WELCOME TO GMBONGO BLOG

To keep the body in good health is a duty... otherwise we shall not be able to keep our mind strong and clear.

TANGAZA NASI SASA

Tuwasiliane kwa Email: gmbongo.chuma@gmail.com

WE ARE HERE TO SERVE YOU

Keep you Entertained always

WE ARE HERE TO SERVE YOU

Habari na Burudani

WELCOME TO GMBONGO WORLD

Kwa habari za Burudani na zenye uhakika.

WAY

Tuesday, August 19, 2014

BAADA YA KUJIFUNZA MENGI AKIWA NDANI YA TWANGA PEPETE HAJI RAMADHANI MAARUFU KAMA HAJI BBS AANZA KUONYESHA UWEZO AANDIKA WIMBO WA KWANZA NDANI YA TWANGA PEPETA KUTOKA HIVI KARIBUNI AUITA MAPENZI YANAUMIZA




                                   HAJJI RAMADHANI
Mwanamuzi ambaye kipaji chake kiliweza kuibuka katika mashindano ya kusaka vipaji BBS,miaka ya hvi karibun Hajji Ramadhani wengi wakimjua Haji BSS ambae kwenye shindano la kwanza hakuweza kufanya vizuri lakini bdaadae akapta second chance na kuibuka kidedea kwa jujizolea kitita cha sh. milioni hamsini na hatimae kuamua kujiunga na band ya Twanga pepeta international Kisima cha Burudani.

Haji kwa sasa ameonekana ameiva kiasi cha kutosha cha kuweza kutunga nyimbo za band na kuleta gumzo  baada ya wimbo wake alioutunga Ndani ya band hiyo na ikiwani mara ya kwanza Tangu atue band hiyo umekua gumzo kwa mashabiki wa Twanga baada kuonekana kuombwa sana baada ya kuupiga mara kadhaa katika show tofauti.

Hajji ambae ameupa jina la MAPENZI  yanaumiza wimbo amesema ni wimbo ambao amekaa na kufikiri kwa muda mrefu na kuamua kutoa wimbo huo ambao anaamini utakua gumzo kama nyimbo nyingine nyingi zilizowahi kutamb za Twanga pepeta kutoka na ubora wa wimbo na ushirikiano wa wanamuzi wa Twanga katika wimbo huo.
                             HAJJI KAZINI-TWANGA
Hivi karibuni Hajji alikua anaanda Album yake binafsi ambayo itakua na mchanganyiko wa wimbo tofauti na kusema kwa sasa ataelekeza nguvu katika kuusukuma wimbo huo wa twanga na kuupa nafasi halafu baada ya hapo ataendelea na project yake.

Wednesday, August 13, 2014

LICHA YA KUIMBA COPY KWENYE MAHOTEL GROUP O BAND YA JIJINI MWANZA WAACHIA SINGLE MOJA HEWANI-NI QUEEN SHEDA



                        MIMI NA HUSNA WA GROUP O
Waimbaji wawili wa muziki wa kiafrica ambao muda mwingi wametumia kuimba miziki yao nje ya nchi kwenye mahotel tofauti ikiwemo Oman, Uholanzi, Saudia Arabia na kwingine na sasa wakiwa nchi Tanzania ambapo wameweka makazi yao Jijini Mwanza GROUP O band ambayo inaundwa na Hassan Muya na Husna wameachia wimbo wao wa QUEEN SHEDA ambao wameupiga katika mahadhi ya zouk dansi.

Kwa mujibu wa kiongozi wa Band hiyo Hassan Muya huo ni mwanzo tu na kusema wanataka kuwaonyesha watu kuwa sio kwamba wanaoimba miziki ya mahotel hawawezi kupiga nyimbo zao ni jambo linalowezekana ila watu watambue kuwa utafutaji ndio unawafanya wapige copy nyingi kushinda nyimbo zao.

Muya amesema huo ni mwanzo tu zipo nyimbo nyingi ambazo zinakuja kuwatambulisha rasmi Group O band ambapo kwa sasa wako jikoni na wanarekodi katika studio za huko huko mjini mwanza na kusema kuwa mziki mzuri unatoka popote na sio Dar es salaam tu.

Tuesday, August 12, 2014

LICHA YA KUREJEA BAND YA WAJASILIAMALI MALU MUIMBAJI WA BAND HIYO JANUARY ELEVEN APIGA SHOW KWENYE SHREHE TOFAUTI ZA MAHARUSI MAKUBWA NA BIRTHDAY ZA MAANA

                              

                                JANUARY ELEVEN 

Muimbaji alierejea mapacha hvi karibuni baada ya kuvunjika kwa band ya Victoria Sound iliyokuwa chini Prince Muumini Mwinjuma,January Eleven ameoneka akionyesha ujasiliamali mwingine wa kujiongezea kipato katika sherehe kubwa ikiwemo maharusi  ambazo zinamkodi kupiga live akiambatana na watu kadhaa katika shows hizo


Akiongea na blog hii japo hakukubali moja kwa moja kuwa ni biashara yake nyingine ya utafutaji wa pesa amesema hali ilitokea tu baada ya marafiki zake kadhaa kuweza kumuomba kutumbuiza katika sherehe zao ambazo wengi wametaka kuonyesha utafauti wa kupiga miziki kwa cd na badala yake wanataka nyimbo hizo live na kwa kuwa mwanamuziki huyo ameonekana ana kipaji kikubwa katika kuimba copy nyingi basi huwa wanamchukua kwa malipo maalumu na kuweza kufanya show ingawa amesema hiyo haiko rasmi kwamba ndio kazi aliyoamua kufanya katika utafutaji zaidi mbali ya band.
                            JANUARY ELEVEN

Lakini ameongeza kuwa anatafakari kama akiona suala hili linalipa basi atajiingiza moja kwa moja na kuitangaza kama kiofisi kabisa lakini kwa anafanya kwa makubaliano maalumu kwa kuwa bado ana majuku ya kuifanyia band yake ya mapacha watu na huwa anafanya show hizo endapo band yake ya Mapacha watatu inakuwa haina onyesho.

Ki ukweli kama shabiki na mpenzi mkubwa muziki wa dansi January nadhani ndie mwanamuziki alie na uwezo wa kuimba nyimbo nyingi zaidi za copy kwa ufasaha kushinda mwanamuziki mwingine yoyote nadhani ndio maana anapata mialiko mingi katika show hizo.

January hivi karibuni aliweza kuombwa na viongozi wa mapacha kkuweza kurejea katika band hiyo na kuweza kusaidia kikazi zaidi na ameweza kurejea kwa makubaliano maalumu ya kufanya kazi ndani ya band hiyo.

Friday, August 8, 2014

MUIMBAJI WA AKUDO IMPACT ZAGREB BUTAMU SURA MVUTO MBIONI KUACHIA VIDEO MBILI KATIKA UTANGULIZI WA ALBUM YAKE BINAFSI YA KIFUA MBELE ASEMA ITAFANYA MAPINDUZI KATIKA MUZIKI



                            ZAGREB BUTAMU NA G MBONGO
Mwanamuziki wa Siku nyingi wa Band ya Akudo impact Zagreb butamu a.k.a Sura mvuto amekamilisha video za nyimbo zake mbili ambazo ataziachia hivi karibuni ili kusindikiza maandalizi ya album yake ya Kifua mbele ambayo anatarajia kuiachia hivi karibuni

Zagreb ambae anafanya album yake hiyo nje ya Akudo impact amesema kwa sasa anamalizia nyimbo moja na kukamilisha idaidi ya nyimbo sita lakini tayari ameshaachia wimbo mmoja radioni lakini katika kusogeza kuipush zaidi album yake hiyo ya kifua mbele, amesema kwa sasa ameshatanguliza wimbo mmoja radioni ambao ameupa jina laSAKUBA lakini pia antarajia kufanya video ya wimbo huo na wimbo mwingine katika album hiyo ni,MKE MWEMA, 

Zagreb amesema nyimbo nyingine zitakazopatikanai katika album hiyo ni pamoja ITAFIKA,AFRIKA,SELEKA,NA KIFUA MBELE ambayo inabeba jina la album hiyo ambao anasema ameifanya peke yake nje ya Akudo Impact

Thursday, August 7, 2014

MUIMBAJI WA SIKU NYINGI WA FM ACADEMIA KING BLAISE KUTOKA NA NYIMBO ZA INJILI YAANI 'GOSPEL SONG'AKAMILISHA MOJA INAITWA MAARIFA



                                 KING BLAISE
Mwanamuziki muda mrefu wa band Kongwe ya muziki wa Dansi ya Kizazi cha sasa FM academia King blaise ambae ni mmoja wa viongozi wa band hiyo ameamua kufanya kazi nje ya bandhiyo ambayo atamuimbia mungu yaani GOSPEL SONG, ambapo amesema mpaka sasa kwa kiasi kikubwa imeshakamilika ila bado nyimbo kadhaa,

King blaise amesema amua kiuimba ili kuwaelimisha vijana licha ya kuimba nyimbo za kidunia lakini pia wana wajibu wa kumsifu mungu kwa kipaji alichowapa lakini pia ili kupunguza madhambi ambayo wanayafanya na  kumuimbia mungu ni jambo la msingi zaidi kuliko kila siku kuwaimbia Mapedeshee.

Blaise ambae anasema kwa sasa ameshatanguliza wimbo nyimbo mbili mmoja ukiitwa MAARIFAna mwingine akiupa jina hakuna kama mungu, lakini mbali na hilo pia katika nyimbo hizo amesema ameshwarikisha wanamuziki wa bongo flever kutoka T.H.T, Makomando akisiitiza pamoja na ubongo flever lakini kawaimbisha gospel.

licha ya kukamilisha nyimbo za INJILI lakini pia Blaise amesema hvi karibuni atatumbulisha nyimbo nyingine ya kidunia iitwayo Ndoa ambayo amemshirikisha Msanii mkongwe Juma kakere na kusema watu waisubiri kwa hamu sana

Wednesday, August 6, 2014

PINDA AWATAKA WAFUGAJI KUFUGA KISASA ILI KUJIKWAMUA KIUCHUMI

 
    WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA
Waziri mkuu Mizengo Pinda amewataka watendaji wa halmashauri kuhakikisha wanabadili fikra za ufugaji ili kuwawezesha kuendehsa ufugaji wa kisasa na wa kibiashara ili kukabiliana na umaskini kwa wafugaji.


Mh.Pinda amesema ni lazima Wizara ibadili mfumo huo kwa maendeleo ya taifa na kuongeza kuwa elimu ya ufugaji bora na wa kisasa nchini itawezesha wafugaji kujikwamua kiuchumi na kuchangia kwa kiasi kikubwa pato la taifa.


Pinda amesema hayo jana mjini Dodoma wakati akizindua mashindano ya maonyesho ya mifugo katika viwanja vya nanenae dodoma na kusema kuwa bado hitaji la mifugo bora hapa nchini ina changamoto kubwa licha ya Tanzania kuwa na idadi kubwa ya mifugo lakini mchango wake kwa pato la taifa ni mdogo.

JUKWAA LA KATIBA LASIKITISHWA NA BUNGE MAALUMU LA KATIBA KUANZA BILA UKAWA


                               Deus Kibamba
Jukwaa la katiba nchini Tanzania limesikitishwa na namna Bunge Maalumu la Katiba linavyotaka kunyamazisha sauti na mijadala ya wananchi, kuhusu kasoro zinazojitokeza katika mchakato unaoendelea wa kutafuta katiba mpya.

Mwenyekiti wa Jukwaa hilo Bw. Deus Kibamba ametoa kauli hiyo jana wakati akiongea na East Africa Radio jijini Dar es Salaam, ikiwa ni siku moja tangu kuanza kwa vikao vya bunge maalumu la katiba ambapo baadhi ya wajumbe wa bunge hilo wamenukuliwa wakiitaka serikali izuie midahalo ya wazi kuhusu mchakato wa katiba mpya

Aidha, Kibamba amesema mwishoni mwa juma hili Baraza la Vyama vya Siasa litakutana na pande hasimu katika mchakato wa katiba, ikiwa ni sehemu ya harakati za kupatanisha pande hizo, katika kile alichoeleza kuwa ni fursa pekee na ya mwisho ya kunusuru mchakato huo dhidi ya hatari ya kuvunjika.


WAKAZI MILIONI 2 VIJIJINI KUNUFAIKA NA HUDUMA YA MAJI SAFI NA SALAMA


 
   Waziri wa maji Pr.Jumanne Maghembe
Kufuatia msaada wa pound za uengereza Milioni 150 zilizotolewa na serikali ya Uengereza kwa serikali ya Tanzania katika kuboresha huduma ya maji vijijini wakazi wa vijijini wapato milioni 2 hapa chini wanatarajiwa kuanza kunufaika na huduma ya maji safi na salama ifikapo desemba mwaka 2015.

Akizungumza mara baada ya msaada huo Waziri wa Maji Pr Jumanne Magembe amesema msaada huo umekuja kwa wakati mwafaka, ambapo wizara yake imeelekeza nguzu vijijini hivyo kupitia msaada huo kutaharakisha utekelezaji wa mpango wa matoke makubw sasa BRN.

Pr Jumanne Magembe amebainisha utekelezaji wa miradi ya maji vijijini na usafi wa mazingira na mpango wa matokeo makubwa sasa kuwa umesaidia sana kuondoa magonjwa sumbufu yaliyokuwa wakiwasumbua wananchi waishio vijijini.

Tuesday, August 5, 2014

KING OF BEST MELODY CHRISTIAN BELLA a.k.a OBAMA KUFANYA ONYESHO MAALUM LA KUWAHAMASASHA WANAWAKE KUPITA "NANI KAMA MAMA"



Akiwa anafanya vyema na wimbo wake uliotokea kutamba katika vituo vya redio nchini Tanzania 'Nani kama Mama', mwanamuziki nyota wa miondoko ya dansi na Bongofleva Christian Bella amepanga kufanya onyesho kubwa la kuwahamasisha wanawake kupitia wimbo huo mpya jijini Dar es Salaam.


Christian Bella ambaye naye ni miongoni mwa wasanii anayewapa kipaumbele kwa akina mama amesema kuwa tukio hilo lililobatizwa jina 'USIKU WA MAMA' litakalofanyika tarehe 29 mwezi huu atatauzindua wimbo huo pamoja na kuuperform kwa mara ya kwanza akishirikiana na wasanii wa miondoko ya Bongo fleva nchini akiwemo Ommy Dimpoz ambaye naye alimpoteza mama yake kipenzi.


Christian Bella aongea na enewz kuhusiana na onyesho hilo na pia sababu haswa ya kuutunga wimbo huo 'Nani kama Mama' ambao ni rasmi kwa ajili ya heshima kubwa kwa akina mama ulimwenguni.

SUPER KWATA BAND CHINI YA ANCO VENA YAACHIA FANYA UJE SASA KUFANYA LISTEN PARTY KWA AJILI YA ALBUM YAO NI KWA MARA YA KWANZA KWA BAND ZA TANZANIA KUFANYA LISTEN PARTY


BAND inayomilikiwa na  Jeshi la polisi nchini Tanzania ambayo inaongozwa na kijana mwenye kipaji cha hali ya juu katika utunzi na uimbaji ANCO VENA ambae amewahi kutamba na band kama BWAGAMOYO SOUND na TWANGA PEPETA na band hiyo yenye makazi yake mjini moshi imetanguliza kwa mshabiki wimbo wa mpya uliombwa na Anco vena kwa stale ya Rumba la aina yake wakiupa wimbo huo jina la 'Fanya uje'

Vena amasema Program inayofata baada ya kuachia wimbo huo nifanya listen party kwa wadau mbalimbali ambao wataweza kuisikiliza album yao ambayo ipo tayari ili waweze kuitolea mawazo ya ya kuijenga kabla ya kuipeleka album hiy kwa mashabiki wa band hiyo.

Vena ameongeza kuwa Licha ya band hiy kumiliwa na jeshi la polisi lakini wanampango wa kuweza kufanya maonyesho sehemu mbalibmali nchini Tanzania na dunianni kwa ujumla katika kuelta mapinduzi ya kuweza kurdisha band zilizokuwa  zikitamba wakati huo kama Polis Jazz,na nyingine nyingi za Enzi hizo

Monday, August 4, 2014

MTOTO WA HEMED MANET KUMUENZI BABA YAKE KWA TAMASHA KUBWA LITAKALOWAKUTANISHA MANGULI WA DANSI YA ZAMANI NCHINI NI KHEIRATY MANET ANAEIMBA NA VIJANA JAZZ KWA SASA




Mtoto wa Aliekua nguli wa muziki wa dansi nchini tanzania mwenye sauti ya pekee na kubatizwa jina la sauti ya chiriku na yeye akijulikana kama mtoto wa chiriku Kheiraty Maneti ambae kwa sasa anaimba na band ya mwisho kuimbia baba yake ya Vijana JAZZ  ameandaa Tamasha kubwa la kuenzi baba yake mnamo  tarehe 07/08/2014. 
                            KHEIRAT MANETI chiriku mtoto
Kwa mujibu wa bi dada huyo amesema anategemea Tamasha hilo litaweza kuwahusisha wanamuziki wa Vijana jazz na nitawakusanya wale wazee wote waliowahi kutingisha ktk muziki na alioimba nao baba wotee John Kitime,Hassan Dalali,Rashid Pembe,Kida Waziri,Kulwa Milonge,Cosmas Chidumule,Juma Choka,Ally Yahya,Mbaraka Othman,Mafumu Bilal na wengine wengi sana mzee King Kikii atasindikiza na band yake na isha mashauzi.
Kheiraty amesema lengo la tamasha hilo ni mkukumbuka mchango wa baba yake katika tansinia ya muziki wa dansi nchini lakini pia kuwaleta pamoja wakongwe wa muziki wa dnsi katika kubadilishana mawazo.


.

.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...