Mbunge wa Mbeya mjini Mh. Joseph Mbilinyi Maarufu kama Sugu
Tanzania ndiyo nchi pekee ambayo bado
inayowauzia wananchi wake mafuta kwa bei ya juu licha ya kuwa bei ya
mafuta katika soko la dunia kushuka kwa zaidi ya asilimia 50.
Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi
ameyasema hayo wakati akiongea na Wananchi wa Halmashauri ya mamlaka
ya mji mdogo wa Kyela na kusema kuwa kumekuwepo na bei kubwa ya
mafuta nchini ikilinganishwa na nchi nyingine.
Mh. Sugu amedai kuwa bei hiyo ya
mafuta ni kubwa ukilinganisha na nchi nyingine duniani ambazo gharama
za mafuta imeshuka zaidi ya nusu kutoka na kupatika kwa wingi kwa
bidhaa hiyo kwa sasa duniani.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chadema
Mkoa wa Mbeya, Joseph Mwachembe maarufu kwa jina la China amesema
kuwa katika maeneo ambayo Chadema imeshinda kuongoza serikali za
mitaa na vijiji, viongozi wake watafanya kazi kwa kuzingatia matakwa
ya wananchi na sio maelekezo kutoka serikali ku.
Nao viongozi wa Ukawa mkoani Mbeya
wamesema kuwa muungano wa vyama vinavyounda umoja huo umeonesha
mafanikio makubwa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na moto huo
huo utaendelea mpaka kwenye uchaguzi mkuu ujao.
0 comments:
Post a Comment