WAY

Tuesday, August 19, 2014

BAADA YA KUJIFUNZA MENGI AKIWA NDANI YA TWANGA PEPETE HAJI RAMADHANI MAARUFU KAMA HAJI BBS AANZA KUONYESHA UWEZO AANDIKA WIMBO WA KWANZA NDANI YA TWANGA PEPETA KUTOKA HIVI KARIBUNI AUITA MAPENZI YANAUMIZA




                                   HAJJI RAMADHANI
Mwanamuzi ambaye kipaji chake kiliweza kuibuka katika mashindano ya kusaka vipaji BBS,miaka ya hvi karibun Hajji Ramadhani wengi wakimjua Haji BSS ambae kwenye shindano la kwanza hakuweza kufanya vizuri lakini bdaadae akapta second chance na kuibuka kidedea kwa jujizolea kitita cha sh. milioni hamsini na hatimae kuamua kujiunga na band ya Twanga pepeta international Kisima cha Burudani.

Haji kwa sasa ameonekana ameiva kiasi cha kutosha cha kuweza kutunga nyimbo za band na kuleta gumzo  baada ya wimbo wake alioutunga Ndani ya band hiyo na ikiwani mara ya kwanza Tangu atue band hiyo umekua gumzo kwa mashabiki wa Twanga baada kuonekana kuombwa sana baada ya kuupiga mara kadhaa katika show tofauti.

Hajji ambae ameupa jina la MAPENZI  yanaumiza wimbo amesema ni wimbo ambao amekaa na kufikiri kwa muda mrefu na kuamua kutoa wimbo huo ambao anaamini utakua gumzo kama nyimbo nyingine nyingi zilizowahi kutamb za Twanga pepeta kutoka na ubora wa wimbo na ushirikiano wa wanamuzi wa Twanga katika wimbo huo.
                             HAJJI KAZINI-TWANGA
Hivi karibuni Hajji alikua anaanda Album yake binafsi ambayo itakua na mchanganyiko wa wimbo tofauti na kusema kwa sasa ataelekeza nguvu katika kuusukuma wimbo huo wa twanga na kuupa nafasi halafu baada ya hapo ataendelea na project yake.

0 comments:

Post a Comment

.

.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...