Waziri mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania
Waziri Mizengo Pinda amekatiza kwa
muda, ziara yake katika Falme za Kiarabu kwa maelezo kwamba ameitwa
nyumbani na Rais Jakaya Kikwete kwa shughuli maalumu.
Waziri Mkuu ambaye yuko katika ziara ya
kutembelea nchi za Falme za Kiarabu, ikiwa ni sehemu ya kudumisha
ushirikiano na kutafuta wawekezaji, amekatisha ziara hiyo siku mbili
baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema
kujiuzulu kutokana na kashfa ya Escrow.
Werema alijiuzulu juzi na Rais Kikwete
akaridhia hatua hiyo, huku umma ukisubiri hatua zaidi dhidi ya
mawaziri na watendaji wa Serikali waliotajwa katika sakata hilo.
Katika barua yake ya kujiuzulu, Jaji
Werema alisema ushauri wake wa kisheria kuhusu Akaunti ya Tegeta
Escrow haukueleweka na hivyo kuchafua hali ya hewa.
Kwa mujibu wa ratiba ya ziara hiyo, leo
Waziri Mkuu alitarajiwa kufanya mazungumzo na washiriki wa maonyesho
ya B2B pamoja na kutembelea maeneo mengine lakini ziara hiyo imefutwa
na badala yake anaondoka asubuhi kurudi nyumbani.
Baadaye leo Pinda alitakiwa kwenda
Doha, Qatar kwa ziara kama hiyo hadi Desemba 23.
Baada ya kukamilisha jukumu aliloitiwa,
Waziri Mkuu anatarajiwa kurejea Falme za Kiarabu Jumamosi kuendelea
na ziara yake.
fRoM Bbc
0 comments:
Post a Comment