WELCOME TO GMBONGO BLOG

To keep the body in good health is a duty... otherwise we shall not be able to keep our mind strong and clear.

TANGAZA NASI SASA

Tuwasiliane kwa Email: gmbongo.chuma@gmail.com

WE ARE HERE TO SERVE YOU

Keep you Entertained always

WE ARE HERE TO SERVE YOU

Habari na Burudani

WELCOME TO GMBONGO WORLD

Kwa habari za Burudani na zenye uhakika.

WAY

Wednesday, August 6, 2014

WAKAZI MILIONI 2 VIJIJINI KUNUFAIKA NA HUDUMA YA MAJI SAFI NA SALAMA


 
   Waziri wa maji Pr.Jumanne Maghembe
Kufuatia msaada wa pound za uengereza Milioni 150 zilizotolewa na serikali ya Uengereza kwa serikali ya Tanzania katika kuboresha huduma ya maji vijijini wakazi wa vijijini wapato milioni 2 hapa chini wanatarajiwa kuanza kunufaika na huduma ya maji safi na salama ifikapo desemba mwaka 2015.

Akizungumza mara baada ya msaada huo Waziri wa Maji Pr Jumanne Magembe amesema msaada huo umekuja kwa wakati mwafaka, ambapo wizara yake imeelekeza nguzu vijijini hivyo kupitia msaada huo kutaharakisha utekelezaji wa mpango wa matoke makubw sasa BRN.

Pr Jumanne Magembe amebainisha utekelezaji wa miradi ya maji vijijini na usafi wa mazingira na mpango wa matokeo makubwa sasa kuwa umesaidia sana kuondoa magonjwa sumbufu yaliyokuwa wakiwasumbua wananchi waishio vijijini.

Tuesday, August 5, 2014

KING OF BEST MELODY CHRISTIAN BELLA a.k.a OBAMA KUFANYA ONYESHO MAALUM LA KUWAHAMASASHA WANAWAKE KUPITA "NANI KAMA MAMA"



Akiwa anafanya vyema na wimbo wake uliotokea kutamba katika vituo vya redio nchini Tanzania 'Nani kama Mama', mwanamuziki nyota wa miondoko ya dansi na Bongofleva Christian Bella amepanga kufanya onyesho kubwa la kuwahamasisha wanawake kupitia wimbo huo mpya jijini Dar es Salaam.


Christian Bella ambaye naye ni miongoni mwa wasanii anayewapa kipaumbele kwa akina mama amesema kuwa tukio hilo lililobatizwa jina 'USIKU WA MAMA' litakalofanyika tarehe 29 mwezi huu atatauzindua wimbo huo pamoja na kuuperform kwa mara ya kwanza akishirikiana na wasanii wa miondoko ya Bongo fleva nchini akiwemo Ommy Dimpoz ambaye naye alimpoteza mama yake kipenzi.


Christian Bella aongea na enewz kuhusiana na onyesho hilo na pia sababu haswa ya kuutunga wimbo huo 'Nani kama Mama' ambao ni rasmi kwa ajili ya heshima kubwa kwa akina mama ulimwenguni.

SUPER KWATA BAND CHINI YA ANCO VENA YAACHIA FANYA UJE SASA KUFANYA LISTEN PARTY KWA AJILI YA ALBUM YAO NI KWA MARA YA KWANZA KWA BAND ZA TANZANIA KUFANYA LISTEN PARTY


BAND inayomilikiwa na  Jeshi la polisi nchini Tanzania ambayo inaongozwa na kijana mwenye kipaji cha hali ya juu katika utunzi na uimbaji ANCO VENA ambae amewahi kutamba na band kama BWAGAMOYO SOUND na TWANGA PEPETA na band hiyo yenye makazi yake mjini moshi imetanguliza kwa mshabiki wimbo wa mpya uliombwa na Anco vena kwa stale ya Rumba la aina yake wakiupa wimbo huo jina la 'Fanya uje'

Vena amasema Program inayofata baada ya kuachia wimbo huo nifanya listen party kwa wadau mbalimbali ambao wataweza kuisikiliza album yao ambayo ipo tayari ili waweze kuitolea mawazo ya ya kuijenga kabla ya kuipeleka album hiy kwa mashabiki wa band hiyo.

Vena ameongeza kuwa Licha ya band hiy kumiliwa na jeshi la polisi lakini wanampango wa kuweza kufanya maonyesho sehemu mbalibmali nchini Tanzania na dunianni kwa ujumla katika kuelta mapinduzi ya kuweza kurdisha band zilizokuwa  zikitamba wakati huo kama Polis Jazz,na nyingine nyingi za Enzi hizo

Monday, August 4, 2014

MTOTO WA HEMED MANET KUMUENZI BABA YAKE KWA TAMASHA KUBWA LITAKALOWAKUTANISHA MANGULI WA DANSI YA ZAMANI NCHINI NI KHEIRATY MANET ANAEIMBA NA VIJANA JAZZ KWA SASA




Mtoto wa Aliekua nguli wa muziki wa dansi nchini tanzania mwenye sauti ya pekee na kubatizwa jina la sauti ya chiriku na yeye akijulikana kama mtoto wa chiriku Kheiraty Maneti ambae kwa sasa anaimba na band ya mwisho kuimbia baba yake ya Vijana JAZZ  ameandaa Tamasha kubwa la kuenzi baba yake mnamo  tarehe 07/08/2014. 
                            KHEIRAT MANETI chiriku mtoto
Kwa mujibu wa bi dada huyo amesema anategemea Tamasha hilo litaweza kuwahusisha wanamuziki wa Vijana jazz na nitawakusanya wale wazee wote waliowahi kutingisha ktk muziki na alioimba nao baba wotee John Kitime,Hassan Dalali,Rashid Pembe,Kida Waziri,Kulwa Milonge,Cosmas Chidumule,Juma Choka,Ally Yahya,Mbaraka Othman,Mafumu Bilal na wengine wengi sana mzee King Kikii atasindikiza na band yake na isha mashauzi.
Kheiraty amesema lengo la tamasha hilo ni mkukumbuka mchango wa baba yake katika tansinia ya muziki wa dansi nchini lakini pia kuwaleta pamoja wakongwe wa muziki wa dnsi katika kubadilishana mawazo.


.

.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...