WELCOME TO GMBONGO BLOG

To keep the body in good health is a duty... otherwise we shall not be able to keep our mind strong and clear.

TANGAZA NASI SASA

Tuwasiliane kwa Email: gmbongo.chuma@gmail.com

WE ARE HERE TO SERVE YOU

Keep you Entertained always

WE ARE HERE TO SERVE YOU

Habari na Burudani

WELCOME TO GMBONGO WORLD

Kwa habari za Burudani na zenye uhakika.

WAY

Monday, February 23, 2015

WAANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUTUMIA KALAMU ZAO KUFICHUA MAUAJI YA ALBINO

                          Waandishi wa habari wakiwa kazini kwenye mkutano

 Waandishi wa habari nchini, wametakiwa kutumia kalamu zao kufichua chanzo cha mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi Albino, ambao umeibuka kwa kasi kubwa siku za karibuni.

Akizungumza leo Mjini Moshi na waandishi wa habari kwenye warsha ya siku tatu iliyoandaliwa na Chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania, (TAMWA),kwa lengo la kufichua ukatili wa kijinsia, Mshauri wa vyombo vya habari, Deo Peter, alisema kuna hajana ya kufichua chanzo cha mauaji hayo.

Amesema inasikitisha kuona watu hao wanaendelea kuuwawa kikatili, huku waandishi wakijikita kuandika tu jinsi wanavyouwawa, bila kufanya utafiti kujua chanzo cha mauaji hayo ni nini, jamo ambalo halisaidii kukomesha kiini cha mauaji hayo.
 
Aidha amesema sambamba na hilo pia hata kwenye seuala la ukeketaji nao waandishi wa habari wakijikita kufichua chanzo cha ukeketaji katika jamii husika ni zipi itasaidia kukomesha pia ukeketaji.

Amesema ukatili wowote ule unapofanyika unamyima mtu kukosa uhuru na kinaleta athari za kisaikolojia miongoni mwa wahusika wa ukatili huo.

Naye Mwakilishi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA),ambaye alikuwepo katika warsha hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Tamwa, Judica Losai, amesema kuwa wanahabari wanapaswa kuunganisha nguvu ili kufichua ukatili wa kijinsia ambao kwa sasa umeshika kasi
kubwa.

Amesema kinachopaswa kuzingatiwa katika uandishi wa habari za kufichu  ukatili wa kijinsia ni umakini, kuzingatia lugha ya kutumia na kuhakikisha waathirika wanapata msaada mwisho wa siku.

Amesema kuwa ukatili wa kijinsia nchini mkubwa ambao kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Afya za mwaka 2013 inaonyesha Mkoa wa Manyara unaongoza ukeketaji kwa asilimia 71, ikifuatiwa na Dodoma asimilia 64 na Arusha asilimia 59.

Thursday, February 12, 2015

SERIKALI IMEANZA KUSAMBZA NAKALA MILIONI MBILI ZA KATIBA INAYOPENDEKEZWA NCHINI NZIMA

                                    Waziri wa Katiba na Sheria Dkt, Asha Rose Migiro

Serikali imeanza kusambaza nakala milioni mbili za Katiba Inayopendekezwa nchini kote ili kuwawezesha wananchi kuisoma na kushiriki katika Kura ya Maoni iliyopangwa kufanyika tarehe 30 Aprili mwaka huu.

Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha-Rose Migiro amesema leo (Jumatano, Februari 11, 2015) jijini Dar es Salaam kuwa kati ya nakala hizo zilizochapwa jijini Dar es Salaam, nakala 1,800,000 zinasambazwa Tanzania bara na nakala 200,000 zinasambazwa Tanzania Zanzibar.

Kwa mujibu wa Waziri Migiro, hadi kufikia jana (Jumanne, Februari 10, 2015), jumla ya nakala 707,140 zilikuwa zimesambazwa katika mikoa 12 ya Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar ambayo imepata nakala 200,000 na kuwa kazi hiyo inaendelea vizuri na inatarajiwa kukamilika katika muda mfupi ujao.

Mikoa hiyo na nakala ziliozosambazwa katika mabano ni Katavi (15,640), Rukwa (27,040), Ruvuma (47,740), Mbeya (78,640), Simiyu (34,840), Mara (52,540), Tabora (58,540) na Kigoma (41,440). Mikoa mingine ni Kagera (54,340), Geita (36,940), Mwanza (57,040) na Pwani ambapo usambazaji umeanza kwa wilaya ya Mafia ambayo imepata nakala 2,400.

Idadi ya nakala ya Katiba Inayopendekezwa kwa kila mkoa inategemea na wingi wa kata katika mkoa, ndiyo maana baadhi ya mikoa unaona imepata nakala nyingi,” amesema Dkt. Migiro ofisini kwake wakati akiongea na baadhi ya waandishi wa Habari waliotaka ufafanuzi kuhusu hatua iliyofikiwa katika kazi ya uchapishaji na uasambazaji wa nakala za Katiba Inayopendekezwa.

Kwa mujibu wa Waziri Migiro, kuna zaidi kata 3,800 nchini kote na lengo la Serikali ni kusambaza nakala 300 katika kila kata ambazo zitasambazwa kwenye vijiji, vitongoji na mitaa kupitia Ofisi za Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za Miji, Manispaa na Majiji.

Kuhusu taasisi za elimu na dini, Waziri Migiro amesema Serikali imepanga kusambaza nakala 658,400 kwa taasisi za elimu, dini, vyama vya siasa na asasi za kiraia na kuwa usambazaji huo utaanza hivi karibuni.

Pamoja na usambazaji huo, Waziri Migiro amewakumbusha wananchi ambao bado hawajapata nakala za Katiba Inayopendekezwa, kuisoma kupitia tovuti ya Wizara ya Katiba na Sheria (www.sheria.go.tz) na tovuti ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (www.agctz.go.tz).

Tuesday, February 10, 2015

TANZANIA YASHUTUMIWA KUWAFADHILI WAASI WA FDLR KUPANGA MASHAMBULIZI CONGO

                      Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaJakaya Kikwete
 Umoja wa mataifa imezituhumu serikali za Tanzania na Burundi kuhusiana na hali katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Ripoti mpya ya kundi la wataalamu wa umoja huo kuhusu Congo, imeituhumu Tanzania kwa kuwaruhusu viongozi wa kundi la waasi wa FDLR kuandaa mikutano nchini humo.

Taarifa hiyo ya Umoja wa mataifa inasema kuwa tangu mwaka wa 2013, viongozi wa FDLR na baadhi ya washirika wao wa kisiasa kutoka Ulaya wamekuwa wakikutana nchini Tanzania.

Hata Hivyo katika kujibu madai hayo serikali ya Tanzania ilikanusha kabisa kuwahi kuakaribisha mikutano yoyote ya waasi ndani ya ardhi yake na kuongeza kuwa hakujawahi kuwa na mazungumzo yoyote kati ya majeshi yake na wapiganaji wa FDLR.

WAFANYABIASHARA WATAKIWA KUENDELEA NA BIASHARA WAKATI MWENYEKITI WAO AKIFIKISHWA MAHAKAMANI LEO

  Mwenyekiti wa wafanyabiashara Tanzania Johnson Minja
Wafanya biashara nchini wametakiwa kuendelea kufanya biashara zao wakati mwenyekiti wa jumuiya ya Wafanyabiashara Johnson Minja akipandishwa kizimbani leo mjini Dodoma nchini Tanzania.
Wito huo umetolewa jana na Minja wakati akifungua kikao cha 

Halamshauri Kuu ya Taifa ya Jumuiya hiyo kilichofanyika mjini hapa ambapo alisema tayari viongozi wa ngazi za juu wa Jumuiya hiyo wameshawasili kuhudhuria kesi hiyo.

“Ni siku moja tu kabla ya siku ya kesi ambayo imefunguliwa Dodoma, jumuiya ya wafanyabiashara wanahudhuria kesi kwa pamoja kama taifa,” alisema Minja na kuongeza kuwa,

“Lakini pia, kumekuwa na muunganiko wa watu wengi ambao wanataka kujua maendeleo ya kesi na kitu gani kinaendelea, naomba wafanyabiashara wawe na amani na utulivu wakati kesi hiyo ikiwa inaendelea.”

Amesema tunaamini kwamba mahakama itatenda haki na mwisho wa siku yale ambayo tumejadiliana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Serikali kwa ujumla, yanaweza kufanyiwa kazi kwa aajili ya manufaa na maslahi mapana zaidi ya Taifa , wafanyabiashara na wananchi wote kwa ujumla.

Amesema, haitakuwa na maana kama viongozi wote watakuwa mahakamani na wafanyabiashara nao wakafunga maduka yao hali itakayosababisha wao na Serikali kukosa mapato na wananchi kukosa huduma.

“Haina maana sisi tuna kesi na wao waendelee kupoteza wanapofunga maduka yao, wao wanapoteza ,wananchi wanakosa huduma na Serikali inakosa mapato, kikubwa tunachoomba kwao ni sala, watuombee lakini wasisitishe huduma, ili watoe huduma kwa wananchi na Serikali ipate mapato,” alisema Minja

Vile vile amesema, kitendo cha wafanaybiashara kufunga maduka yao yao wakati kesi hiyo ikiendelea mahakamani,inaweza kusababisha Jumuiya hiyo kushindwa kufikia azma yao kwa Serikali ya mazungumzo katika kuwasaidia kufikia muafaka wa changamoto zinazowakabili , kwa njia ya majadiliano.

Leo Minja anatarajiwa kufikishwa mahakamani kwa mara ya pili, mara ya kwanza alifikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma mjini mnamo Januari 28 mwaka huu kwa tuhuma ya kuwachochea wafanyabiashara wasilipe kodi ya Serikali.

Pia Minja anatuhumiwa kwa kosa la kuwapa maelekezo wafanyabiashara ya kutotumia mashine za Kilektoniki (EFDs).

.

.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...