WAY

Saturday, July 21, 2012

MSANII ANAEKUJA JUU KATIKA BONGO FILM BHOKE WAMBURA WAMBURA AFUNGUKA KUHUSIANA NA SKENDO ZA KUTENGENEZA NA ASEMA JAMII ISICHUKULIE MAISHA YA FILAM KAMA NDIO MAISHA YAO HALISI

Akizungumza na KONA YA BONGO FILM ndai ya kipindi cha EXTRA AFRICA ndani ya SAFARI RADIO MTWARA TANZANIA. 
BHOKE WAMBURA anaetamba na movie kama NDANI YA GUNIA ambayo ndani yake kuna nguli wa maigizo DOTNATA,CLOUD, WOLPER ambapo ameigiza kwa umahiri wa hali ya juu pia yumo katika movie ya MY REAL MOM ya DOKII ambaye kwa mujibu wa bhoke ni moja kati ya wasanii waliomuinspire yeye kuingia kwenye filamu llicha ya binamu yake KAJALA MASANJA kuweza kumpa msukumo zaidi lakini dokii ndie alimpa saport kubwa sana ya kuingia kwenye film industries.
                                       BHOKE WAMBURA WAMBURA

 BHOKE amefunguka kuhusiana na jamii inavowachukulia kwa kile ambacho wanaigiza na kusema jamii lazima ielewe kuwa kile wanachofanya kwenye movies ni maigizo ya moja ya tabia ambazo zinapatikana katika jamii inayotuzunguka laki sio kwamba ndio tabia walionayo wao huki akitolewa mfano wa filamu mpya ambayo yeye atakua kinara ya RETURN OF THE J-LO ambayo inaandaliwa na kampuni ya STEP INTERTAIMENT ambapo ndani yake atakuwemo nguli wa kike katika filamu na mshindi wa tuzo kadhaa MONALISA,lakini pia atakuwemo mwanadada alitikisa katika tasnia ya maigizo kipindi hicho SINTA ambae kwa sasa najulikana kama J-LO wa bongo lakini pia atakuwepo mtangazaji maarufu aliegeukia filamu BEN KINYAIYA.
                                   COMING SOON THE RETURN OF THE J-LO
AIDHA BHOKE amefunguka kuhusiana na skendo ya kwamba wengine wanatengeneza stroy ili mradi kujipatia umaarufu amesema hilo sio kweli ila hilo huwa linatokea kwa marafiki au ndugu wa karibu wenye tamaa ya hela ndio huwa wanaenda kuuza pics au stroy kwenye magazeti na pia dhahiri inaonekana kwa sasa magazeti hayawezi kuuza bila wao na ndio maana wanafatiliwa sana lakini hakuna anaentengeneza ili kuweza kuwa maarufu.
Lakini pia amezungumzia filamu industries kuwa kwa sasa inakua sana tofauti na zamani ingawa wapo wengine ambao huwa hawajielewi na pia kusema wapo baadhi ambao wanachukulia filami kama kupata umaarufu na si kazi kama kazi zingine na kuna wale ambao mpka walale na producer ndio apewe sceen nzuri zaidi.BHOKE amesisitiza kuwa kwenye RETURN OF THE J-LO wategee vitu vizuri zaidi,
bhoke kwenye tasnia ya filamu si wa muda mrefu lakini kwa sasa ni mmoja kati ya wanaotikisa soko la filamu na anbayo hawajui basi bhoke ni mtu na binamu yake na KAJALA MASANJA huyo ndio  BHOKE WAMBURA WAMBURA ikitaka zaidi sikiliza mahojiano ya moja kwa moja aliyoyafanya na KONA YA BONGO FILM.
                                   BHOKE AKIWA NA KAJALA MASANJA

0 comments:

Post a Comment

.

.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...