Deus Kibamba
Jukwaa
la katiba nchini Tanzania limesikitishwa na namna Bunge Maalumu la
Katiba linavyotaka kunyamazisha sauti na mijadala ya wananchi, kuhusu
kasoro zinazojitokeza katika mchakato unaoendelea wa kutafuta katiba
mpya.
Mwenyekiti
wa Jukwaa hilo Bw. Deus Kibamba ametoa kauli hiyo jana wakati
akiongea na East Africa Radio jijini Dar es Salaam, ikiwa ni siku
moja tangu kuanza kwa vikao vya bunge maalumu la katiba ambapo baadhi
ya wajumbe wa bunge hilo wamenukuliwa wakiitaka serikali izuie
midahalo ya wazi kuhusu mchakato wa katiba mpya
Aidha,
Kibamba amesema mwishoni mwa juma hili Baraza la Vyama vya Siasa
litakutana na pande hasimu katika mchakato wa katiba, ikiwa ni sehemu
ya harakati za kupatanisha pande hizo, katika kile alichoeleza kuwa
ni fursa pekee na ya mwisho ya kunusuru mchakato huo dhidi ya hatari
ya kuvunjika.
0 comments:
Post a Comment