Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Usalama
Barabarani nchini Mohamed Mpinga
Jeshi
la Polisi nchini Tanzania Kikosi cha Usalama Barabarani,kimewasilisha
kanuni nne mpya za ukaguzi wa Magari nchini ikiwa ni sehemu ya
mkakati wa kukabiliana na Ongezeko la ajali za barabani hususani kwa
magari yanayosafirisha abiria nchini.
Wakati
akifungua majadiliano ya namna kanuini hivyo zitakavyosaidia
kukabiliana na ajali hizo,Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Usalama
Barabarani nchini Tanzania,Kamanda Mohamed Mpinga amesema kanuni hizo
zitasaidia kuyabaini magari ambayo yamechakaa kwa kutumia mfumo wa
kisasa.
Kwa
upande wake aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa nchi kavu
na Majini SUMATRA,Ahmad Kilima amesema kanuni hizo zitaponguza ajali
zisizo za lazima zinazosababishwa na uchakavu wa magari.
0 comments:
Post a Comment