WAY

Tuesday, December 9, 2014

WANANCHI RUANGWA WALALAMIKIA UTAFITI WA MADINI WA MUDA MREFU BILA RIPOTI YOYOTE

Wananchi Wilayani Ruanga Mkoani Lindi wameitaka Serikali kchukua hatua juu ya Mwekezaji wa Kampuni ya Utafiti wa Madini PAC, mkoani humo baada ya kufanya utafiti huo kwa miaka sita bila kutoa ripoti yoyote wala kuchangia miradi yoyote ya Maendeleo.
        Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa akitoa ufafanuzi wa miradi mbele ya viongozi wa Serikali
Wakizungumza wananchi hao wamesema kwa miaka sita wameshudia maroli yakiondoka na udongo katika eneo hilo na hakuan taarifa yoyote juu ya mafaniko ya utafiti huo zaidi ya kuona wanaibiwa rasilimali zao bila faida yoyote.


Akizungumza hali hiyo mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Rubeni Mfini amekiri kuwepo kwa kampuni na kusema kuwa inakua vugumu kutatua mgogor huo kutokana na kukosekana ofisi ya madini katika wilaya hiyo.


Aidha Mkurugenzi huyo amesema kuwa kilio cha wananchi walishakipeleka kwa mkuu wa wilaya ambae tayari ameshamwandia katibu mkuu ambae amesema kuwa waziri wa nishati na madini atatembelea eneo hilo ili kutatua mgogoro huo.
MWISHO.
........................................... 
MKUU WA MKOA MWANZA AANZA NA POLISI

Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo, amelitaka jeshi la polisi mkoani hapa kutotumia nguvu pamoja na kufurumusha mabomu ya machozi kuwatimua wafanyabiashara ndogondogo maarufu machinga mara wanapoombwa na halmashauri ya jiji bila kupata maelekezo toka kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa.
              Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo akiongea na Waandhisi wa habari
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuhitimisha ziara yake ya ghafla katika wilaya ya Nyamagana, Mulongo amesema kamanda wa polisi wa mkoa huo, hatakiwi kuruhusu polisi wake kuwafyatulia mabomu machinga huku viongozi wa jiji wakiwa wamekaa ofisini bila kujishughulisha kusikiliza malalamiko yanayowakabili.


Aidha, Mulongo ameutaka uongozi wa halmashauri ya jiji la Mwanza kuhakikisha tatizo la uchafu linamalizwa ili kuliweka jiji hilo katika hali ya usafi zaidi.


Pia mkuu wa mkoa huyo amemtaka afisa afya wa jiji, Danford Kamenya na mwenyekiti wa kikosi kazi cha usafi wa jiji, Kaobwe Phidelis, kufanya mazungumzo ya amani na wafanyabiashara ndogo ndogo na kuwatafutia maeneo yaliyoboreshwa.
MWISHO.
................................................. 
 20 WASHILIWA NA JESHI LA POLISI MOROGORO KWA VURUGU ZA WAKULIMA NA WAFUGAJI

Watu zaidi ya 20 wanashikilia na jeshi la polisi mkoani Morogoro kwa nchini Tanzania kwa tuhuma za kuhusika katika mgogoro kati ya wafugaji na wakulima uliopelekea vijana kufunga barabara ya Morogoro, Dodoma katika eneo la dumila pamoja na Kuchoma Nyumba moto,
                         Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Morogoro Leonard Paul
Wakiongea kwa Jazba vijana hao wamesema kuwa wamechukua hatua hiyo kwa kuwa wamechoka kuonea na jamii ya wafugaji kwa kuwatishia kuwaua pindi mifugo yao inapokula mazao ya wakulima hao.


Wameongeza kuwa pia wameamua kufunga barabara baada ya kuona mashataka yao hayasikilizwi na serikali na kusema kuwa polisi wa eneo hilo wanaoneka kula njama na wafugaji hao na kiasi ambacho wanashindwa kuchukua hatua yoyote.


Akithibitisha kutokea kwa vurugu hizo kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Morogoro Leonard Poul amesema chanzo za vurugu hizo ni wazee zaidi ya kumi kuzuiwa kulima katika mashamba yao na kupeleka mashataka yao kwa afisa tarafa.
MWISHO.
.....................................

SHUGHULI ZA UZALISHAJI ZA KWAMA KWA UBOVU WA DARAJA KYAMABALE-BUKOBA

Wananchi wa kata Mikoni Wilayani Bukoba nchini Tanzania wameiomba serikali kujenga upya daraja la Kyamabale ambalo liliharibiwa na maji na sasa limekuwa kikwazo kwa wananchi na limesababisha mamia ya watu kupoteza maisha katika daraja hilo.
                  Meya wa Manispaa ya Bukoba Anatory Amani
Wakiongea wananchi wa kata hiyo wamesema watu wengi wamepoteza maisha katika daraja hilo ambalo sasa miundombinu yake imechakaa na sasa wamekuwa wakishindwa hata kuvusha mazao yao kwa ajili ya kuyasafirisha na kusababisha hasara kubwa kwa wananchi wanao ishi katika maeneo hayo.


Kwa Upande wake Diwani wa kata hiyo Pius Alibaliwo amekiri kuwepo kwa uchakavu mkubwa katika daraja hilo na kwamba amekuwa akifanya jitihada kwa viongozi wa halmashauri ya Bukoba ambapo amesema halmashauri sasa imetoa zaidi ya milioni miambili ambazo zitatumika kukarabati daraja hilo.

0 comments:

Post a Comment

.

.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...