THE
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone:
255-22-2114512, 2116898
E-mail:
ikulucommpress@googlemail.com
Website :
www.ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425 |
|
PRESIDENT’S OFFICE,
STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzani
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Katibu
Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Yohana Sefue, amemsimamisha kazi kwa
muda Ndugu Eliakim Maswi, Katibu Mkuu ya Wizara ya Nishati na
Madini, ili kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake, kama
ilivyoelekezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa
Jakaya Mrisho Kikwete.
Balozi
Sefue amemsimamisha kazi Ndugu Maswi kuanzia leo, Jumanne, Desemba
23, 2014, kwa kutumia madaraka aliyonayo kama Mamlaka ya Nidhamu kwa
Watumishi wa Umma wanaoteuliwa na Rais, wakiwemo Makatibu Wakuu.
Taarifa
iliyotolewa na Ofisi ya Balozi Sefue mjini Dar es Salaam imesema kuwa
amechukua hatua hiyo “Kwa
mujibu wa Kifungu 4(3) (d) cha Sheria ya Utumishi wa Umma, Na. 8 ya
mwaka 2002 (kama ilivyorekebishwa)”
ambapo “Katibu
Mkuu Kiongozi ndiye Mamlaka ya Nidhamu kwa Watumishi wa Umma
wanaoteuliwa na Rais, wakiwemo Makatibu Wakuu.”
Badala
yake, Balozi Sefue amesema kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati
na Madini, Mhandisi Ngosi C. Mwihava atakaimu nafasi ya Katibu Mkuu,
Wizara ya Nishati na Madini, hadi uchunguzi dhidi ya Ndugu Eliakim C.
Maswi utakapokamilika.
Taarifa
hiyo ya Balozi Sefue pia imekariri kauli ya Rais Kikwete katika
hotuba yake kwa Taifa jana, Jumatatu, Desemba 22, 2014 ambako Rais
alisema:
“Kuhusu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, kwa vile ni Mtumishi wa
Umma, anatawaliwa na Sheria na Kanuni za Utumishi wa Umma, hivyo
nimeshaelekeza Mamlaka kuchunguza tuhuma zake na hatimaye ikibainika
ana makosa hatua za kinidhamu zitachukuliwa.”
Ndugu
Maswi, aliyekuwa Mwanasheria Mkuu Ndugu Frederick Werema pamoja na
Mawaziri wawili walituhumiwa wakati wa Kikao cha Bunge kilichopita
kuhusiana na Akaunti ya Tegeta Escrow.
Wakati
huo huo, Rais Kikwete ameelekeza kuwa pamoja na hatua nyingine
zinazochukuliwa, Shirika la Umeme (TANESCO) waendelee na majadiliano
na IPTL kuhusu uwezekano wa kushusha tozo la uwekezaji (capacity
charge)
zaidi ya punguzo la awali lililopatikana kupitia Kituo cha Kimataifa
cha Kusuluhisha Migogoro ya Kimataifa (ICSID).
Imetolewa
na:
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu
– Dar es Salaam.
23
Desemba,2014
0 comments:
Post a Comment