WAY

Sunday, October 16, 2011

UNALIJUA JEMBE LA EXTRA BONGO KWENYE DRUMS?

                         MARTIN KIBOSHO
Kiumri ni kijana mdogo sana lakini ana jina kubwa na ana mambo makubwa sana katika muziki wa dansi tanzania baada yakusimama na band nyingi sana ncchini tanzania.
Alizaliwa mnamo mwaka 1985 huko mkoani kilimanjaro akiwa ni mchanganyiko wa mchanga na mbena wa iringa
 Rasmi kwenye muziki aliingia mnamo mwaka 2001 akiwa kama mcheza sarakasi na mpiga ngoma katika kikundi cha MUUNGANO CULTURE TROUP  ambapo hapo alikuwa na wakli wa sarakasi kipindi hicho wakina TUPATUPA,KILIAN,MOSHI MKALI,MUSA ambaye sasa anafanya shughuli zake za sanaa ndani ya jiji la LONDON-UINGEREZA na hapo muun gano ndipo alipopatamwalimu wa kupigangoma am drums kwa lugha iliyozoeleka kwa wana band wengi. katika kijipima kama amefuzu upigaji wa drums kuotka kwa mwalimu wake huyo martin
 alijiunga na band ya TANGO STARS akiwa na mkongwe mlemavu mwenye uwezo wa hali ya juu ANANIA NGOLIGA hiyo ikiwa ni mwaka 2004.
           MKALI MARTINI KIBOSHO AKITAFAKARI JAMBO KITAA
Mwaka 2005 aliweza kujiunga na band ilyokua chini ya aset chini ya mkugurugenzi iron lady ASHA BARAKA katikaband iliyokua inajulikana kama AFRICAN REVOLUTION WANA TAM TAM hapo ikiwa katika jina jipya baada ya lile la african revolution wanachumvi chumvi so marin kibosho  alikua na kina BADI BAKULE,WAZIRI SONYO, ambapo aliweza kupiga katika nyimbo mbili tu kutokana na uchanga aliokua  nao kipindi hicho!

          MARTIN KIBOSHO MZIGONI AKING'UTA DRUMS KIHATARI HATARI

 Mwaka 2006 aliweza kujiunga na band iliyotikisa sna kipindi hicho iliyokua chini ya kiongozi wake Kamarade ALLY CHOKI, kipindi hicho ikiitwa EXTRA BONGO 3*3 lakin baadae band hiyo ikafa lakini wakaunganisha band moja kwa mbili na martin aliendelea kuwa mpiga drums wao ni EXTRA BONGO NA DOUBLE M SOUND  wakajiunga na baada ya hapo ikaitwa DOUBLE EXTRA viongozi ama wakurugenzi wa band hiyo wakiwa ni ALLY CHOKI NA MUUMIN MWINJUMA ambapo hapo waliweza kutoa album moja ambayo hata hivyo haikufanya vizuri sana sokoni

         KAZI NA DAWA SI UNAJUA DRUMS KAZI YAKE HAPA ANATUPIA KITU CHA MSOSI
Mwaka 2007 alijiunga na band ya MCHINGA GENERATION iliyokua chini ya mh MUDHIHIR MUDHIHIR hapo alipiga MWAKA WA TABU na NGUZO TANO na mwishoni mwa mwaka huo huo aliweza kwenda kujiunga na bandya twanga chipolopolo iliyokuna na le GENERAL BANZA STONE NA KINA MSAFIRI DIOF ambapo hapa aliweza kuandaa nyimbo moja iliyoitwa hujafa hujaumbika.


                              MARTIN KIBOSHO AKIZIKAANGA CHIPS LAZIMA UCHEZE
   Mwaka 2008 aliweza kupata deal ya kwenda kupiga nchini SAUDI ARABIA pale DUBAI ambapo hapo aliunda band yake aliyoiita THE ROUTE BAND akiwa na kina GOD KANUTI,HOSEA,SUPER K,SUZY CRAZY na wengineo na baada ya kuisha kwa mkata wake huko ndipo aliporudi tena bongo na kungana tena na wana EXTRA BONGO NEXT LEVEL WAZEE WA KIZIGO ambapo aliikuta album ya MJINI MIPANGO ikiwa jikoni ambapo alipata nafasi ya kupiga nyimbo ya FIRST LADY ambayo ilikua ni utunzi wake ALLY CHOKI kibabu cha loliondo 
Lakini MARTIN KIBOSHO amesharekodi nyimbo nne kati ya sita zitakazo patikana katika album mpya ya extra bongo ambayo bado haijapewa jina huku ikiwa inatamba na nyimbo mbili radioni MTENDA AKITENDEWA NA WATU NA FALSAFA ZA MAISHA
 MARTIN aaanasema mvuto wake wa kupiga drums ulikuwa kutoka kwa mwalimu wake wa kipindi hicho JIMMY KIBELO,NA PETIT MAKAMBO

    MARTIN KIBOSHO a.k.a MUUZA SURA AKIFANYA VITU NA WAZEE WA KIZIGO
           FOR MORE ADVICE  KWA MARTIN KIBOSHO NI kiboshodrama@yahoo.com








1 comment:

.

.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...