WAY

Tuesday, September 17, 2013

BAADA YA KUTEKESEKA KWA MUDA MREFU NA MADAWA YA KULEVYA AISHA MADINDA AACHA UTEJA NA ARUDI TWANGA PEPETA IKIWEZEKANA KUWEPO KWENYE TOUR YA BONANZA LA TWANGA NDANI YA MAKONDE BAECH CLUB 29.9.2013


 Kutoka kulia aliyekuwa mnenguaji  nyota wa  bendi ya Twanga Pepeta Aisha Madinda na Mkurugenzi wake Asha Baraka  katika ofisi za ASET, zilizopo Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Aisha Madinda  akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi  Mtendaji wa ASET , Kampuni inayomiliki bendi ya Twanga Pepeta Asha Baraka 'Iron Lady', Kiongozi wa bendi Luiza Mbutu, Kushoto kwa Aisha ni Haji Ramadhani 'Haji BSS'  na Kalala Junior.

Aisha Madinda hivi sasa anajifua kwa mazoezi ya hali ya juu akijiwinda kurudi tena ulingoni ambako ameahidi kuwa atakuwa moto wa kuotea mbali , hiyo ni baada ya kutopea katika utumiaji wa dawa za kulevya ambazo hivi sasa amefanikiwa kuacha na kuwa akipata huduma katika kliniki ya watumiaji wa dawa hizo iliyopo katika Hospitali ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam.

Wakizungumza na Bongoweekend  katika nyakati tofauti wasanii wenzake kama Kiongozi wa bendi hiyo Luiza Mbutu 'Mamaa Brian' alisema kwamba wanashukuru mungu kwa kuona msanii mwenzao ameweza    kupambana na utumiaji wa dawa za kulevya na wanamkaribisha kwa mikono miwili kundini. Wakati huohuo Kalala Junior alisema kwamba "Kama nilivyotunga wimbo wangu wa Nyumbani ni Nyumbani' nasema Kurudi nyumbani siyo kosa hivyo jamii na wadau wampokee Aisha kwa mikono miwili.

0 comments:

Post a Comment

.

.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...