WAY

Thursday, August 7, 2014

MUIMBAJI WA SIKU NYINGI WA FM ACADEMIA KING BLAISE KUTOKA NA NYIMBO ZA INJILI YAANI 'GOSPEL SONG'AKAMILISHA MOJA INAITWA MAARIFA



                                 KING BLAISE
Mwanamuziki muda mrefu wa band Kongwe ya muziki wa Dansi ya Kizazi cha sasa FM academia King blaise ambae ni mmoja wa viongozi wa band hiyo ameamua kufanya kazi nje ya bandhiyo ambayo atamuimbia mungu yaani GOSPEL SONG, ambapo amesema mpaka sasa kwa kiasi kikubwa imeshakamilika ila bado nyimbo kadhaa,

King blaise amesema amua kiuimba ili kuwaelimisha vijana licha ya kuimba nyimbo za kidunia lakini pia wana wajibu wa kumsifu mungu kwa kipaji alichowapa lakini pia ili kupunguza madhambi ambayo wanayafanya na  kumuimbia mungu ni jambo la msingi zaidi kuliko kila siku kuwaimbia Mapedeshee.

Blaise ambae anasema kwa sasa ameshatanguliza wimbo nyimbo mbili mmoja ukiitwa MAARIFAna mwingine akiupa jina hakuna kama mungu, lakini mbali na hilo pia katika nyimbo hizo amesema ameshwarikisha wanamuziki wa bongo flever kutoka T.H.T, Makomando akisiitiza pamoja na ubongo flever lakini kawaimbisha gospel.

licha ya kukamilisha nyimbo za INJILI lakini pia Blaise amesema hvi karibuni atatumbulisha nyimbo nyingine ya kidunia iitwayo Ndoa ambayo amemshirikisha Msanii mkongwe Juma kakere na kusema watu waisubiri kwa hamu sana

0 comments:

Post a Comment

.

.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...