WELCOME TO GMBONGO BLOG

To keep the body in good health is a duty... otherwise we shall not be able to keep our mind strong and clear.

TANGAZA NASI SASA

Tuwasiliane kwa Email: gmbongo.chuma@gmail.com

WE ARE HERE TO SERVE YOU

Keep you Entertained always

WE ARE HERE TO SERVE YOU

Habari na Burudani

WELCOME TO GMBONGO WORLD

Kwa habari za Burudani na zenye uhakika.

WAY

Friday, October 28, 2011

FATILIA PICHA ZA SHOW YA FM ACADEMIA KUSINI MWA TANZANIA -NDANI YA MTWARA




HIVI NDIVYO WAZEE WA NGWASUMA WALIPOFANYA BALAA LAO PALE MASASI NDANI YA BR NIGHT CLUB.
                                PATCHO MWAMBA TAJIRI AKIFANYA VITU VYAKE!
   MULE MULE FBI AKIKONGA MASHABIKI
                   NYOSHO ELSADAAT RASI WA FM ACADEMIA AKIFANYA VITU VYAKE.
 KUANZIA KUSHOTO KWENDA KULIA,TOSCANEE NZIMBU,DISPACH BUTELEZ,WATUNDA,NYOSHI ELSAADAT,MULEMULE,KING BLAISE,
           KALIJO MWANA KITOKORORO MAANA YAKE KUKU
        CHEKI WALIOUZA NA G.MBONGO KWENYE SHOW HIYO
     DISPACH BUTTELEZI NA G.MBONGO
             PATCHO MWAMBA TAJIRI NA G.MBONGO
    G.MBONGO NIKIWA NA MULE MULE FBI
  G.MBONGO NIKIWA NA NYOSHI EL SADAAT
   MIMI NIKIWA NA KING BLAISE NA KALIJO MWANA KITOKOLOLO.
                HII NDIYO ILIYOUZA ZAIDI NIKIWA NA CHEK DAR RAPER WA FM ACADEMIA

Tuesday, October 25, 2011

BABA NA MAMA YA DOGO RAMA SASA KIDEONI

  Video ya wimbo wa BABA NA MAMA wa dogo rama msanii wa tegemezi wa twanga pepeta sasa umekwisha kamilika hii ikiwa ni nyimbo ya 3 kufanyiwa kutoka katika album ya DOGO RAMA iliyopewa jina la KILIOMETA 10000 nyingine zikiwa ni CHUKI ZA NINI,IMANI YA MAPENZI,KILOMETA ELFU 10000 na sasa imekamilia ya BABA NA MAMA ambapo nyimbo hiyo amemshirikisha mwanana dada nguli wa miondoko ya dansi KHADIJA MNOGA KIMOBITEL,hii ikiwa ni katika kukamilisha mpango wake wa kutolea video nyimbo zake zote zilizo kwenye lbum yake hiyo mpya ambayo yupo mbioni kuizindua akiwa na wana kilometa ingawa bado hajabainisha ramsi ni lini ataizindua album hiyo na kuingia mtaani ila kiukweli mimi kama mdau ninayo ina rhumba za ukweli ambazo huwezi kuchoka kuzisikiliza hata kidogo.


                               DOGO RAMA JEMBE a.k.a VUALAAAAA
nyimbo nyingine zilizo katika album hiyo ni UZURI WANGU ambao amemshirika nguli mwingine kutoka twanga pepeta AMIGOLASI BABA NA SOPHII na nyingine ni SIRI YA MAPENZI ambayo amewashirikisha wakali wawili kutoka bnd tofauti ikiwa NI ROGERT HEGGA CARTAPILER WA EXTRA BONGO NA MWINGINE NI ERIC CANTONA MGOGO WA MAZIZINI KUTOKA DIAMOND MUSICA VIJANA CLASSIC

                               JEMBE IN ACTION DOGO RAMA!

Sunday, October 16, 2011

UNALIJUA JEMBE LA EXTRA BONGO KWENYE DRUMS?

                         MARTIN KIBOSHO
Kiumri ni kijana mdogo sana lakini ana jina kubwa na ana mambo makubwa sana katika muziki wa dansi tanzania baada yakusimama na band nyingi sana ncchini tanzania.
Alizaliwa mnamo mwaka 1985 huko mkoani kilimanjaro akiwa ni mchanganyiko wa mchanga na mbena wa iringa
 Rasmi kwenye muziki aliingia mnamo mwaka 2001 akiwa kama mcheza sarakasi na mpiga ngoma katika kikundi cha MUUNGANO CULTURE TROUP  ambapo hapo alikuwa na wakli wa sarakasi kipindi hicho wakina TUPATUPA,KILIAN,MOSHI MKALI,MUSA ambaye sasa anafanya shughuli zake za sanaa ndani ya jiji la LONDON-UINGEREZA na hapo muun gano ndipo alipopatamwalimu wa kupigangoma am drums kwa lugha iliyozoeleka kwa wana band wengi. katika kijipima kama amefuzu upigaji wa drums kuotka kwa mwalimu wake huyo martin
 alijiunga na band ya TANGO STARS akiwa na mkongwe mlemavu mwenye uwezo wa hali ya juu ANANIA NGOLIGA hiyo ikiwa ni mwaka 2004.
           MKALI MARTINI KIBOSHO AKITAFAKARI JAMBO KITAA
Mwaka 2005 aliweza kujiunga na band ilyokua chini ya aset chini ya mkugurugenzi iron lady ASHA BARAKA katikaband iliyokua inajulikana kama AFRICAN REVOLUTION WANA TAM TAM hapo ikiwa katika jina jipya baada ya lile la african revolution wanachumvi chumvi so marin kibosho  alikua na kina BADI BAKULE,WAZIRI SONYO, ambapo aliweza kupiga katika nyimbo mbili tu kutokana na uchanga aliokua  nao kipindi hicho!

          MARTIN KIBOSHO MZIGONI AKING'UTA DRUMS KIHATARI HATARI

 Mwaka 2006 aliweza kujiunga na band iliyotikisa sna kipindi hicho iliyokua chini ya kiongozi wake Kamarade ALLY CHOKI, kipindi hicho ikiitwa EXTRA BONGO 3*3 lakin baadae band hiyo ikafa lakini wakaunganisha band moja kwa mbili na martin aliendelea kuwa mpiga drums wao ni EXTRA BONGO NA DOUBLE M SOUND  wakajiunga na baada ya hapo ikaitwa DOUBLE EXTRA viongozi ama wakurugenzi wa band hiyo wakiwa ni ALLY CHOKI NA MUUMIN MWINJUMA ambapo hapo waliweza kutoa album moja ambayo hata hivyo haikufanya vizuri sana sokoni

         KAZI NA DAWA SI UNAJUA DRUMS KAZI YAKE HAPA ANATUPIA KITU CHA MSOSI
Mwaka 2007 alijiunga na band ya MCHINGA GENERATION iliyokua chini ya mh MUDHIHIR MUDHIHIR hapo alipiga MWAKA WA TABU na NGUZO TANO na mwishoni mwa mwaka huo huo aliweza kwenda kujiunga na bandya twanga chipolopolo iliyokuna na le GENERAL BANZA STONE NA KINA MSAFIRI DIOF ambapo hapa aliweza kuandaa nyimbo moja iliyoitwa hujafa hujaumbika.


                              MARTIN KIBOSHO AKIZIKAANGA CHIPS LAZIMA UCHEZE
   Mwaka 2008 aliweza kupata deal ya kwenda kupiga nchini SAUDI ARABIA pale DUBAI ambapo hapo aliunda band yake aliyoiita THE ROUTE BAND akiwa na kina GOD KANUTI,HOSEA,SUPER K,SUZY CRAZY na wengineo na baada ya kuisha kwa mkata wake huko ndipo aliporudi tena bongo na kungana tena na wana EXTRA BONGO NEXT LEVEL WAZEE WA KIZIGO ambapo aliikuta album ya MJINI MIPANGO ikiwa jikoni ambapo alipata nafasi ya kupiga nyimbo ya FIRST LADY ambayo ilikua ni utunzi wake ALLY CHOKI kibabu cha loliondo 
Lakini MARTIN KIBOSHO amesharekodi nyimbo nne kati ya sita zitakazo patikana katika album mpya ya extra bongo ambayo bado haijapewa jina huku ikiwa inatamba na nyimbo mbili radioni MTENDA AKITENDEWA NA WATU NA FALSAFA ZA MAISHA
 MARTIN aaanasema mvuto wake wa kupiga drums ulikuwa kutoka kwa mwalimu wake wa kipindi hicho JIMMY KIBELO,NA PETIT MAKAMBO

    MARTIN KIBOSHO a.k.a MUUZA SURA AKIFANYA VITU NA WAZEE WA KIZIGO
           FOR MORE ADVICE  KWA MARTIN KIBOSHO NI kiboshodrama@yahoo.com








Saturday, October 15, 2011

MJUE SHARO BARO ANAETIKISA NDANI YA EXTRA BONGO-RAMA PENTAGONE

              RAMA PENTAGONE
 alizaliwa mnamo mwaka 1979 ambapo alizaliwa na kusomea elimu yake hadi kidato cha nne katika jiji la mwanza
 Rasmi alianza kujiingiza katika tasnia ya muziki mnamo miaka ya 2000 akianzia katika band ya magereza  MAGEREZA BAND kipindi hicho wanapiga bwaloni magereza
mwaka 2004RAMA PENTAGONE alijiunga na band ya DOUBLE M a.k.a WANAMSHIKEMSHIKE kipindi hicho ikiongozwa na kocha wa dunia ambapo hapo aliweza kushirika katika album mbili zilizotolewa na band hiyo kipindi hicho ikiwa ni ile ya CALL BOX ambapo nadni ya album hiyo aliweza kushiriki nyimbo mbili tu lakini album iliyofata ya TITANIC aliweza kushiriki nyimbo zote za album hiyo 
                             RAMA PENTAGONE MI NAPENDA KUMWITA SHAROBARO
Mwaka  2005 DOUBLE M iliweza kujiunga na bad nyingine ya SERENGETI BAND ambapo hapo ikaitwa SERENGETI MSHIKEMSHIKE wakati huo akiwa nawatu kama AMOROSO ambaye kwa sasa ni producer,RASHID SUMUNI,AMINA NGALUMA,KASSIM RASHID,KAWANINGA,JUMA KATUNDU  na wengineo!
  mwaka 2007 aliweza kurudi home city Mwanza na akajiunga na ban ya CARNIVAL ya jijini mwanza ikijulikana kama TAIFA STARS wakati huo akiwa na kina ALLY YAHYA,PETIT MAKAMBO,ROGAROGA,SEBA  huku ikiongozwa na mkongwe BENO VILLA ANTONY

            RAMA PENTAGONE AKIONYESHA MAVOCAL
Mwaka 2008 aliweza kujiunga na band ya MILE  LEVENT MUSICA ambapo hapo aliweza kushiriki kutoa album ya MAMA KABIBI  hukuakindika nyimbo kama MCHAKATO,LIFE JACKET na wakati huo akiwa nakina RICH MAARIFA,BOB KISSA,ATANAS NA SUZUKI
  Mwaka 2009 alijiunga rasmi na EXTRA BONGO NEXT LEVEL WAZEE WA KIZIGO ambapo aliwezac kusimama vyema kwenye album ya kwanza ya MJINI MIPANGO  aidha rama pentagone anatarajia kutoa album nyingine akiwa na wa extra bongo huku akitarajikuweka nyimbo yake ya jeolus

         RAMA PENTAGONE AKIWA NA WANA EXTRA BONGO
   RAMA PENTAGONE  kuandaa album yake binafsi  ikiwa na nyimbo kama NJIA PANDA,CHINI YA MTI,AZIZA,MKE WA MWENZIO USIMNONG'ONEZE SIKIO, aidha rama amesema mashabiki na wapenzi wa EXTRA BONGO wategemee makubwa kutoka kwake kwa kuwa anaamini ni mmoja kati ya wanamuziki wenye vipaji vya hali ya juu hapa Tanzania na mm nasaport hilo!
 kwa ushauri wowte juu  ya dogo rama mtafute kupitia 0713-541508 

                             RAMA PENTAGONE SHARO BARO NA MUREMBO RAHMA
 

.

.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...