Rais
wa Zimbawe na Mwenyekiti wa umoja wa Africa Robert Gabriel Mugabe
Rais
wa Zimbawe na Mwenyekiti wa umoja wa Africa Robert Gabriel Mugabe
amewataka viongozi wa nchi za Africa kukataa kuwa vibaraka wa mataifa
tajiri duniani na badala yake wajitoe katika kuwatumikia waafrika
ili kufikia mafanikio ya kimaendeleo katika ustawi wa bara hili.
Rais
Mugabe ametoa mwito huo wakati akizungumza katika mkutano wa
kimataifa wa viongozi Vijana kutoka nchi mbalimbali za Bara la Afrika
na China unaofanyika katika ukumbi wa mikotano wa Ngurdoto nje kidogo
ya Jiji la Arusha.
Katika
hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano huo Rais Mugabe ametumia muda
mwingi kuwaasa na kutoa mwito kwa viongozi hao vijana akisistiza kuwa
Bara la Afrika linategemea mchango wa Fikra zinazojali uwajibikaji na
nidhamu ya hali ya juu katika utumishi.
Awali
akizungumza katika Mkutano huo,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dakta Jakaya Kikwete ameonyesha imani aliyoanayo kupitia
mkutano wa viongozi vijana kutoka Afrika na Uchina kwamba utatoa
fursa ya kutoka na maazimio yatakayokuwa na tija kwa mustakabali wa
watu wote