Mwenyekiti Baraza la Biashara Afrika Mashariki
Mwenyekiti
wa baraza la biashara la nchi wanachama wa jumuiya ya afrika
mashariki bw. Felexs Mosha amesema jitihada za kukabiliana
na tatizo la ajira kwa vijana wakiwemo wanaomaliza Vyuo
Vikuu zitakuwa na mafanikio kama serikali za nchi wanachama
zitakubali kuwa na mfumo shirikishi wa elimu na unaozingatia
mahitaji soko la ajira kwa sasa
Bw.
Mosha ameyasema hayo katika mkutano wa baraza hilo la
biashara na baraza la vyuo vikuu la afrika mashariki,
ulioandaliwa kwa ushirkiano na benki ya Maendeleo ya Afrika
Mashariki, unaofanyika Kigali, nchini Rwanda.
Katibu
mtendaji wa Baraza hilo Prf. Mayunga Nkunya amesema pamoja
na changamoto zinazowakaabili wahitimu wa vyuo vikuu katika
nchi za Afrika Mashariki uchunguzi umeonyesha kuwa wana uwezo
mkubwa wa kuleta mabadiliko kama mfumo uliopo utabadilika
0 comments:
Post a Comment