WAY

Wednesday, August 6, 2014

PINDA AWATAKA WAFUGAJI KUFUGA KISASA ILI KUJIKWAMUA KIUCHUMI

 
    WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA
Waziri mkuu Mizengo Pinda amewataka watendaji wa halmashauri kuhakikisha wanabadili fikra za ufugaji ili kuwawezesha kuendehsa ufugaji wa kisasa na wa kibiashara ili kukabiliana na umaskini kwa wafugaji.


Mh.Pinda amesema ni lazima Wizara ibadili mfumo huo kwa maendeleo ya taifa na kuongeza kuwa elimu ya ufugaji bora na wa kisasa nchini itawezesha wafugaji kujikwamua kiuchumi na kuchangia kwa kiasi kikubwa pato la taifa.


Pinda amesema hayo jana mjini Dodoma wakati akizindua mashindano ya maonyesho ya mifugo katika viwanja vya nanenae dodoma na kusema kuwa bado hitaji la mifugo bora hapa nchini ina changamoto kubwa licha ya Tanzania kuwa na idadi kubwa ya mifugo lakini mchango wake kwa pato la taifa ni mdogo.

0 comments:

Post a Comment

.

.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...