Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein amewataka wafanyabiashara
wa Zanzibar kuwa wabunifu na wajasiriamali wa kuibua maeneo mapya
ya biashara na kuondoakna na mfumo wa kulingana.
Dkt. Shein ametoa changamoto hiyo
wakati akizindua mkutano wa nane wa baraza la biashara la Zanzibar
ambapo amesema Wafanyabishara wengi wamekuwa biashara zao zinalingana
hali inayosababisha kuwepo mazingira magumu na amewataka wabuni
maeneo mapya
Mapema waziri wa Biashara ,Viwanda na
Masoko Mhe Nassor Ahmed Mazrui alieleza mafanikio na mikakati ya
baraza hilo la biashara ambapo amesema ushirikiano wa sekta binafsi
na seriklai umeongezeka.
Baadhi ya wafanyabishara nao walipata
fursa ya kuelezea hali halisi ya mfumo wa biashara unavyokwenda
nchini.
huu ni mkutano wa nane wa baraza la
biashara la Zanzibar ambapo mwenyekiti wake na huwa rais wa Zanzibar
na kauli mbiu ya mwaka huu ni uimarishaji wa mazingira ya biashara
zanzibar na unahudhuriwa na viongozi na wafanyabisharawa zanzibar.
0 comments:
Post a Comment