WAY

Monday, October 3, 2011

Je unamfahamu ROGERT HEGGA a.k.a CARTAPILA a.k.a KILIMANJARO TANZANIA?

                       HUKU NDIKO ALIKOTEKA  ROGERT HEGGA (CATAPILA)
ROGERT HEGGA alizaliwa katika miaka ya 1973 jijini Dar-es-salaam na kusoma shule ya msingi na kumaliza na hatimaye alijunga na chuo cha ufundi Dar-salaam DAR TECH
   Rasmi rogert alijiinga katika muziki mnamo mwaka 1987 kwa kuimba kwaya kanisani,
baada ya hapo mwaka huo huo wa 1987 alijunga na band iliyoitwa SAFARI BAND mwenyewe akiita band ya mtaani wakati huo katika band alikuwa na mchekeshaji maarufu katika tasnia ya uigizaji KINGWENDU NGWENDULILE ambapo alidumu na band hiyo ya safari mpaka mwaka
       1989 ambapo alijunga na band nyingine iliyokua inajulikana kama CITY SOUND ambapo alikutana na mkonge wa muziki wa kiafrica toka south Africa TABOO nadhani wafatiliaji wa muziki wa dansi  watakua wanamkumbuka taboo
 Baaday ahapo mwaka 1992 alijiunga na band ya kipindi hicho iliyoanzishwa mwishoni mwa miaka ya tisini na kina kamarade ALLY CHOKI band ya BANTU GROUP lakini wakati ROGGERT  anajiunga na band hiyo tayari inaesemekana ni muasisi wa band ya bantu group KOMANDOO HAMZA KALALA ndio alikua amejiunga na band hiyo ambayo roggert alidumu nayo mpka mwaka 1995
       lakini maka wa 1995 ROGGERT alifanikiwa kutoa album yake mwenye kama kazi binafisi(SOLO ARTIST) huku akiwa na kundi lake dogo la AFRI GENERATION wakati huo akiwa ametokea nchini ZIMBABWE ambako alikwenda kufanya kazi hiyo hiyo ya muziki wa dansi
 album hiyo ambayo aliipa jina la MAMA RADHIA ambacho ni moja ya kibao ambacho kilimtambilisha vilivyo rogert hegga nyimbo nyingine zilizopatikana katika album hiyo ni ASMA,SINTO KATA TAMAA,THEO MAZIMBABWE,
        Mwaka 1997 roggert alijiunga na band ya MASAI BAND ambayo ilikua na maskani yake pale kijitonyama jijini DAR-ES-SALAAM kipindi hicho akiwa na kina YAHAYA MKANGO,JOHN MPONI, ambapo hapo alidumu kwa muda wa mwaka mmoja tu na hatimaye
        Mwaka 1998 alijiunga na band ya TWIGA BAND ilyokua na maskani yake mwananyamala ambapo hapo alikutana na mtu mmoja maarufu sana CHE MUDUNGWAO, pamoja na JOHN MPONI ambapo hakudumu sana.
   

                                 CARTAPILLER ROGGERT HEGGA

Mwaka 1999 alijiunga  na band ya AFRICAN STAR kabla haijapewa jina la TWANGA PEPETA
ambapo hapoa likutana wanamuziki mbali mbali akiwemo LE GENERAL BANZA STONE,LUIZA MBUTU kipindi hicho akiitwa LIUZA NYONI,AMIGOLASI,YAHYA MKANGO,JOSEPH KANUTI,DEO MWANAMBILIMBI,MICHAEL LILOKO,BOB GAD WILLIUM,JESCA CHALS,MAREHEM ABUU SEMHANDO kipindi hicho ilikua ni HOTEL BAND ambayo ilikua ikipiga pale BAHARI BEACH lakini walifanikiwa kutoa album moja ya KISA CHA MPEMBA ambapo ndani yake kulikuan nyimbo moja ambayo ni utunzi wake roggert FADHILA KWA WAZAZI NO. 01 hata hivyo hakumaliza mwaka na african star mwisho mwa
         Mwaka 1999 alitimkia nchini KENYA katika jiji la NAIROBI katika band moja iliyojulikana kama BENGA INTERNATIONAL ambapo hapo alikutana na wanamuziki nguli kwa sasa kama MUUMINI MWINJUMA,RASHID SUMUNI,hakudumu sana katika band hiyo na baadae kutimkia katika mji wa KISUMU ambapo hapoa pia likutana na mtu kama kamarade ALLY CHOKI ambae alikua kiongozi kwenye Band iliyoitwa EXTRA KIMWA ambapo hapo vile vile kulikupwepo na mpiga gita maarufu tanzania kwa sasa EPHRAIM JOSHUA  NA MTOTO  WA KING MAJUTO ATHMAN MAJUTO, ambapo hapo alikaa kwa muda kidog na baandae kurejea tena tanzania,
              mwanzoni mwa mwaka 2000 alitua tena AFRICA STAR ambapo aliikuta album ya pili ya twanga pepeta JIRANI ikiwa jikoni na yeye kuweza kupata kushiriki katika kuimba katika nyimbo zilizokuwemo katika album hiyo ambayo ilatakiwa kuitwa AUNGURUMAPO SIMBA lakini kabla haijamalizika kiongozi wa wakati huo banza stone aliondoka na ndipo ali choki alipewa jukumu la kuandika nyimbo itakayobeba jina la album 
                 Safari ya roggert haikuishia hapo mwaka huo huo wa 20000 mwishoni alijitoa yeye na wenzake na kwenda kuanzisha band ya MCHINGA SOUND ambapo alikutana na wenzake kina ADOLPH MBINGA,MWIJUMA MUUMIN,JOSEPH WATUGURU,MOSHI MSELELA,GODFREY KANUTI,MICHAEL LILOKO,SELEMAN BONGO napo hakudumu sana katikati ya mwaka 2001 akajiunga tena african stars ambapo alidumu sasa kwa muda na kuweza kutoa nao album za
 2001-fainali uzeeni 2002-chuki binafsi-ambapo alitunga nyimbo ya LA MGAMBO 2003-ukubwa jiwe-2004 mtu pesa ambapo ndani ya album hiyo alitunga nyimbo ya FAMILY COMFLICT
              
            ROGERT HEGGA CARTAPILER a.k.a KILIMANJARO AKIWA NA  TWANGA

 Baada ya hapo mwaka 2004 roggert akatoka tena african stars na kujiunga tena na mchinga lakini safari hii ikiitwa MCHINGA GENERATION AU G8 ikiundwa na kina kamarade ALLY CHOKI,RASHID MWENZINGO,MUSEMBA MINYUNGU,OMARI SESEME,KALALA JOUNIOUR,SAULO FERGASON,ATHMAN MAJUTO,GOD KANUTI,BONZO KWEMBE,AMOUR ZUNGU,
  Ambapo hapoa aliweza kutoka album mbili akiwa na band hiyo ambazo ni 2005 NAFSI-2006 MWAKA WA TABU na aliweza kukaa mchinga generation mpka mwaka
      2008 Alijiunga na T.O.T PLUS wana achimenengule ambayo ilikua chini ya kocha wa dunia MUUMUNI MWINJUMA ambapo hapo aliweza kuandika nyimbo ya CHEUPE SANDRA na baada ya hapo mwaka 2009 band ikabadilishwa jina na kuitwa T.O.T RESPECT hapo ilikua chini ya mzee wa kijiko kamarade ally choki.

                                      LUIZA MBUTU NA ROGGERT WAKICHAPA KAZI

mwaka 2010 alirudi tena TWANGA PEPETA na sasa ivi inaitwa TWANGA PEPETA INTERNATIONAL ambapo hapo ailifanikiwa kutoa albm moja ambayo inaitwa MWANADAR-ES-SALAAM ambapo ndani kuna nyimbo ya RAFIKI ADUI ambayo ni utunzi wake mwenyewe roggert
     na mwaka 2011 alihamia band yenye wanamuziki nguli wa siku nyingi na inayofanya vizuri katika tasnia ya muziki wa dansi ambayo ipo chini ya mkurugenzi mtendaji ally choki EXTRA BONGO NEXT LEVEL a.k.a WAZEE WA KIZIGO ambapo hapo ametunga nyibma ya UFISADI WA MAPENZI ambao utakuwepo kwenye album ambayo bado haijapewa jina na yeye yupo kama kiongozi wa band na hapo anaunga na wanamuziki LE GENERAL BANZA STONE,RAMA PENTAGONE,ATANASI,ALLY CHOKI MWENYEWE,SUPER NYAMWELA, AISHA MADINDA na wengine kibaoooooooooooooooo
                     FUNDI ANAYETAMBA KATIKA TASNIA YA MUZIKI WA DANSI SASA    
           
                     ROGGERT AKIWA NA WANA EXTRA BONGO

   ROGGERT,BANZA NA ALLY.


ROGGERTHEGGA  a.k.a CARTAPILAa.k.a                                     KILIMANJARO TANZANIA.   


 

0 comments:

Post a Comment

.

.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...