WAY

Wednesday, September 25, 2013

SALEHE KUPAZA ASIMAMISHWA KAZI TWANGA PEPETA HATARINI KUIKOSA BONANZA YA TWANGA NDANI YA MTWARA


MUIMBAJI mwenye sauti ya aina yake Salehe Kupaza , amesimamishwa kazi  na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya The African Stars  (ASET)  Asha Baraka ,inayomiliki bendi kongwe ya muziki wa dansi ya Twanga Pepeta International.
Kusimamishwa kazi kwa muimbaji huyo kunatokana na kosa la utovu wa nidhamu aliouonesha mbele ya Mkurugenzi wake.
Akizungumza na Bongoweekend  Asha alisema kwamba ametoa amri asimamishe ili kujifunza adabu mpakaatakavyoambiwa vinginevyo.
liongeza kwa kusema kwamba kumsimamisha kazi Kupaza ni njia mojawapo katika kumwonesha kwamba anawajibu wa kumuheshimu yeye kama Mkurugenzi wake.Kupaza amekumbana na kibano hicho baada ya kumtusi bosi wake ikiwa ni bada ya kuhojiwa juu ya uchelewaji kazini  kutoroka  mazoezini na kwenda katika mazoezi ya bendi ya Victoria  na kuomba kazi .Pia aliwatukana wanamuziki wenzake .Adhabu hiyo ameanza kuitumikia kuanzia Jumatatu Septemba 23  bada ya kizaazaa kilichotokea kwenye ofisi za ASET zilizopo Kinondoni jijini Dar es Salaam-

0 comments:

Post a Comment

.

.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...