama nchi kubwa wataweza kubadilisha uzoefu
katika masula ya kupambana na VVU, na UKIMWI.
0 comments:
Post a Comment