Wawakilishi
wa vijana kutoka Afrika mashariki pamoja na balozi wa vijana katika
jumuiya ya Madola
Vijana
katika nchi za Jumuiya ya Afrika mashariki wameanza kuonyesha hofu
yao,juu ya namna wanavyotumiwa na baadhi ya wanasiasa, wenye maslahi
binafsi katika kuleta machafuko, huku wakibainisha kutokuridhishwa na
mwenendo wa ushirikishwaji, katika masuala ya maendeleo na uchumi.
Wawakilishi
wa vijana kutoka Afrika mashariki pamoja na balozi wa vijana katika
jumuiya ya Madola kwa pamoja wamekutaka katika Kituo cha Maendeleo ya
Kimataifa cha MS TCDC-USA RIVER Arusha katika ushirikishwaji mpana
zaidi unaolenga kuwafanya vijana waweze kuwa sehemu ya kupanga na
kufanya maamuzi katika kuitengeneza Jumuiya.
Akizungumza
katika majadiliano hayo,Mkuu wa Wilaya ya Arusha Nyirembe Munasa
ameonya dhana ya kuwachukulia Vijana kama bomu linalosubiri kupasuaka
na badala yake wafikiriwe kama rasilimali inayoweza kuijenga Afrika.
Kwa
upande wake Mwakilishi wa Vijana kutoka nchini Kenya Noli Kaaya
amesema kuwa vijana wanaweza kuwa wawakilishi wazuri wa taifa katika
shughuli mbalimbali za kimaendeleo na uongozi katika kukuza uchumi.
0 comments:
Post a Comment