Waziri wa Uchukuzi Dkt, Harrison Mwakyembe
Serikali ya Tanzania imesema udhibiti
wa vitendo vya wizi pamoja na idadi ya wateja wanaotumia bandari
kumechangia kuongezeka kwa kiwango cha mapato kutoka shilingi
bilioni 428 mwaka 2012 hadi kufikia shilingi bilioni 529 Juni mwaka
huu.
Akizungumza jana jijini Dar es salaam
Waziri wa Uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe katika mkutano wake na
wadau wa sekta ya uchukuzi wakiwemo wawakilishi wa wafanyabiashara
kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na kuongeza kuwa pia Mizigo
nayo ikiongezeka toka Tani Million 13.7 mwaka jana na kufikia Tani
Million 15.4 mwaka huu iliyoingia kupitia bandari hiyo
Kwa upande Mwingine Mwakyembe amemtaka
Mkurugenzi wa Kampuni ya Kimataifa ya Huduma za Makontena katika
bandari ya Dar es Salaam – TICTS, kufika kesho saa mbili kamili
asubuhi,ofisini kwa waziri kutoa maelezo kuhusiana na tuhuma kuwa
kampuni yake imekuwa ikitoza gharama za juu kubadilishia fedha za
kigeni tofauti na viwango vinavyotolewa na benki kuu ya Tanzania.
Kwa upande wao Wafanyaiashara toka
Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo wameulalamika mfumo mpya wa utoaji
na uingizaji migizo bandarini unaosimamiwa na mamlaka ya mapato
Tanzania kuwa umekuwa ukisababisha usumbufu na gharama zisizo na
msingi, tuhuma ambazo zimeungwa mkono na wamiliki wa bandari za nchi
kavu nchini.
0 comments:
Post a Comment