WAY

Thursday, November 14, 2013

JESHI LA POLISI LINAWASHIKILIA WATU KUMI KUHUSIKA NA MAUAJI YA MWANAHARAKATI NA MWANASHERIA DK. SENGODO MVUNGU AKIRI KUHUSIKA NA TUKIO HILO

Jeshi la polisi kanda maalumu ya dar-es-salaam linamshikilia mtuhumiwa mmoja John Ikodia kwa kosa la kushiriki kikamilifu kwenye mauaji ya mwanasheria dk sengodo mvungi.
Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa kanda maalum dar-es-sallm Suleiman Kova amesema walipata taarifa kutoka kwa raia wema kwamba alishiriki kikamilifu katika tukio lilisababisha kifo cha dk mvungi.
Kamanda kova amesema baada ya kumhoji mtuhumiwa alikiri moja kwa moja katika tukio hilo na kwenda kuonyesha vitu walivyopora ikiwemo bastola aina ya REVOLVER No BDN 6111 pamoja na risasi 21.
Aidha Kova alisema mtuhumiwa huyo ni wa kumi kukamtwa kuhusiana na tukio hilo nab ado opersheni inaendelea ili kuhakikisha yoyote aliehusika na tukio hilo anakamatwa.





0 comments:

Post a Comment

.

.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...