Wednesday, November 13, 2013
Home »
» MWENYEKITI WA NCCR MAGEUZI ATOA RATIBA YA MAZISHI YA DK SENGODO MVUNGI JESHI LA POLISI LASEMA LINAWASHIKILIA WATU TISA KUHUSIANA NA TUKIO HILO
MWENYEKITI WA NCCR MAGEUZI ATOA RATIBA YA MAZISHI YA DK SENGODO MVUNGI JESHI LA POLISI LASEMA LINAWASHIKILIA WATU TISA KUHUSIANA NA TUKIO HILO
Mkurugenzi wa Katiba, Sheria
na Haki za Binadamu wa NCCR-Mageuzi, Dk Sengodo Mvungi amefariki dunia jana
alasiri nchini Afrika Kusini alipokuwa akipatiwa matibabu.
Taarifa za kifo chake
zimethibitishwa na Mwenyekiti Taifa wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia.
Akizungumuza na safari radio
leo asubuhi Mbatia amesema taratibu za mazishi zimekwishapangwa ambapo mwili wa
marehemu utawasili nchini siku ya ijumaa ya tar 15 na kusomewa ibada tar 16
katika kanisa la mt joseph jijini Dar-es-salaam
Aidha siku hiyo hiyo saa 9 na nusu utapelekwa karimjee kwa ajili ya
kupewa heshima za mwisho na viongozi pamoja na watu mbalimbali.
Mbatia ameongeza kuwa jumapili
ya tar 17 jioni mwili utasafirishwa kupelekwa mkoani Kilimanjaro katika wilaya
ya mwanga kwa ajili ya maziko yatakayofanyika tar 18.
Dk Mvungi alijeruhiwa kwa
kukatwa na mapanga kichwani Novemba 13, mwaka huu nyumbani kwake Kibamba
Msakuzi na watu wanaosadikiwa ni majambazi.
.


0 comments:
Post a Comment