WAY

Wednesday, July 25, 2012

KULWA KIKUMBA a.k.a DUDE AFUNGUKA KUHUSU SAKATA LA BAADHI YA WASANII FILAMU KUMCHUKIA ASEMA LAZIMA KIUNDWE CHOMBO CHA WASANII CHA KUSIMAMIA MAADILI AZUNGUMZIA SAKATA LAKE NA FROLAH MVUNGI

Msanii aliejizolea umaarufu katika tamthilia ya BONGO DAR-ES-SALAAM ambayo ilikua inaonyeshwa kwenye televisheni ya taifa TBC KULWA KIKUMBA a.k.a DUDE amesema kinachomfanya wasanii wenzake wengi wa filamu hasa wa kike wamchukie ni kutokana na kusimamia upande wa maadili na kukasirishwa na skendo zisizo na msingi wowte na mwisho wa siku kuonekana wasanii wote walio katika tasnia ya uigizaji hawana maana kutokana baadhi yao tu kupenda kuandikwa kwa mabaya na huku akisema yote hayo yanatokana na kutokua na usimamizi maalum na utaratibu unaoeleweka katika kuingia katika tasnia ya uigzaji na mwisho wa siku hata machizi wanaweza kuingia kwenye filamu lakini kwa sasa lazima wakae chini na kiundwe chombo maalum ambacho kitaweza kusimamia maadili na kumchunguza yoyte yule anaetaka kuigia katika tasnia hii ya uigizaji na pia dude akathibitisha kuwepo kwa wale ambao wanatengeneza skendo ili kuweza kuandikwa sana kwenye magazeti na ndio unakuta hata mwezi mzima watu watakaotamba kwenye vichwa vya magazeti ya udaku ni wasanii wa filamu au maigizo wakati kuna wanamichezo wengi tu ambao ni maarufu sasa kwanini wasanii wa maigizo hii ni kutokana na wengi kupenda kuandikwa sasa hata ukimkuta mwanamuziki basi ujue ana mahusianao na muigizaji sasa kwanini waigizaji ndio iwe wao tu hii ni kutokana na kutokua na utaratibu maalum wa kuingia katika tasnia ya filamu

PIA DUDE ameeweka bayana zile shutuma za kumjia juu msanii FROLAH MVUNGI na kusema ni kweli alimchana live FROLAH kwa kuwa ni msanii wake kwa tabia yake ya kuweka mambo yao ya chumbani hadharani kati yake na IRENE UWOYA na kusema huko ni kujidhalilisha na kuidhalilisha tasnia nzima ya filamu hivyo aliweza kumwambia aachane na mabo hayo ya kutangaziana mambo yao ya ndani

AIDHA DUDE amesema sasa ana mapngo wa kutengeneza mchezo mifupi mifupi na kuiweka kwenye CD ili watu wengi waipate na waweze kujifunza kuliko hii ya kufanya kwenye tv mwengine anaweza asione na akaibiwa vile vile na amesema pia mikataba ya kuonyesha michezo hiyo kwenye televisheni kwa sasa hailipi kutokana na mikataba iliyopo kwenye matelevisheni hivyo imebidi atumie njia hiyo ya kutnengeneza michezo hiyo na kuiingiza sokoni ambayo itakua inapatikana kwenye vcd na dvd huku akitanabiasha kuja kusini mwa tanzania katika kuweza kuweka mambo sawa.

0 comments:

Post a Comment

.

.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...