WAY

Saturday, October 1, 2011

MJUE FUNDI SELEMARA,MPIGA DEBE,MTAALAM WA NGOMA ZA DAKU NA MCHIRIKU SASA NI LULU KATIKA MUZIKI WA DANSI!

   LE GENERAL BANZA STONE a.k.a MWALIMU
    Alizaliwa mnamo mwaka 1972
Rasmia le general BANZA STONE alianza muziki yeye anauitwa wa ukweli mnamo mwanzoni mwa miaka ya 90 ambako alikuwa akisomea muziki katika chuo cha cha sanaa KOREA CULTURAL MUSIC CENTRE na wakati huo pia alikua akishughlika na uchezaji show nikiwa na maana dansi kama walivyokua wakina marehem BLACK MOSES,marehem MAX, na banza nae alikua napitia humo humo lakini
 mwaka 1992 aliingia rasmi katika fani ya uimbaji pale alipojiunga na ya THE HEART STRESS BAND ambayo ilikua ikijihusisha zaidi kupiga muziki kwenye mahotel toafauti tofauti yaan ni hotel band ambako alikaaa kwa muda wa miaka kadhaa ambapo baada ya hapo
    1994 alijiuga na band nyingine ya hotel iliyokuwa ikiitwa AFRISUEZ lakini utofauti wa band hii walikua wakipiga nyimbo mchnanyiko yaani copy na nyingine walizotunga wao hapo ndipo BANZA STONE alipoandika nyimbo yake yakwanza ambayo ilikua kwenye staili ya dansi ambayo alikuja kuirudia baadae katika band ambayo nakutaka uendelee kunifatilia utaijua band gani, nyimbo alioitunga akiwa afrisuez iliitwa KUMEKUCHA lakini hata hivyo hakuwahi kurekodi nyimbo hiyo na kipindi hicho band hiyo ilikua ikipiga mahotelini kama kawaida alikaa afri suez kwa muda wakati huo alikua akiendelea na kazi yake ya ufundi selemara akiwa na mshkaji wake wa karibu lakini 
    Mwaka 1998 le general Banza stone ambaye jina lake la kuzaliwa ni ramadhani masanja asili yake ikiwa ni msukuma wa shinyanga lakini aliekulia jijini DAR-ES-SALAAM alihamia band ambsayo ilikua ikipiga hotel vile vile kwa wakati huo AFRICAN STARS na kama watu walikua hawajui siri ya twanga pepeta basi le general ndio muasisi ya jina la TWANGA PEPETA kwani zamani ilijulikana kama african stars 
   
                               ENZI HIZO LE GENERAL BANZA STONE MWALIMU WA WALIMU
Mwaka 1999 banza aliweza kukirudia kibao chake alichokitunga afrosuez cha kumekucha na kuitoa bana hyo kutoka kwenye kupiga kwenye mahotel na kuanza kupiga katika kumbi mbalimbali akiwa na wanamuziki wenzake kibao wa wakati ndio walikuwa wakiunda african stars  LUIZA MBUTU,JESCA CHARLES,AMIGOLASI,ALDOPH MBINGA,MAREHEMU ABUU SEMHANDO,MCD na ndipo walipofyatua album yao ya kwanza ikibeba jina la KISA CHA MPEMBA ukiwa ni utunzi wake LE GENERAL BANZA STONE 
    Mwaka 2002 wakati wanajiandaa kutoa album yao ya pili ambayo tayari ilishapewa jina la AUNGURUMAPO SIMBA kibao ambacho kilitungwa na banza stone alichomoka kutoka african stars ambapo albm hiyo ilipewa jina jingine na banza akajiunga na band ya T.O.T PLUS(wanaachimenengule)  ambapo alikutana na kina TOTO TUNDU,ABDUL MISAMBANO hapo aliweza kutoa album ya kwanza iliyotikisa na wimbo wa MTAJI WA MASIKINI na ndio uliobeba jina la album lakini ndani ya album hiyo kulikua na nyimbo kamatushirikiane na mwngine  uliitwa jahazi zote zikiwa ni utunzi wake banza stone
   Mwaka 2004 banza tena akiwa na kina ley chinyama ambae alipiga gita la solo na bado akiwa na t.o.t plus aliibuka na ELIMU YA MJINGA ambayo nayo ilibeba jina album 
   Mwaka 2005 banza tena akiwa bado na wana t.o.t aliweza tena kutoa remix vision ya AUNGURUMAPO SIMBA  VOL 2 na ndio ikabeba jina la album tena humo kukiwa na nyimbo iliyotikisa kwa kipindi hicho KWA HERI wakati huo akiwa na WAZIRI SONYO,TOT TUNDU, NA ABDUL MISAMBANO.
 

   LE GENERAL BANZA  AKICHAPA KAZI NA MSAFIRI DIOF SOKOINE
Na mnamo MWAKA 2004 aliibukia katika bend  ya africa stars hapa jina la TWANGA PEPETA likiwa limesha komaa toka alipokua muasisi wakati linaanza na hapo aliibuka na kitu cha MTU PESA ambacho kilitikisa uliwngu wa dansi Tanzania na sio bongo tu hadi kiliweza kuchukua tuzo ya BBC AWARD kama nyimbo bora ya dansi na vile vile yeye mwenye kuibuka BEST MALE VOCALIST kwenye KILI AWARD za mwaka 2005 kutokana na kibao cha mtu pesa kufanya vizuri na album kupewa jina la MTU PESA lakin mwaka huo wa 2005 na tano akahamishiwa band Tanza ya african revolution ili kuongeza nguvu baada ya aliekua akiiongoza band hiyo muumini mwinjuma kujotoa na kuanzisha band yake wakati huo band ya african stars akirudishwa ALLY CHOKI kutoka mchinga sound 
    Mwaka huo 2005 alifanikia kushiriki kwenye album ya safari 2005  ya twanga chipolopolo baada ya hapo akatengeneza band yake mwenyewe aliyoipa jina la BAMBINO SOUNG wakati huo akiwa na kina KALALA JUNOUR,ATNASI,BOB KISA,
 baada ya hapo mwaka 2006 mwishoni wakaunda band ya mafahari watatu ambao walikua ni yeye mwenyewe LE GENERALY BANZA STONE.ALLY CHOKI,NA MUUMINI MWINJUMA,

kutoka kushoto khadija mnoga kimobilte,ally choki banza stone,muumini mwinjuma enzi za mafahari.

lakini band hiyo haikudumu sana ndipo ally choki akatoka na kuanziah band yake na muumin kuunda band yake lakini na yeye kurudi bambino
 lakini mwaka 2007 mwishoni hadi 2009 akapata matatizo ya kiafya kwa takribani miaka miwili na hatimaye mwaka 2009 aliweza kurejea kidogo na kupata afueni na kuanza tena shughuliza muziki na kuibuka tena na band yake ya BAMBINO SOUND




                         LE GENERAL BANZA STONE a.k.a MAKAVELI

lakini hakuweza kukaa sana na band yake hiyo na
   mwaka 2010 alijuinga na band ya RUFITA CONNECTION ambapo alikuwa nao mpaka
    20011 akajiunga na band mbayo inatikisa sasa EXTRA BONGO ambapo ameungana na mwanmuziki  mweznie nguli ambaye pia ndie mkurugenzi wa band hiyo ally choki na mtuzni wa siku nyingi Roggert hegga cartapilla!
     Le General banza stone  wa kwanza kulia akiwa mzigoni na wana extra bongo.

     








1 comment:

.

.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...