WAY

Thursday, June 28, 2012

WASANII WA ZAMANI WA CHUCHU SOUND NA SASA WAKO MACHOZI BAND WAKANA KUIREJESHA CHUCHU SOUND NI MAO SANTIAGO NA JONIKO FLOWER

Wakiongea na g mbongo kwa nyakati tofauti MAO SANTIAGO  ambae alishawahi kutamba sana na bend ya chuchu sound iliyokua ikipiga mitindo maridhawa ya chakacha na mduara kipindi hicho wakiwa na kina OMARY MKALI, aABABUU MWANA ZANZIBAR,YUSUPH CHUCHU  mwenyewe JONIKO FLOWER ,KING JOVANII, na wengine kibao inasemekana walirejea tena chuchu sound siku ilipozinduliwa band mpya ya muziki wa taarabu MANUARY MORDEN TAARAB lakini pia walieweza kwenda kupiga tena katika uwanja wenye mashamu shamu mengi ambao unatikisa jjiji kwa sasa DAR LIVE
Kwa mujibu wa mao santiago alisema kuwa wao walijiita wasani waliokua chuchu zamani ili kujikumbushia zile za zamani zilizoweza kutamba kama vile USIONE VYAELEA,CHANUO,UTAMU WA NDIZI na nyingine nyingi ambazo waliwahi kutamba nazo wakiwa chuchu sound kwa hiyo wao sio kwamba wamerudi chuchu sound au wameirejesha chuchu sound ila waliitwa na watu waliokuwa wanataka ladha ya chuchu sound kwa hiyo yeye kama mao santiago ataendelea kubaki machozi band mpaka hapo atakaposema yeye mwenyewe kuwa anahama lakini sio kwa mtu yoyote kusema kuwa anahama na sasa pia yuko mbioni kutengneneza wimbo mpya atakaorekodi akiwa na machozi band huku akisema kurekodi solo project kwa sasa bado kwa sababu tu hajapata msimamizi wa kuweza kuzisimamia kazi zake

 Lakini pia kwa upande wake msanii nguli mwenye sauti ya gharama na kali sana JONIKO FLOWER nae amesema yeye aliombwa tu kwenda kuimba na band hiyo lakini sio kwamba amerudi chuchu sound lakini pia yeye kama yeye baada yakumaliza album ya machozi band ambayo wako mbioni kuikamilisha yuko mbioni kutengeneza albm yake binafsi ile kuleta ladha ile wanayoitaka mashabiki wake huku akisema album yake atapiga karibu kila aina ya muziki lakini wakiafrica zikiwemo RHUMBA,CHAKACHA,SEBENE,MIDUARA,MDUNDIKO na nyingine kibao kwa hiyo mashabiki wake wakae mkao wa kula lakini pia akiwa na machozi band wamekwisha kamilisha wimbo wake mpya lakini sasa anasuburi nyimbo za wengine zikamillike ili waweze kuitoa album hiyo ya MACHOZI BAND.
                                 JONIKO FLOWER AKIWA NA WANA MACHOZI BAND

0 comments:

Post a Comment

.

.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...