Wajumbe wa SHIVYAWATA baada ya kutoka Ziarani Austaria
VYAMA vya Watu wenye ulemavu nchini,
wanakusudia kuishitaki serikali kwenye vyombo vya kimataifa, endapo
mauaji ya watu wenye ulemavu wangozi (Albino) yataendelea.
Akizungumza leo kwenye warsha ya
ujumuishaji wa watu wenye ulemavu, katika nyanja za maendeleo
iliyowezeshwa na EDAN ambayo ni programu ya Jumuiya ya Makanisa
Duniani, Mshauri wa mradi wa watu wenye ulemavu, kuhusu haki na
maendeleo yao,Dk. Elly Macha amesema Tanzania imesaini
mkataba wa kutetea haki za watu wenye
ulemavu,lakini imeshindwa kuwalinda na matokeo yake wanauwawa ovyo.
Amesema kuwa hali ya mauaji ikiendelea
kuwa kama ilivyo sasa, wataelewa wazi kuwa serikali imewaacha peke
yao na watalazimika kwenda kwenye vyombo vya kimataifa kuishtaki
serikali kw akushindwa kuheshimu mkataba huo.
Aidha amesema kuwa mbali na hilo katika
warsha hiyo wamkubaliana na kutoa wito kwa serikali
kusimamia,kuelekeza, kutekeleza na kufuatilia ujumuishaji wa watu
wenye ulemavu katika nyanja za maendeleo hususani, kuhakikisha
sera,sheria, mipango na upatikanaji wa rasilimali unawezesha
ujumuishaji wa masuala hayo.
Dk.Elly amesema kupitia warsha hiyo
wametoa tamko la kulaani mauaji ya kinyama ya Albino yanayoendelea
kutekelezwa kw akasi, hasa kanda ya ziwa na kuitaka serikali kuchukua
hatua madhubuti kukomesha tatizo hilo.
Naye Katibu Mkuu wa Shirikisho la
Vyama vya watu wenye ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA), Felician Mkude,
amesema kuna kesi nyingi zimeamuliwa na wengine wamehukumiwa
kunyongwa, ila mpaka sasa hakuna aliyenyongwa wapo magerezani,hivyo
wanaomba hukumu ikitolewa
izingatiwe, kwani isionee huruma
wahusika hao wanaoua wenzao kama wanyama.