Kamanda wa polisi mkoa we Kagera
Kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi Henry Mwaibambe
JESHI la Polisi mikoa ya Kigoma,Kagera
na Geita limezindua mpango endelevu wa kuuangamiza mtandao wa
uhalifu wa kutumia silaha kwa kuwatahadharisha wananchi kuepukana na
tabia ya kuwakarimu wageni wanaowatilia mashaka na badala yake
wawaripoti Polisi au kwa mamlaka zingine.
Tahadhari hiyo imetokana na baada ya
wananchi wa Kitongoji cha Mhama, kijiji cha Ilyamchele Wilayani
Bukombe Mkoani Geita Januari 19 mchana kujikuta wakiwakirimu
majambazi wakiwemo kutoka nchi jirani kwa chakula na vinywaji
wakidhania ni Askari wa hifadhi kutokana na nguo walizokuwa wamevaa
kufanana na sare za Askari wa hifadhi kumbe ni majambazi kabla ya
kuwageuka na kutoa silaha za kivita na kuwapora.
Sanjari na kuchukua tahadhari hiyo
wananchi wameombwa kutoa ushirikiano kwa polisi kwa kutoa taarifa za
siri zitakazoiwezesha polisi kuwanasa watu wote wanaoendesha vitendo
vya uhalifu wakiwemo wanaowaficha na wanaoshirikiana na watu kutoka
nchi jirani katika mikoa ya Kagera,Kigoma na Geita.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita
Kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi Joseph Konyo
Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita
Kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi Joseph Konyo amesema hayo leo
baada ya kikao maalum kati ya Kamanda wa polisi mkoa we Kagera
Kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi Henry Mwaibambe cha
kuzindua mkakati kabambe wa kuusaka mtandao wa uhalifu
kilichonfayika katika kijiji cha Nyakanazi Wilayani Biharamulo Mkoani
Kagera Juzi januari 20.
‘’Wananchi wabadilike ..kama siyo
mjambazi hao kuingiwa na hofu baada ya kupata taarifa ya kuwepo
porini kwa Kikosi cha kupambana na Uhalifu wa kutumia Silaha cha
mkoani Geita majambazi hao wangeweza kufanya kufuru lakini kwa
kuhofia hilo waliamua kufyatua risasi juu na kisha kuiba mchele kilo
60 na baiskeli tatu walizotumia kubebea mchele walioiba kabla ya
kuzitupa kwa kuhofia kukutana na kikosi cha Antroberry’’alidai
Konyo.
Aliongeza majambazi hao wanadaiwa
walifika katika kijiji hicho wamevaa nguo zinazofanana na sare za
Askari wa hifadhi na wanakijiji waliwakarimu kama watumishi wa
serkali kwa kuwanunulia chakula na vinywaji lakini mwanakijiji mmoja
aliwadokeza wenzake kuwa wale watu pamoja na kuvaa sare za Askari wa
hifadahi kwa juu lakini ndani walikuwa wamevaa sare za jeshi kama la
wananchi Jwtz lakini wenzake walimpuuza.
‘’Baada ya kukirimiwa pombe na
chakula ghafla watu hao walitoa bunduki za kivita ikiwemo bunduki
nzito inayodaiwa kuwa Light Mchine Gun[LMG]na kuwaamuru wananakijiji
waliokuwepo kukaa chini ya ulinzi kwa muda kwa kufyatua risasi hewani
na kisha kuondoka na kilo 60 za mchele na baiskeli tatu ambazo
baadaye walizitupa wakihofia kunaswa’’alisema Konya
Wakati wakitoka eneo la tukio
wakiondoka majambazi hao walichoma kibanda[Kijumba]kwa moto kwa lengo
la kuwafanya wanakijiji wasiwafuate na badala yake washughulikie
uzimaji moto kibanda kile na ndicho kilichofanyika na wakatumia fursa
hiyo kutoweka huku wanakijiji wakiwarushia mishale bila ya
mafanikio.
Kamanda Konyo alisema uchunguzi wa
kiintelijensia umebaini watu hao walivuka na kuingia nchi jirani
bila ya kuitaja kwa sababu za kiupelelezi…na ni sehemu ya mtandao
ambao umekuwa unaedesha uhalifu katika mikoa ya Kagera,Kigoma na
Geita huku pori la akiba la Kigosi lililopo wilayani Bukombe
linalopakana na wilaya za Biharamulo mkoani Kagera na mkoa wa Kigoma
likitumiwa kama maficho ya wahalifu hao.
Hata hivyo watu hao walitupa baiskeli
hizo baada ya kuhofia kukutana na Askari wa kikosi maalum cha
kupambana na Uhalifu wa kutumia silaha[Ant-robberry]na kufanikiwa
kutokomea kabla ya Askari kufika eneo la tukio hata hivyo taarifa
zilizokwishapatikana za kiintelijensia zimedaiwa zitasaidia kuunasa
mtandao huo na kuwataka wahalifu wote kujisalimisha wao au silaha zao
kwani siku zao zimehesabiwa kutoka sasa iwapo wananchi nao watasimama
kidete kutoa ushirikiano kuwafichua wahalifu hao kwani wanawatambua
na baadhi wanaishi nao.
Inasadikiwa mtandao huo ni sehemu ya
mitandao ya uhalifu wa kutumia silaha iliyopo katika Miji ya
Lunzewe,Namonge,Kasanda na Mabamba iliyopo katika mikoa ya
Geita,Kagera na Kigoma na baada ya hapo huvuka na kuingia nchi
jirani na hushirikiana na wenyeji ambao wao huratibu utekelezaji wa
matukio hayo na wageni huja kutekeleza.
Kikosi nguvu kazi hicho
kitakachowashirkisha makachero na wale wa Kikosi cha kupambana na
unyang’anyi wakutumia silaha katika mikoa mitatu kitakuwa kiungo
mhimu katika utekelezaji mkakati huo huku ukiwemo mfumo wa
kubadilishana taarifa za uhalifu na zile za
kikachero’’kiintelejensia’’katika mikoa hiyo mitatu kwa lengo
la kuufyeka kabisa mtandao huo ambao umekuwa kero kubwa katika mikoa
ya Geita,Kagera na Kigoma
Hata hivyo wadau waliohojiwa mkoani
Geita kwa masharti ya kutotajwa majina yao juu ya hali ya uhalifu
mkoani humo wamesema idadi ya matukio ya uhalifu wa kutumia silaha
yamepungua ikilinganishwa na miaka miwili iliyopita kulikochangiwa
na ushirikishwaji wa wananchi kwa kuhakikishiwa usalama wao katika
kufichua uhalifu…baada ya kutoa taarifa za siri badala ya
kusalitiwa na Askari wasio waadilifu kwa kuzigeuza kuwa dili.
Wamesema hatua hiyo inatokana na Timu
madhubuti iliyopikwa na uongozi uliopo sasa wa polisi mkoani hapa kwa
kurejesha imani kwa wananchikwa kuwalindawatoa taarifa za siri na
kusikilizwa,pia kikosi cha Kuapambanana uhalifu wakutumia silaha
kimekuwa imara wakati wote tofuati na awali.
Mwaka jana watu wanaosadikiwa kuwa
majambazi walivamia kituo kikuu cha polisi wilaya ya Bukombe Mkoani
Geita na kuua Askari wawili na kupora silaha,lakini kutokana na
ushirikiano kati ya polisi na wanachi watuhumiwa waliweza kukamatwa
pamoja na silaha zote zilizokuwa zimeibiwa.