WAY

Tuesday, August 12, 2014

LICHA YA KUREJEA BAND YA WAJASILIAMALI MALU MUIMBAJI WA BAND HIYO JANUARY ELEVEN APIGA SHOW KWENYE SHREHE TOFAUTI ZA MAHARUSI MAKUBWA NA BIRTHDAY ZA MAANA

                              

                                JANUARY ELEVEN 

Muimbaji alierejea mapacha hvi karibuni baada ya kuvunjika kwa band ya Victoria Sound iliyokuwa chini Prince Muumini Mwinjuma,January Eleven ameoneka akionyesha ujasiliamali mwingine wa kujiongezea kipato katika sherehe kubwa ikiwemo maharusi  ambazo zinamkodi kupiga live akiambatana na watu kadhaa katika shows hizo


Akiongea na blog hii japo hakukubali moja kwa moja kuwa ni biashara yake nyingine ya utafutaji wa pesa amesema hali ilitokea tu baada ya marafiki zake kadhaa kuweza kumuomba kutumbuiza katika sherehe zao ambazo wengi wametaka kuonyesha utafauti wa kupiga miziki kwa cd na badala yake wanataka nyimbo hizo live na kwa kuwa mwanamuziki huyo ameonekana ana kipaji kikubwa katika kuimba copy nyingi basi huwa wanamchukua kwa malipo maalumu na kuweza kufanya show ingawa amesema hiyo haiko rasmi kwamba ndio kazi aliyoamua kufanya katika utafutaji zaidi mbali ya band.
                            JANUARY ELEVEN

Lakini ameongeza kuwa anatafakari kama akiona suala hili linalipa basi atajiingiza moja kwa moja na kuitangaza kama kiofisi kabisa lakini kwa anafanya kwa makubaliano maalumu kwa kuwa bado ana majuku ya kuifanyia band yake ya mapacha watu na huwa anafanya show hizo endapo band yake ya Mapacha watatu inakuwa haina onyesho.

Ki ukweli kama shabiki na mpenzi mkubwa muziki wa dansi January nadhani ndie mwanamuziki alie na uwezo wa kuimba nyimbo nyingi zaidi za copy kwa ufasaha kushinda mwanamuziki mwingine yoyote nadhani ndio maana anapata mialiko mingi katika show hizo.

January hivi karibuni aliweza kuombwa na viongozi wa mapacha kkuweza kurejea katika band hiyo na kuweza kusaidia kikazi zaidi na ameweza kurejea kwa makubaliano maalumu ya kufanya kazi ndani ya band hiyo.

0 comments:

Post a Comment

.

.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...