Katibu Mkuu wa Chadema
Dkt. Wilbrod Slaa
Chama
cha siasa upinzani cha Chadema, kimekosoa maamuzi ya rais Jakaya
Mrisho Kikwete kuhusu kashfa ya ubadhirifu wa fedha katika akaunti ya
Tegeta Escrow kwa madai kuwa hatua alizochukua hazikuzingatia
maazimio ya bunge.
Akizungumza
na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam leo, Katibu Mkuu wa Chadema
Dkt. Wilbrod Slaa amesema rais Kikwete ameshindwa pia kutumia mamlaka
ya kinidhamu aliyopewa na Katiba, kwa kushindwa kuwawajibisha
watuhumiwa wa kashfa hiyo hasa majaji wanaotuhumiwa kuhusika katika
sakata hilo.
Kwa
mujibu wa Dkt. Slaa, hata utenguzi wa nafasi ya Waziri wa Ardhi,
Profesa Anna Tibaijuka haukufanyika kwa kuzingatia misingi ya utawala
na kwamba hata kitendo cha kumweka kiporo Waziri wa Nishati na Madini
Profesa Sospeter Muhongo nacho kinaonyesha jinsi serikali
ilivyoshindwa kutekeleza maazimio ya bunge kuhusu hatua zinazostahili
kuchukuliwa watuhumiwa wa Escrow.
Hivi
karibuni Bunge la Tanzania liliapitisha maazimio nane ambapo miongoni
mwa maazimio hayo ilikuwa ni pamoja na serikali kuwachukulia hatua ZA
kinidhamu pamoja na kuwafuta kazi mawaziri na maafisa wa serikali
waliohusika katika sakata hilo.
0 comments:
Post a Comment