PROF. JUMMANNE MAGHEMBE
Idadi
kubwa ya wakazi wa Tanzania hasa waishio maeneo ya vijijini wapo
hatarini kuendelea kukosa maji safi na salama kutokana na kushindwa
kutunza vyanzo vya maji hali inayochangiwa na shughuli za binadamu.
Hayo
yameelezwa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Maji Profesa
Jumanne Maghembe wakati wa mkutano wa pamoja wa wadau wa sekta ya
maji, wenye lengo la kuangalia mafanikio yaliyopatikana katika awamu
ya kwanza ya utekelezaji wa mpango wa miaka sita katika sekta hiyo.
Profesa
Magembe amesema ni lazima serikali na wananchi kwa ujumla kutambua
hali hiyo na kuchukua hatua za makusudi kutunza rasilimali hiyo kwa
lengo la kuwa endelevu na amewataka wananchi kufuata sheria
zinazoelekeza namna ya kuhifadhi vyanzo vya maji.
0 comments:
Post a Comment