WAY

Wednesday, August 13, 2014

LICHA YA KUIMBA COPY KWENYE MAHOTEL GROUP O BAND YA JIJINI MWANZA WAACHIA SINGLE MOJA HEWANI-NI QUEEN SHEDA



                        MIMI NA HUSNA WA GROUP O
Waimbaji wawili wa muziki wa kiafrica ambao muda mwingi wametumia kuimba miziki yao nje ya nchi kwenye mahotel tofauti ikiwemo Oman, Uholanzi, Saudia Arabia na kwingine na sasa wakiwa nchi Tanzania ambapo wameweka makazi yao Jijini Mwanza GROUP O band ambayo inaundwa na Hassan Muya na Husna wameachia wimbo wao wa QUEEN SHEDA ambao wameupiga katika mahadhi ya zouk dansi.

Kwa mujibu wa kiongozi wa Band hiyo Hassan Muya huo ni mwanzo tu na kusema wanataka kuwaonyesha watu kuwa sio kwamba wanaoimba miziki ya mahotel hawawezi kupiga nyimbo zao ni jambo linalowezekana ila watu watambue kuwa utafutaji ndio unawafanya wapige copy nyingi kushinda nyimbo zao.

Muya amesema huo ni mwanzo tu zipo nyimbo nyingi ambazo zinakuja kuwatambulisha rasmi Group O band ambapo kwa sasa wako jikoni na wanarekodi katika studio za huko huko mjini mwanza na kusema kuwa mziki mzuri unatoka popote na sio Dar es salaam tu.

0 comments:

Post a Comment

.

.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...