Kamanda wa polosi mkoa wa Tabora kamishna msaidizi wa polisi Suzan Kaganda
Mtu mmoja aliefahamika kwa
jina Batholomeo Edward mkazi wa mtaa wa majengo mjini Nzega mkoani
Tabora amefariki dunia na mwingine kujeruhiwa vibaya kwa kupigwa
risasi na askari wa jeshi la polisi wakati wakisubiri matokeo ya
uchaguzi baada ya kupiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa
uliofanyika jana kote nchini.
Kaimu Mganga Mfawidhi wa
hospitali ya serikali ya wilaya ya Nzega Dkt. Joseph Bahati amesema
hospitali yake imepokea majeruhi wawili majira ya saa 11.00 alfajiri
mmoja akiwa amejeruhiwa tumboni na kitu chenye ncha kali kilichotowa
utumbo wake na mwingine ubavu na mkono wa kushoto na kuwa wakiwa
wanapewa matibabu mmoja wao akafariki dunia kutokana na kutokwa damu
nyingi.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa
tukio hilo limetokea majira ya saa 10.00 alfajiri katika mtaa wa
majengo ambapo baadhi ya wakazi wa eneo hilo wakiwa wakisubiri
matokeo msimamizi wa uchaguzi alimtangaza mgombea wa CCM, kuwa
mshindi hali iliyosababisha taharuki miongoni mwa vijana na hivyo
askari wa jeshi la polisi kuingilia kati na kuanza kuwatawanya kwa
kupiga mabomu ya machozi hewani na baadae kupiga risasi za moto na
kuwajeruhi Batholomeo Edward na Lucas Daudi ambao wanadaiwa kuwa ni
wafuasi wa umoja wa katiba ya wananchi (ukawa).
Viongozi wa Umoja wa
Katiba ya Wananchi (UKAWA) Wilayani Nzega wamelaani vikali kitendo
cha jeshi la polisi kutumia silaha za moto kuwatawanya watu waliokuwa
wakishangilia ushindi na hatimaye kusababisha mauaji hayo na kuwa
suala hilo watalifikisha kwenye vyombo vya sheria ili iweze kuchukua
mkondo wake.
Akizungumza kwa njia ya
simu Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora Bi. Suzan Kaganda amethibitisha
askari wa jeshi lake kutumia mabomu ya machozi na risasi za moto
zilizopigwa juu kutawanya mkusanyiko wa watu waliokuwepo eneo hilo.
0 comments:
Post a Comment