WAY

Sunday, December 28, 2014

KUCHELEWA KUCHUKUA MAAMUZI KATIKA SAKATA LA ESCROW KUMEKIANGUSHA CHAMA CHA MAPINDUZI SERIKA ZA MITAA-WASSIRA

   Mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi CCM, Mh Stephen Wassira
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi CCM, Mh Stephen Wassira,amekiri kuwa kutochukua hatua za mapema kuhusu sakata la uchotwaji wa fedha katika akanti ya tegeta escrow ni moja ya sababu ambayo imesababisha chama hicho kutofanya vizuri katika uchaguzi wa serikali za mitaa.

Mh, Wassira ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu ameyasema hayo nyumbani kwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Kijijini Butiama, ambapo amesema kitendo cha serikali kushindwa kutoa taarifa kwa wakati kimechangia kuwachanganya Watanzania kuhusu sakata hilo.

Hata hivyo mjumbe huyo amesema hivi sasa taifa linakabiliwa wimbi kubwa la baadhi ya viongozi wake kukosa uzalendo na uadilifu huku wakitanguliza mbele maslahi binafsi kitendo ambacho amesema kinaondoa dhana nzima ya kumuenzi baba wa taifa

0 comments:

Post a Comment

.

.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...