•MAHAKAMA ya Rufaa Oktoba 30 mwaka huu inatarajiwa kusikiliza marejeo
ya hukumu iliyotolewa na mahakama hiyo katika kesi iliyokuwa ikimkabili
mwanamuziki Nguza Viki maarufu kama Babu seya na wanawe.
•Baada ya hukumu hiyo, Babu Seya na mwanawe pamoja na wakili wao Mabere Marando waliomba marejeo ya hukumu hiyo.
•Marejeo hayo yanatarajiwa kusikilizwa na Jopo la Majaji watatu wa
mahakama hiyo ambao ni Nathalia Kimaro, Mbarouk Mbarouk na Salum
Massati. Katika hukumu hiyo iliyotolewa Februari 2010,mahakama hiyo
iliridhia hukumu ya kifungo cha maisha kwa Babu Seya na mwanawe, Papii
Nguza huku ikimuwaachia huru watoto wawili wa Babu Seya, Nguza Mbangu,
na Francis Nguza.(A.M)
•Juni 25,
2004 Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kusutu, Dar es
Salaam,iliwatia hatiani Babu Seya na wanawe Papii Nguza, Papii Kocha,
Nguza Mbangu na Francis Nguza kwa kupatikana na hatia ya kubaka na
kulawiti.
Januari 27 mwaka 2005, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar
es Salaam, Thomas Mihayo alitupilia mbali rufaa yao iliyokuwa ikipinga
hukumu iliyotolewa na aliyekuwa Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu,Addy Lyamuya ambaye aliwatia hatiani kwa makosa yote
waliyokuwa wameshitakiwa nayo Juni 25 mwaka 2004.
•Babu Seya na
wanawe walidaiwa kutenda makosa 10 ya kubaka watoto wenye umri kati ya
miaka sita na minane na makosa mengine 11 ya kulawiti watoto wa kike
wenye umri huo huo kati ya April na Oktoba 2003 katika maeneo ya Sinza
kwa Remmy, Dar es Salaam.