WAY

Thursday, November 20, 2014

SOMA HABARI HIZO KATIKA BLOG HII

 WANAWAKE WAMELETA MABADILIKO NCHINI- MAKINDA

Spika wa bunge kutoka Tanzania Anne Makinda amesema wabunge wanawake nchini  wamefanya kazi kubwa katika kuleta mabadiliko juu ya mtizamo wa watu kuhusu wanawake kwenye jamii.

Spika Makinda ambaye kwa sasa ni rais wa bunge la nchi za kusini mwa Afrika SADC amefafanua wajibu wa bunge hilo  Kwa kueleza kile kilichojadiliwa na kikao hicho cha maandalizi cha mkutano wa maspika kwa mwaka 2015.

Mh. Makinda amesema moja ya Agenda ambazo zitajaliwa katika vikao vya bunge hilo ni pamoja na kuona ni jinsi gani nchi zimefikia malengo ya milenia lakini pia na kuangazia masula ya Jinsia katika nchini Wanachama.
MWISHO


WAFUGAJI WATAKIWA KUISOMA KATIBA INAYOPENDEKEZWA
...................................
Wakulima  na  wafugaji   nchini  Tanzania  wameshauriwa   kuisoma  na  kuielewa   katiba  iliyopendekezwa   ili  ukifika  wakati   wa  kupiga  kura  wachukue  maamuzi   sahihi   badala  ya  kusubiri  kusomewa  na  wanasiasa majukwaani kwani asilimia  kubwa  wanasukumwa  na  maslahi   yao.

Akizungumza  na  wanachama  wa mtandao   wa  vikundi  vya   wakulima  Tanzania (MVIWATA)  Mkoa  wa  Arusha  Mkuu   wa  Wilaya  ya  Monduli  Bw,  Jowika  Kasunga  amesema  changamoto  nyingi  zinazoyakabili  makundi   hayo  ni  matokeo   ya kukosekana  kwa  uelewa  wa  kutosha  wakati   wa  kufanya  maamuzi   yanayowahusu.

Aidha  Bw.  Kasunga   amewataka   wadau  wanaosaidia  makundi  hayo   ukiwemo  mtandao  wa  (mviwata ) kuongeza  jitihada  za  kuwaunganisha  na  kuwaeleza  ukweli  juu  ya  masuala  yanayowahusu   hatua  itakayosaidia  kuziba  mianya  ya  watu wachache  wanaotaka  kuwatumia  kwa  maslahi  yao 

...................................
WATOTO 130,00 WANA VIRUSI VYA UKIMWI NA VVU NCHINI TANZANIA
Takwimu  zinaonesha kwamba watoto 1,30,000 wana maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI (VVU) Huku kati ya hao 39317 wamefikiwa na kupatiwa huduma ya dawa za kupunguza makali ya virusi hivyo.

Hayo yamesemwa jana na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dkt. Pindi Chana wakati akifungua kongamano la nne la kitaifa la  VVU na UKIMWI kwa watoto linalofanyika  katika Ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere uliopo jijini Dar-es-salaam.

Dkt . Chana alisema asilimia 39 ya watoto walio katika hatari ya kupata maambukii ya  UKIMWI hupimwa vipimo vya kubaini maambukizi ya VVU ndani ya miezi miwili baada ya kuzaliwa hivyo basi kuna  umuhimu kwa watoto hawa kupata huduma za tiba mapema.

Akizungumzia maambukizo ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto waziri huyo alisema Tanzania imepiga hatua katika kuzuia maambukizo kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto lengo likiwa  ni kutokomeza kabisa maambukizi mapya kwa watoto wachanga.
.....................................
MIRADI YA MENDELEO NCHINI KENYA NI NJIA YA KUKOMESHA UGAIDI
Naibu Mwakilishi wa kudumu wa Kenya kwenye Umoja wa Mataifa Balozi  Koki Muli Grignon amesema uanzishwaji wa miradi yenye lengo la kutokomeza umaskini ni mojawapo ya hatua za serikali za kukabiliana na vita dhidi ya ugaidi na misimamo mikali.

Akihutubia Baraza hilo wakati wa mjadala wa ngazi ya juu wa wazi kuhusu ugaidi, wapiganaji mamluki Balozi Muli amesema miradi hiyo inatekelezwa kupitia mamlaka za majimbo nchini Kenya kupitia mfumo wa ugatuaji madaraka.

Amesema ugatuaji wa matumizi ya fedha na uchukuaji wa maamuzi kwenye maeneo  husika ni msingi wa kutokomeza umaskini na tayari hatua hiyo ya  ugatuaji imejumuishwa kwenye katiba ya Kenya.

ZAIDI YA SERIKALI  100 ZIMEAHIDI KUZUIA UTAPIAMLO DUNIANI
…................................
Zaidi  ya  serikali 170 zimeahidi kuchukua  hatua zaidi  kuzuwia utapia  mlo  duniani, zikiidhinisha  kwa  hiyari  yao  misingi  ya kuhimiza  vyakula  vyenye  afya  na  kupunguza  viwango vya  unene kupita  kiasi  wakati wakianza  mkutano  wao  wa  siku  tatu ulioandaliwa  na  Umoja  wa  Mataifa.

Kwa  hivi  sasa , kiasi ya  watu  bilioni  mbili , ikiwa  ni  theluthi  ya watu wote  duniani, wanataabika  kwa  kukosa chakula  bora, ikiwa ni  pamoja  na  vitamini A, madini  ya  joto  na  zinki.

Ukosefu  huo  unasababisha  vifo  vya  asilimia  45  ya  watoto  wote waliofariki  mwaka  2013.

Wakati  huo  huo , kiasi  ya  watoto  milioni 42  chini  ya  miaka  5 wanauzito  wa  juu  na  kiasi  ya  watu wazima  milioni  500  ni  wanene  kupita  kiasi  katika  mwaka  2010 kwa  mujibu  wa  tarakimu  za  Umoja  wa  Mataifa.
....................................
WATU 10 WA FAMILIA MOJA WAMEUAWA NCHINI MISRI
Watu  kumi  wa  familia  moja  wameuwawa  usiku wakati  jeshi  la anga  la  Misri  liliposhambulia  nyumba  moja  katika  rasi  ya  Sinai kwa  makosa.

Watu  hao  kumi, ikiwa  ni  pamoja  na  wanawake watatu  na  watoto  watatu, wamefariki  walipofikishwa  katika hospitali  ya  al-Arish   katika  mji  mkuu  wa  jimbo  hilo. 

Majeshi ya Misri yamekuwa katika mlolongo wa  kampeni  za kupambana na makundi ya wapiganaji wa Jihadi tangu Agosti 2011katika eneo la jangwani linalopakana na Israe na  eneo la Palestina la Ukanda wa Gaza.
.............................
CCM WAITAKA SERIKALI KUWAWAJIBISHA WALIOSHINDWA KUVIENDELEZA VIWANDA
Chama  Cha Mapinduzi kimeitaka Serikali kuchukua hatua kali dhidi ya waliobinafshiwa viwanda nchini sanjali na kunyang'anywa viwanda hivyo na kurudishwa kuwa mali ya umma.

Katibu Mkuu wa Chama hicho Taifa, Bw. Abrahmani Kinana,inakuja mara baada ya kutembelea na kujionea,mlundikano wa korosho na msururu wa magari ya kisubili kupakuliwa,huku moja ya kiwanda cha kubangua korosho na ufuta kikigeuzwa ghala la kuifadhia vifaa vya kusambazaia umeme.

Bw. Kinana akihutubia kwenye mkutano wa hadhara katika mji mdogo wa Nachingwea Mkoani Lindi,ameitaka serikali kuwawajibisha viongozi au watumishi wa umma,ambapo amesema serikali haipaswi kuogopa watu wachache hasa wenye fedha na kuwacha mamilioni ya  watanzania waliowaweka madarakani wakitaabika.
TCCIA KIMEWATAKA WAFANYABIASHARA KULIPA KODI
.............................................
Chama cha wafanyabiashara wa viwandani na kilimo (TCCIA) kimetoa wito kwa wafanyabiashara kote nchini kuitumia vizuri wiki ya mlipa kodi inayoendelea nchini ili waweze kupata elimu ya kutosha kuhusiana na faida za kulipia kodi biashara zao kwa mustakabali wa Taifa.

Wito huo umetolewa leo na mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Dodoma, Fautine Mwakalinga wakati akizungumza na East Afrika Radio kuhusiana na faida za wiki ya mlipa kodi kwa wafanyabiashara nchini.

Mwakalinga amesema kuwa elimu inayotolewa na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kuhusiana na umuhimu wa kulipa kodi  ina faida kubwa kwa wafanyabiashara hata kwa wale ambao wanakwepa kulipa kodo kwani wakipata elimu ya kutosha wanaweza kuanza kulipa kodi kwa ajili kukuza uchumi wa Taifa.

Pia ametoa wito kwa jumuiya za wafanyabiashara kuhakikisha kuwa zinatatua matatizo yao na serikali kwa kukaa mezani na kuachana na migomo isiyokuwa na tija kwa taifa.

MUSWADA WA KUSANYAJI DATA ZA SIMU MAREKANI WAKATALIWA
Mswada  ambao  ungezuwia  ukusanyaji  wa  data  za  simu unaofanywa  na  shirika  la  usalama  wa  taifa  nchini  Marekani , NSA, umezuiwa  na  wabunge  mjini  Washington. 

Kura  hiyo  katika baraza  la  Seneti  ilikuwa  kura  58  za  ndio  na 42  za  hapana , ikiwa  ni  kura  mbili chini  ya  kura  60  zinazohitajiwa  kuupitisha mswada  huo.

Mswada  huo uliokataliwa  ungefikisha  mwisho  ukusanyaji  wa  data za  simu  za  mamilioni  ya  Wamarekani.   Wanaoupinga  wanasema ukusanyaji  wa  data  ni  muhimu  kwa  ajili  ya  juhudi  za  kupambana na  ugaidi.

Kiwango  cha  udukuzi  huo ulikuwa  miongoni  mwa  ufichuaji uliofanywa  na  mfanyakazi  wa  zamani  wa  shirika  la  NSA Edward Snowden.

0 comments:

Post a Comment

.

.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...