WAY

Sunday, August 28, 2011

JE WAIJUA ILIPOTEKEA Q BAND? NI BAND YENYE WASANII LUKUKI NA WENYE VIPAJI VYA HALI YA JUU

                                                      LET'S GO AFRICA
the q band imeanzishwa miaka mitatu iliyopita ikiwa miaka miwili ya kujenga band na mwaka mmoja wa kazi mpaka sasa,the q band ni band inayongozwa na watu wawili ambao wote ni waimbaji.ambao ni: LEAH MOUDDY alieye wahi kushiriki mashinndano ya kimuziki na kutambulika kitaifa na kimataifa kama: bongo star seach shindano la kutafuta vipaji maalumu Tanzania na kuweza kuibuka mshindi wa nafasi ya pili na aliweza kuchaguliwa kuiwakilisha Tanzania katika mashindano yajulikanayo kama TUSKER PROJECT FAME mashindano yaliyofanyika nchini Kenya na kufika nafasi ya robo fainal na hapa nyumbani Tanzania amewahi kuajiriwa ka mwimbaji katika BAND YA TANZANITE na B Band. Mwimbaji mwingine ni SIZ Q aliyewahi kushiriki mashindano ya pop star na hakufanikiwa kushinda na baada ya hapo alijiunga katika band ya B. band kama muasisi wa band hiyo na aliweza kutoa  nyimbo itwayo kasoro akiwa amemshirikisha mwanadada Ray c iliyomtambulisha kitaifa na kimataifa na aliweza kudumu kwenye band ya b band kwa miaka kumi mpaka alipo kutana na Leah na kuamua kuanzisha band yao na kuipa jina la Q Band. Q Band ilianza tarehe 5/9/2009 nailifanya mazoezi kidogo kidogo kutokana na ufinyu wa pesa Q Band ilipumzika mazoezi na kuanza kujipanga upya mwaka 2010 Q Band  ilirudi tena kambini na wanamuziki wapya na walifanya mazoezi kwa muda wa miezi sita na likatokea tatizo la vyombo ndipo tulipo pumzisha band na kujipanga na kuepuka tatizo la vyombo ambavyo tulikuwa tunavikodi ndipo tulipoagiza vyombo uingereza kwa mtu ambae tunafamiana alitupa msaada huo wa vyombo vyote vya band hapo tuka wa kamili na tarehe 3/1/2011 tukanza mazoezi rasmi na tarehe mwezi wa sita mwaka 2011 walianza kazi ya kwanza kufanya moja ya show za washiriki   walioiwaikilisha tusker project fame kutoka Tanzania nao ni PETER MSECHU LEAH MOUDDY na Aneth Kushaba show ilikuwa nzuri na ilikuwa changamoto kwa Q Band na kuanzia hapo Q band ikanza kujulikana hapa na pale na kuweza kuendelea kutafuta kazi tofauti tofauti kwa sasa Q Band ina toa burudani katika Club Le Mambo na Trinity zote za Dar es salaam Tanzania
 Q Band ipo katika mfumo wa hotel band ambayo inatoa burudani ya muziki tofauti wa copy kama Kwaito,Zouk,Afro Jazz,R&B,Bolingo,Pop,Zilipendwa na nyimbo zetu wenyewe muziki wa kizazi kipya Bongo Flaver malengo ni kuweza kutambulika dunia nzima na kuitambulisha Tanzania katika ulimwengu wa muziki wa live Band.

Facebook: Qband live
Email:theqband@live.com


                   hapa ni Q Band wakiwa mzigoni siz q na nuruely wakiongoza mashambulizi


   hapa utamu wa Q.BAND HATARI TUPU AISEEEEEEEEEEEEEEE!




Kwa wanaojua mziki ukiambiwa utaje watu kumi wenye sauti hautamuacha nuruely sasa hapa yupo mzigoni na Q Band.


presidaa wengine wanaita rais lkn huyu ni wa Q band akiwa na mtazamo wa kimataifa zaidi


vice presidaa wa Q.Band natamani kusema first lady ni vocalist wa kike kati ya wale watatu tanzania wanamwita LEAH MOODY hapa mzigoni na wana Q.band

0 comments:

Post a Comment

.

.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...