Naibu Waziri wa Elimu anaeshughulikia Elimu Mh.
Kassimu Majaliwa
Serikali
imesema kuwa Halmashauri ziache kuwatoza walimu kodi za mwezi katika
nyumba ambazo zinajengwa na serikali kwa kuwa lengo la serikali
kuwarahishia walimu kuweza kuishi karibu na maeneo ya Kazi na kufanya
kazi kwa ufanisi.
Tamko
hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Elimu anaeshughulikia Elimu Mh.
Kassimu Majaliwa na kusema kuwa Halmashauri zinazowakata walimu
mishahara yao kama kodi za pango za nyumba zilizojengwa na serikali
ni makosa Makubwa.
Mh.
Majaliwa amesema kuwa lengo la serikali kuzijenga nyumba hizo ni
kuwajengea mazingira mazuri ya ufundishaji walimu na kuweza kuwapa
urahisi wa kuhudhiria kazini ikiwa ni katika mpango wa kupata matokeo
makubwa sasa katika sekta ya Elimu.
0 comments:
Post a Comment