WELCOME TO GMBONGO BLOG

To keep the body in good health is a duty... otherwise we shall not be able to keep our mind strong and clear.

TANGAZA NASI SASA

Tuwasiliane kwa Email: gmbongo.chuma@gmail.com

WE ARE HERE TO SERVE YOU

Keep you Entertained always

WE ARE HERE TO SERVE YOU

Habari na Burudani

WELCOME TO GMBONGO WORLD

Kwa habari za Burudani na zenye uhakika.

WAY

Thursday, January 30, 2014

KALUNDE BAND KUZINDUA ALBUM YAO KWENYE KUTIMAMIZA MIAKA NANE YA BAND HIYO NI VALENTINE DAY PALE GIRRAFE,BOD RUDALA,SARAFINA MSHINDO,JUNIOR KUREJEA BONGO KWA AJILI YA UZINDUZI WAONGEZA MADANSA KUTOKA AKUDO

Baada ya mwaka jana kushindwa kuzindua album yao kutokana na wasanii wengi ambao ni watunzi  walikua nje ya nchi wakipiga miziki kwa mikataba maalum ambapo mikataba hiyo ikiwa inaelekea ukikongoni mwezi na hivyo kurejea bongo ndipo mkurugenzi na mwimbaji wa band hiyo DEO MWANAMBILIMBI alipofunguka kwa wanataka kuzindua album hiyo siku ya VALENTINE DAY ambayo ndio itakua siku ya birthday ya band ya kutimiza miaka nane tangu kuaznishwa kwake na huku wakitarajia album hiyo kuwa na nane wakiongeza nyimbo mbili zaidi moja ikiwa rhumba na nyingine chakacha,


DEO amesema wasanii walionda nje ya nchi kwa ajili ya kazi ya kimuziki anatarajia kurudi bongo kasoro mpiga gita mmoja ndio hataweza kurudi kutokana na kubwana na mktaba wa band yake nchini malysia,lakini BOB RUDALA aliekuwa sweeden atarudi soon na SARAFINA MSHINDO aliebangladesh nae atarudi na JUNIOR GRINGO alieko ITALIA nae yuko mbioni kurudi kwa ajili ya uzinduzi huo huku deo akijatamba kwa kuongeza safu ya mashumbulizi katika show kwa kuongeza wacheza show waili kutoka AKUDO IMPACT lakini pamoja na muimbaji mmoja kutoka LAVENT ya morogoro,

Tuesday, January 28, 2014

ALIYEKUWA mwanamuziki mahiri wa bendi ya African Stars 'Twanga Pepeta' Soud Mohammed (MCD) amefariki usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya KCMC-Moshi.

ALIYEKUWA mwanamuziki mahiri wa bendi ya African Stars 'Twanga Pepeta'  Soud Mohammed (MCD) amefariki usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya KCMC-Moshi.
Taarifa kutoka ndani ya Twanga Pepeta usiku wa jana, zinasema kuwa MCD alikuwa amelazwa hopsitalini hapo kwa kusumbuliwa na akiwa anasumbuliwa na matatizo ya miguu.
Inaelezwa kuwa mwanamuziki huyo aliyewahi kuwa Bingwa kucheza Disko mkoa wa Kilimanjaro kabla ya kujitosa kwenye muziki wa bendi alifariki majira ya saa saa 2:30 usiku.
Enzi za uhai wake MCD aliwahi kuzipigia bendi ya Diamond Sound 'Wana Ikibinda Nkoy', Twanga Pepeta na hivi karibuni alihamia Mashujaa Band kabla ya kurejea Twanga ambapo aliondoka wiki kadhaa kuelekea kwao Kilimanjaro kujiuguza na kukutwa na mauti hayo.
                                                MASOUD,ME AND MAREHEMU MCD
Safari rado inatoa pole kwa wanafamilia, ndugu na jamaa za mwanamuziki huyo pamoja na kuwapa pole wana Twanga Pepeta na wadau wa muziki wa ujumla.
Mzishi ya msanii huyo yanatarajiwa kufanyika leo mchana mjini Moshi,Mungu aiweke roho ya marehemu Mahali Pema Peponi.
Taarifa kutoka ndani ya Twanga Pepeta usiku wa jana, zinasema kuwa MCD alikuwa amelazwa hopsitalini hapo kwa kusumbuliwa na akiwa anasumbuliwa na matatizo ya miguu.
Inaelezwa kuwa mwanamuziki huyo aliyewahi kuwa Bingwa kucheza Disko mkoa wa Kilimanjaro kabla ya kujitosa kwenye muziki wa bendi alifariki majira ya saa saa 2:30 usiku.
Enzi za uhai wake MCD aliwahi kuzipigia bendi ya Diamond Sound 'Wana Ikibinda Nkoy', Twanga Pepeta na hivi karibuni alihamia Mashujaa Band kabla ya kurejea Twanga ambapo aliondoka wiki kadhaa kuelekea kwao Kilimanjaro kujiuguza na kukutwa na mauti hayo.
Safari rado inatoa pole kwa wanafamilia, ndugu na jamaa za mwanamuziki huyo pamoja na kuwapa pole wana Twanga Pepeta na wadau wa muziki wa ujumla.

Mzishi ya msanii huyo yanatarajiwa kufanyika kesho mchana mjini Moshi,Mungu aiweke roho ya marehemu Mahali Pema Peponi.

Monday, January 27, 2014

BAADA YA UZINDUZI WA ALBUM YA NINI YA FM ACADEMIA LAKINI ALBUM YENYEWE HAIONEKANI MITAANI RASI WA FM ACADEMIA NYOSHI ELSAADAT ALITOLEA UFAFANUZI ASEMA WAMEPELEKA NYIMBO ZOTE NJE KUZIFANYIA MASTERING ILI KUEPUKA MAHARAMIA LAKINI PIA NI KATIKA KUWAPA WATU HAMU YA KUITAFUTA ALBUM ILI KIINGIA SOKONI IPAPATIKIWE ASEMA HIYO NDIO STYLE YAO MPYA KATIKA BIASHARA YA MUZIKI

Licha ya tar 21-dec 2013 Kuizindua rasmi album ya CHUKI YA NINI pale mzalendo pub lakini album hiyo hiyo imekua ikiuliziwa na mashabiki kwa kuwa kila wakienda sokoni hawaipati na wala kwenye maonyesho ya fm academia pia hawaipati zaidi ya kupata nyimbo hizo live,kutokana na hili nikaona nimtafute rais wa fm academia NYOSHI EL SADAAT SAUTI YA SIMBA ili aweze kulitolea ufafanuzi suala hili ndipo alipofunguka na kuweka wazi kuwa kwa sasa audio na video za album hiyo wamezipeleka nje kwa ajili ya kufanyiwa mastering ili zisiwezi kuibiwa kirahisi lakini pia amesema kwa kufanya hivyo ni kuongeza soko kwa mashabiki wa band hiyo kwa kuwa watakuwa na hamu sana ya kuitaka album hiyo na pidnipo watakapoiingiza sokoni basi itaweza kupapatikiwa sana kwa sababu kila mtu atakuwa na hamu nayo ila uzinduzi walioufanya ni kwamba kuanza sikuh hiyo itakua rasmi wanapiga nyimbo za kwenye album mpya na kuwazoesha mashabiki na huku akisema soon wakae tayari kuweza kupata wimbo mpya wa OTILIA ambao utakua katika album hiyo,

                                               NYOSHI, ME AND KING BLAISE
AIDHA amewataka mashabiki wa fm academia wasichoke kusubiri album hiyo ya chuki ya nini ambayo imesheheni nyimbo nzuri nyingi zinazovutia zaidi na tafauti na miaka yote kwa kuwa walikaa kimya muda mrefu kwa ajili ya kuweza kutoa album itafunika hata zile vuta nikutvute na hata duniak kigeugeu

Thursday, January 23, 2014

TWANGA PEPETA YAHAIRISHA ZOEZI LA KUPUNGUZA WANAMUZIKI SASA WAAMUA KUBAKI NAO ILA ATAKAEPATA SEHEMU NYINGINE HAKATAZWI KUONDOKA MWAKU HUU KUTOTOA ALBUM YOYOTE ZAIDI YA SINGO-MANENO YA RAIS WA BAND MAAMA LUIZA NYONI MBUTU

akiongea na blog hii ya abracadabra LUIZA MBUTU nilipomuuliza kuhusiana na zoezi la kutengeneza band kwa kupunguza wanamuziki wambao wanaonekana mzigo kwa band kwa kuongeza gharama bila kuwa na kazi yoyote luiza mbutu amesema mkurugenzi wa band hiyo ameghairi kufanya hivyo kutokana na kila mtu anaemgusa kulia na matatizo yake na kuogopa kuaibika kutokana na kujipanga kimaisha pamoja na mjuku mengine ya kifamilia hivyo imebidi awaache na kuendelea kuwa nao mpka kila mmoja atakapoona amepata sehemu ya kujishikiza basi ni ruhusa kufanya hivyo na kusema wote waliosimamishwa wamerudishwa kazini kama kawaida.


Akiongea kuhus kutoa album kama kawaida ya twanga kwa kila mwaka amesema kwa mwaka huu hawezi kutoa tena album bali wataweza kutoa singo ili kuweza kuipisha album ya nyumbani ni nyumbani kufanya vizuri katika soko baada ya serikali kuweka mfumo mzuri wa uuzwaji wa wa kazi za wasanii kwa sasa hviyo wapenzi wa twanga wategemee sana kupata singo za twanga badala album kama walivyozoea kupata miaka yote iliyopita

Baadhi ya mabasi yanayofanya safari zake kupitia barabara ya Dodoma hadi Dar es Salaam yamesitisha safari hizo kutokana na kuvunjika kwa daraja la eneo la Dumila mkoani Morogoro.

 Baadhi ya mabasi yanayofanya safari zake kupitia barabara ya Dodoma hadi Dar es Salaam yamesitisha safari hizo kutokana na kuvunjika kwa daraja la eneo la Dumila mkoani Morogoro.
Kutokana na mabasi hayo kukataisha safari zake  abiria wanaopita njia hiyo wamepata wakati mgumu kutafuta usafiri wa kufika huko, huku nauli za mabasi zikiwa juu.
Akizungumza na kituo hiki, Wakala Mkuu wa mabasi katika stendi ya Mkoa wa Dodoma, Rashidi Zuberi amesema baadhi ya mabasi yamekatisha safari zao lakini mengine yanaendelea na safari kama kawaida kupitia njia ya Iringa.
“Asubuhi mabasi yote yalikuwa yanapitia Iringa kwa nauli ya Sh. 30,000 badala ya Sh. 17,000 hadi Sh. 22,000 lakini baadae tulivyoona mabasi ya Mwanza yakipita njia ya Kilosa na mabasi mengine yameanza kupitia njia hiyo ya Kilosa.
“Hata hivyo mabasi kama Shabiby na Kimbinyiko naona wenyewe wameamua kusitisha safari zao labda wanahofia ubovu wa barabara ya Kilosa,” alisema
Akizungumzia hali hiyo, mfanyakazi wa Ofisi ya Mabasi ya Kampuni ya Shabiby, Mushi Abdul amesema  kuwa mabasi ya Shabiby yalifanya safari zake, mwisho basi la saa tatu asubuhi kwa kupitia njia ya Kilosa.
“Safari za mabasi mengine zimesitishwa na tiketi zilizokuwa zimeuzwa jana kwa basi la saa tano tumewarudishia abiria fedha zao,” alisema
Hata hivyo kulikuwa na idadi ndogo ya mabasi ambayo yalikuwa yanapakia abiria kwa siku ya leo tofauti na siku nyingine.
Akizungumzia adha hiyo ya usafiri abiria aliyekuwa anatafuta usafiri wa kwendaa Jijini Dar es Salaam, Michael Lembu alisema tangu amefika kituoni hapo anatafuta usafiri lakini bado hajapata.
“Tunaiomba Serikali ifanye haraka kujenga daraja lililobomoka ili safari zirejee kama kawaida,” alisema.
Kwa upande wake  mmoja wa wakala wa mabasi katika stendi hiyo ambaye hakutaka  kutaja jina lake alisema nauli ya Dodoma hadi Dar es Saam kwa njia ya Kilosa imepanda kutoka Sh. 17,000 hadi Sh. 20,000 na kwa mabasi ya Luxury nauli ni Sh. 30,000.
“Hata hivyo barabara ya Kilosa ni mbaya kuna baadhi ya magari ambayo yana matairi mawilimawili hayawezi kupita,” alisema.
Mwisho.

HILI NDIO TAMKO LA CHAMA CHA MAPINDUZI KUHUSU MAWAZIRI MIZIGO PAMOJA NA TAMKO LA UTEUZI WA MAWAZIRI WAPYA SOMA HAPA

Mara baada ya kuundwa kwa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa inayoongozwa na Katibu Mkuu Ndg. Abdulrahman Kinana mwanzoni mwaka mwaka jana, Sekretarieti hiyo imejiwekea utaratibu wa kufanya ziara mikoani kukutana na wananchi kusikiliza kero zao,kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na kuimarisha Chama mikoani. Utaratibu huu ni agizo la mkutano mkuu wa Taifa wa nane wa CCM uliofanyika Novemba 2012 mjini Dodoma. Nanukuu azimio hilo;

“ Chama Cha Mapinduzi lazima kiwe karibu na wananchi, kisikilize changamoto zao na kiwasemee wananchi na hasa wanyonge” Moja ya maazimio ya Mkutano Mkuu wa nane wa CCM 2012.

Kwa hiyo msingi wa kwanza wa ziara hizo ni maagizo ya Mkutano Mkuu wa CCM Taifa ambacho ndicho kikao cha juu kabisa cha Chama. Msingi wa pili ni ukweli kuwa CCM ndio iliyopewa dhamana na kuingia mkataba na wananchi kupitia ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010/2015, hivyo inayowajibu wa kukagua utekelezaji wa ilani hiyo.

Na bila shaka wote tumeshuhudia jinsi ziara hizo zilivyoinua uhai wa Chama nchi nzima na kuongeza kasi ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi na kutatua kero mbalimbali za wananchi kwenye maeneo yao, kiasi cha kuongeza imani ya wananchi kwa CCM.

Tumeshuhudia makundi mbalimbali ndani ya jamii yakija kueleza changamoto zao ndani ya Chama. Makundi hayo ni pamoja na makundi ya wakulima, wafugaji, wafanyabiashara, wanafunzi na wafanyakazi hasa walimu. Huu ni uthibitisho wa kuongezeka kwa imani yao kwa CCM.

Katika mwendelezo wa ziara hizo mwishoni mwa mwaka jana Katibu Mkuu wa CCM na baadhi ya wajumbe wa Sekretarieti walifanya ziara ya siku 26 katika mikoa ya Ruvuma, Mbeya na Njombe. Pamoja na mambo mengine wananchi walilalamikia baadhi ya watendaji wa serikali hasa baadhi ya mawaziri wakiamini kuwa yapo mapungufu kadhaa yanayotokea kwenye wizara zao.

Naomba upokee tamko hili kutoka kwa katibu wa itikadi na uenezi ndugu Nape Nnauye, alilolitoa leo majira ya saa nne, makao makuu ya chama cha mapinduzi CCM jijini dar es salaam mbele ya waandishi wa habari.

NB: komputer yangu adobe inasumbua so natuma sauti, utaandaa hii habari ni nzuri sana kwetu.

Tamko

CCM kama lilivyo agizo la Mkutano mkuu la kuwasemea wananchi tulisikiliza kilio chao na kwa kufuata utaratibu, baadhi ya mawaziri hao waliitwa na kuhojiwa kwenye Kamati Kuu ya CCM mwezi Disemba 2013.

 Utaratibu wa watendaji wa serikali kutoa taarifa za utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwenye vikao vya Chama sio mgeni na wala haujaanza jana. Wakuu wa wilaya hutoa kwenye wilaya, wakuu wa mikoa hutoa mikoani kwao,hivyo sio utaratibu mpya.

Baada ya mahojiano hayo Kamati Kuu ya CCM ilitoa ushauri kwa serikali wa namna ya kurekebisha mapungufu yaliyoelezwa na wananchi. Kwakuwa kwa mujibu wa Katiba ya Nchi mwenye mamlaka na mawaziri ni Rais mwenyewe, CCM ililiacha suala hili kwake aangalie njia ipi bora ya kuondoa mapungufu tuliyoyaeleza.

Na kwenye taarifa yetu kwa vyombo vya habari baada ya kikao hicho tulisisitiza kuwa sio lazima awafukuze mawaziri husika isipokuwa wanaweza kufanya mabadiliko katika mfumo,sheria nk ili mradi kuwepo na mabadiliko katika kushughulikia mambo yaliyolalamikiwa na wananchi.

Hivi karibuni Rais amefanya mabadiliko kidogo kwenye baraza lake la mawaziri na kuwarudisha baadhi ya mawaziri waliolalamikiwa na wananchi na wabunge, ambao malalamiko hayo yaliungwa mkono na CCM. Ni kupitia malalamiko hayo ndipo lilipozaliwa jina la mawaziri mizigo. Baada ya uteuzi huo kukaibuka mjadala mkubwa nchini wakihoji kulikoni Rais kaamua kutowatimua mawaziri hao.

Kwanza haikua hoja ya CCM kuwafukuza mawaziri hao bali kuchukua hatua za kurekebisha mapungufu husika. Kufukuza inaweza kuwa ni njia ya kutatua tatizo lakini sio njia pekee. Hivyo basi CCM tunaamini kuwa kurudishwa kwao wamepewa fursa ya kurekebisha mapungufu tuliyoyasema kwa niaba ya wananchi. Tunaamini mawaziri wote hawatabweteka bali watatimiza wajibu wao na kuhakikisha wanawatumikia wananchi ambao ndio waajiri wa serikali.

Ifahamike kuwa Chama Cha Mapinduzi hakitasita kuchukua hatua kali dhidi ya mawaziri na watendaji wengine watakaoshindwa kurekebisha mapungufu na watakaoshindwa kutimiza wajibu wao vizuri. Wakumbuke kushindwa kwao kutimiza majukumu yao ni hujuma kwa Ilani ya uchaguzi ya CCM, CCM haitavumilia usaliti huo. Kukaa kimya kwa CCM itakua ni kujinyonga yenyewe jambo ambalo hatutaruhusu kabisa.

Tunajua wapo baadhi ya watendaji wa serikali wasiopenda kuhojiwa utendaji wao, tunawasihi kwa moyo safi wasiotaka kuulizwa juu ya utendaji wao waondoke serikalini wenyewe kwani CCM tutakuwa wakali sana kwenye mapungufu,kwani tukikaa kimya tutakua tunajihujumu wenyewe.

Tutatumia vizuri wingi wa wabunge wetu bungeni na wingi wa madiwani wetu kwenye halmashauri kuisimamia vizuri serikali. Hivyo kuanzia sasa kasi ya CCM kuisimamia serikali, kuisifu itakapofanya vizuri na kukosoa itakapofanya vibaya itaongezeka mara dufu kwa kila ngazi.

Tunawaomba watanzania kwa ujumla tuwape muda wateule hawa wa Rais watimize wajibu wao, lakini tusisite kusema pale tutakapoona mambo hayaendi kama tunavyotarajia. Uwajibikaji wa kweli ndio msingi wa mafanikio na maendeleo yetu.

CCM inawatakia kila lakheri kwenye kutimiza wajibu wao. Tuna matumaini makubwa kuwa wote kwa pamoja hawataisaliti ilani ya Uchaguzi ya CCM na kwamba hawatayaangusha matumaini ya wananchi kwa serikali yao.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI!

 MWISHO

MAJERUHI WA AJALI YA ILIYOHISHA WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI SABODO WANAENDELEA VIZURI BAADA YA KUPATA MATIBABU BAADA YA KUPATA MATIBABU KATIKA HOSPITAL YA LIGULA MKOANI MTWARA.

Majeruhi wa ajali ya iliyohisha wanafunzi wa shule ya sekondari sabodo wanaendelea vizuri baada ya kupata matibabu baada ya kupata matibabu katika hospital ya ligula mkoani mtwara.
Wakiongea na safari radio baadhi ya wanafunzi hao ambao wamejeruhiwa wameelezea hali zao zinavyoendelean a pia jinsi ya tukio lilivyokuwa
Aidha wazazi na wauguzi wa majruhi hao wameshukuru madaktari nawauguzi wa hosptali ya ligula kwa kuweza kuwahudumia wanafunzi hao kwa umakini katika kuokoa maisha yao.
Jana asubuhi Wanafunzi wa watano  wa shule ya sekondari sabodo walifariki dunia  katika ajali ya gari iliyotokea kijiji cha msijute halmashauri ya mtwara vijijini.
Akizungumzia tukio hilo kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa mtwara zelothe steven amesema ajali hiyo imelihusisha gari namba T-174AEB Mercedes benz lililokuwa likitokea manispaaa ya mtwara kuelekea lindi likiendeshwa na dereva bw. Bakari mgwegwe.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya mkoa wa mtwara bw WILMAN NDILE amesema tukio hilo limewashtua sana na kwa sasa wameshaunda kamati ya kuweza kushughulia mazishi ya wanafunzi hao.

MWISHO

Tuesday, January 21, 2014

JE WAJUA? ALLY CHOKI ILIMLAZIMU KULALA CCM SEHEMU ZA KUOGESHEA MAGARI WAKATI ANATAFUTA KUTOKA KIMUZIKI ASEMA HATA BAADA YA KUMALIZA SHULE ALIEDNELEA KUTUMIA UNIFORM ILI AWEZE KUPANDA DALADALA KWA BEI RAHISI AKAPIGE MIZIKI DAR KUTOKA KIBAHA nNA LEO NDIO MKURUGENZI WA EXTRA BONGO

Leo katika je wajua mkurugenzi wa EXTRA BONGO le kamarade ally choki amesimuli alipotokea katika muziki na changamoto alizokutana nazo katika muziki ni pamoja kuweza kulala katika sehemu za maegesho ya magari tena usiku mnene na kuamika asubi sana kuendelea na harakati zingine mpka alipoweza kupata band katika miaka ya 87 na kuanza kuimba na mwisho wa siku kuweza kuelekea hadi nchini kenya lakini hata hivyo kitu kingine anachokikumbuka ni kuweza hata baadaa ya kumaliza shule aliweza kuendelea kuvaa uniform ili aweze kupanda daladala kwa bei ya mwanafunzi ali aweze kwenda kufanya miziki mjini dar kutokea kibaha

Akizungumzia siri ya mafanikio yake katika muziki amesema inatokana na juhudi pamoja kuupenda muziki na ndio maana mpka leo ameweza kujielewa na kuweza kusimama na band yake mwenywe ingawa kuna wenzake walitoka pamoja huko ila kutokana na mipango wengine wameshindwa kufanya kama alivyofanya yeye ila anasema malengo aliyoyaweka toka aanza muziki ndio yaliyomfikisha mpka alipo hii hii leo.
 
   
ALLY CHOKI amelia sana na wakurugenzi wa baadhi ya band kwa kuwa wabania wanamuziki kwa kutaka wasipate kama wanavyopata wao yaani viongozi wengi hawapendi kuona mwanamuziki wake anaendesha gari ya thamani zaidi yake kitu ambachokwa mujibu wa ally choki ni wivu usiokuwa na maendeleo au hata mwanamuziki akitaka kufanya kazi yake njee ya kundi au kwenda kutafuta maisha au kumjali mwanamuziki baada ya kuungua nacho ni kitu ambacho anasema wakurugenzi wanatakiwa kutoa vipaumbel zaidi.

Wazazi wilayani MASASI wametakiwa kuipa eilimu kipaumbele

MASASI 20/1/2014
Wazazi wilayani MASASI wametakiwa kuipa eilimu kipaumbele,sambamba na kuacha mitazamo hasi na potofu.
Hayo yameelezwa na mwalimu mkuu wa  shule ya msing CHIGUGU wilayani Masasi Bw.YOHANA ABUNUAS wakati akizungumza na safari radio ofisini kwake.

ABUNUAS amesema miongoni mwa changamoto kubwa wanazo kumbanana nazo wilayani Masasi ni mwamko mdogo wa wazazi wa kutambua umuhimu wa elimu kwa watoto wao,kama wazazi wataipa elimu kipaumbele elimu itakua mkombozi kwa vijana wengi hapa nchini.

Aidha amelaani kitendo cha baadhi ya wazazi na walezi kupuuza umuhimu wa elimu na kushindwa kupeleka watoto wao shule pasipo sababu yeyote ya msingi.

Katika Hali isiyo ya kawaida shule ya msingi CHIGUGU hadi kufikia January 17 mwaka huu jumla ya watoto 35 pekee ndio wameandikishwa darasa la kwanza ,huku matarajio ya shule hiyo ikiwa ni kuandikisha watoto 135 wasajiliwe darasa la kwanza.

Kufuatia hali hiyo ABUNUAS amewahimiza wazazi na walezi wenye watoto wanao stahili kuingia darasa la kwanza wapelekwe  shule kwani hiyo ni haki yao ya msingi.
BEATRICE RIWA



Vijana wilayani Lindi wametakiwa kujiunga na vikundi mbalimbali vya uzalishaji mali ili kuweza kujipatia fursa ya kujikwamua kimaisha

Vijana wilayani Lindi wametakiwa kujiunga na vikundi  mbalimbali vya uzalishaji mali ili kuweza kujipatia fursa ya kujikwamua kimaisha  badala ya kujiingiza kwenye makundi ambayo hayana tija.
 
Wito huyo umetolewa na mkuu wa wilaya Lindi Dk Nasoro Himidi wakati alipofunga mafunzo ya  ujasilimali Kata ya Chiponda jimbo la Mtama yaliyodhaminiwa na mbunge wa jimbo hilo Bernard Membe.
 
Dk Nassoro alisema wilaya Lindi inavijana wengi wenye uwezo wa kufanya kazi za uzalishaji lakini kinachokosekana ni vijana kutokujitambua, hivyo ni vyema wakajikita kwenye vikundi vya uzalishaji mali ili kuepukana kujiunga na makundi mabaya.
 
Alisema lengo la viongozi wetu akiwemo mbunge wenu dhamira yake kuwakuza na kuwaendeleza kijasiliamali  ili mwisho wa siku muweze kujimudu kimaisha  tofauti na ilivyo hivi sasa vijana wengi ujiingiza katika makundi mabaya na wengine wakiishi vijiweni.
 
Akizungumza kwa niaba ya washiriki wa mafunzo hayo Zuwena Yusuph alisema kuwa wajasiliamali 97 wanawake 45 na wanaume 52 kutoka vikundi 9 vya ujenzi, kilimo,useremala,ufugajikuku  na nyuki mama Lishe na ufyatuaji wa matofali.
 
Zuwena alisema wanavikundi hao wanaojiusisha na uzalishaji wamepata elimu ya ujasiliamali ikiwemo ya utunzaji wa vitabu vya hesabu kuwa mafunzo waliyopata yatasaidia kuwaongeza uelewa jinsi ya kuendesha biashara, kutafuta masoko ,kutunza mitaji pamoja na ushindani wa soko.
 

Kaya zaidi 60 katika kijiji cha Mtama jimbo la Mtama wilaya Lindi zimekosa makazi kufuatia nyumba zao kubomolewa na mvua iliyoambatana na upepo.

Kaya zaidi 60 katika kijiji cha Mtama jimbo la Mtama wilaya Lindi zimekosa makazi kufuatia nyumba zao kubomolewa na  mvua iliyoambatana na upepo.
 
Mkazi wa kijiji hicho Zainabu Isa alisema kwamba mvua hiyo ilianza kunyesha zaidi ya masaa saba kuanzia saa 9 alasiri hadi saa 5 usiku na kusababisha hasara ya kuharibu nyumba na chakula ambayo thamani yake haijatambulika hadi sasa,
 
zainabu alisema wakati mvua hiyo inanyesha maji yalikuwa yakitokea ardhini  na kuungana na  mvua yaliyokuwa yakitoka juu na kusababisha kubomoa nyumba za wakazi wa kijiji hicho.
 
Alisema mvua ilipokuwa ikiendelea kunyesha watu walioathiriwa waliweza kuhifadhi kwenye nyumba za majirani mpaka mvua iliponyamaza majira ya saa tano usiku,
 
Kwa upande wake mtendaji wa kijiji cha Majengo ‘A’ Safu Hamisi alisema kuna kaya 28 ikiwemo 16 za Majengo zimekubwa na maafa hayo ya mafuriko.
 
Alisema vijiji vilivyokumbwa na mafuriko hayo ni  Makonde,Majengo, A , B na Mtama yenyewe na taarifa za kutokea kwa tukio hilo zimefikishwa kwa viongozi wa wilaya akiwemo Mkuu wa wilaya na Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo.
 
Mkuu wa wilaya hiyo Dk Nadoro Hamidi alikiri kutokea kwa tukio na kueleza kuwa aliwatembea waathiriwa kwa lengo la kuwapa pole na amewaangiza wataalamu wake kufanya tathimini ya hasara iliyotokea ikiwemo kutafuta namna ya kuwapa msaada wa haraka waathirika hao.

Monday, January 20, 2014

JUICE YA MACHUNGWA MKALI ALIEKUA ANAUNDA DIAMOND SOUND ALIA NA BEN KINYAINYA ASEMA ALIMPA LAKI NNE LAKINI HAKUPIGA NYIMBO YAKE NA MWISHO WA SIKU AKASEMA UZALENDO KWANZA SASA AIBUKA NA BAND YAKE AKIITA THE BEST 4 BYE 4

JINA la JUICE YA MACHUNGWA si geni katika masikio ya watu na hasa kama umeifuatilia diamond sound international ambayo iliweza kutamba na wimbo wake wa MAPENZI KITU GANI,ambapo kipande chake cha sasa umefika muda wa kuchezaaaaa............... na baada ya kufariki kwa aliekuwa mkurugenzi wa band hiyo ndipo band hiyo ilipoanza kusuasua na mwisho wa siku kugawanyiika na kuwa band mbili moja ikiitwa diamond musica origal ingine ikiitwa diamond musica nternational vijana classic lakini baadae ikashindwa kuhimili ndipo alipoweza kugawanyika rasmi na ndipo waliobaki kila mmoja akifanya kazi kivyake ambapo ALAIN MULUMBA akaweza kutoa kibinda nkoi remix ambayo alimshirikisha huyo huyo JUICE YA MACHUNGWA


SASA rapa huyo wa zamani wa DIAMOND MUSICA anasema watangazaji wengi wanajifanya wanainua muziki wa dansi lakini ndio wauaji wa muziki wa dansi akimtolea BENNY KINYAIYA na kusema alichokifanya hawezi kukisahau kamwe baada ya kutengeneza project yake na kuipeleka kwa media ndipo alipofika katika mikono ya benny kinyaiya alipomwambia ampe laki nne kwa ajili ya promotion ndipo alipoitafuta kwa udi na uvumba na kuipata kisha kumpa benny lakini mwisho wa siku nyimbo yake haikupigwa wala kufanyiwa promo kama alivyoahidiwa na mwisho wa siku ndipo alipoamua kumtafuta kwenye simu na alichoambuliwa ni matusi na dharau na kuambiwa kuwa kwa sasa wanafanya uzalendo kwa wanamuziki wa kitanzania kwa vile yeye mcongo basi hawezi kupewa promo na mwisho wa siku nyimbo hiyo mpaka sasa ameamua kutoipeleka kwengine  na sasa ameamua kufanya album na baada ya hapo aweze kuizindua,

ILA juice ya machungwa kwa sasa amesema kuwa ameanzisha band yake inaitwa THE BEST 4 BYE 4 ambayo kwa sasa ameshaanza kufanya show baada ya kushindikana kwa kuanzishwa kwa band ya LA MUSICA BAND kutokana na mdhamini kulega lega na kushindwa kusimimamia kikamilifu uanzishwaji wa band hiyo na kusisitiza kutoka kwenye band yake mpka mwezi wa tano atakua ameshakamilisha album yake

Friday, January 17, 2014

BAADA YA AHADI NYINGI ZA UZINDUZI WA BAND NA ALBUM SASA MANGUSTINO AFUNGUKA KILICHOSABABISHA KUTOKAFANIKISHA SUALA HILO ILA ASEMA MWAKA HUU NI ZAMU YA K MONDO SOUND






Akiongea na blog hii kiongozi wa band ya K.MONDO sound ameweka wazi kilichosababisha kushindwa kufanya uzinduzi wa band ya k mondo pamoja na uzinduzi wa album ya MAGAMBO na kusema ni maswala ya kiutawala yalikuwa hayajakamilika sasa ikabidi mmiliki wa band hiyo aweze kuahirisha zoezi hilo mpka ambapo amepata uongozi wa kiutalawa ambao unaweza kumuongoza katika kuzindua band hiyo pamoja na album kwa mwaka huu kabla ya kufika mwezi wa sita na kusema kawaida ya nyimbo za band huwa zinachelwa kuhits na hivyo wataweza kuzindua album yao ambayo toka mwaka jana imeshaisha kwa kuwa kwa sasa ndio nyimbo zake zimeanza kufanya vizuri katika media mbalimbali kwa hiyo mpka siku ya uzinduzi basi nyimbo zitakuwa zimeshaeleweka vichwani kwa wapenzi wa k mondo sound ambapo kwa mujibu wa mangustioni akisema kuwa band yake mpka sasa ni band ya pekee katika medani ya band zinazopiga katika makumbi tofauti na kusema mwaka huu wataanza kupiga show zao sehemu tofauti tofauti na mwaka jana ambapo walikuwa wanapiga maeneo mawili tu kwa ila kwa sasa wamejipanga kujitanua zaidi na kuweza kufanya vizuri na kuwa gumzo la jiji la dar-es-salaam,

Wednesday, January 15, 2014

BAADA YA KUPIGA MZIKI KATIKA FALME ZA KIARABU BONZO KWEMBE AREJEA BONGO KUENDELEZA LIBENEKE SASA KUACHIA ALBUM NNE KWA MPIGO HATARI


MCHARAZAJI gitaa maarufu nchini aliyewahi kuzipigia bendi mbalimbali ndani na nje ya nchi, Ismail Kwembe 'Bonzo Kwembe' anayemiliki bendi binafsi iitwayo 'The Bokwe Tunes Band' anajiandaa kuingia studio kurekodi albamu yake ya kwanza tangu ajitegemee (solo artist).
Bonzo aliiambia MICHARAZO kuwa, albamu hiyo itakayokuwa na nyimbo nne itapigwa katika miondoko tofauti ikiwamo Zouk na itawashirikisha wasanii kadhaa nyota na chipukizi nchini.
Mwanamuziki huyo alisema kwa kuanza ataanza kurekodi wimbo uitwao 'Mapenzi ya Mbali' atakaoimba na mwanamuziki mmoja mkongwe (jina hataki liwe hadharani kwa sasa) na Said Kaunga, chipukizi wa dansi na kipa wa zamani wa Toto Africans.
"Nitaanza na Mapenzi ya Mbali nitakayoimba na wanamuziki Said Kaunga niliye naye katika bendi yangu na mkongwe mmoja, kisha utafuata nyingine zilizosalia," alisema Bonzo.
Bonzo ambaye mbali na kupiga gitaa pia ni mtunzi na muimbaji kwa sasa, alizitaja nyimbo nyingine zitakazokuwa katika albamu hiyo ni pamoja na 'Shida za Dunia', 'Janga la Ukimwi',  na 'Upendo wa Moyo'.
Kuhusu bendi yake, Bonzo alisema inaendelea na maonyesho yake kwenye mahoteli na katika harusi kwa mialiko maalum wakiwa wakijikita kupiga na kuimba nyimbo za 'kukopi' za wasanii na makundi mbalimbali ya kimataifa.

Tuesday, January 14, 2014

TOTOO ZE BINGWA AFUNGUKA KUHUSIANA NA WALIOFUKUZWA MALAIKA BAND ASEMA MANENO MANENO YAMEWAPONZA NA KUVIMBA KICHWA NA VIJIPESA VIDOGO NDIO VIMEWAPONZA NA KUWA WATOVU WA NIDHAMU ASEMA MALAIKA BAND BADO INASONGA

Kiongozi wa Malaika band Totoo za bingwa amefunguka rasmi kuhusiana na waliofukuzwa ndani ya band ya malaika band na kisa kizima ni kuwa wanamuziki hao walijidanganya kuwa wao ni wzuri baada ya kusifiwa nao na ndio maana wakaanza kuvimba kichwa na kuwa watovu wa nidhamu kiasi ya kwamba wakataka kuwalizimisha viongozi hao kufanya wale wanayotaka wao na mwisho wa siku ndipo uongozi ulipoamua kuwasimamisha mpaka pale watakapojirekebisha lakini mwisho wa siku wakaanza maneno ya kuwavunjia heshima ndipo totoo ze bingwa akiwa kiongozi alipoamua kuwafukuza kabisa na kusema hawezi kufanya nao kazi tena na band kwa kuwa ni ya watu watatu cristian bella,totoo ze bingwa na andrew sekidia kwa hiyo wanamuziki waliowachukua ilikua kama kufanya back up ya uimbaji lakini mwisho wa siku na wao wakataka kujifanya ni wenye band wak hiyo malaika band itaendelea


Mbali na hilo pia amelalamikia vyombo vya habari watu wanaoandika blog kwa kuandika maneno ya kupotosha ili kuwachafua lakini kwa kufanya hivyo hawaharibu bali wanawafanya wazidi kusonga mbele zaidi.

BANZA STONE KUREJEA JUKWAANI TAR 25 KUTAMBULISHWA RASMI NA EXTRA BONGO MBIONI KUREKODI MEGA MIX YAKE

Baada ya kuoguakwa muda mrefu na sasa akiwa anarejea katika hali yake banza stone amezana mazoezi na band yake ya extra bongo huku akitarajiwa kuweza kureja rasmi ulingoni kwenye jukwaa hilo kwa utambulisho rasmi utaoafanyika katika ukumbi qwa nyumbani wa meenda sinza ambapo kwa mujibu wa kamarade ally choki mkurugenzi wa extra bongo amesema kwa sasa  banza yupo katika hatua za kufanya mazoezi zaidi kwa kuwa hali ya imezidi kuimarika kidogo na toka wafanye ziara kanda ya ziwa ambapo alikuwa asimama kwa muda mfupi jukwanii lakini kiwango chake cha sauti kikiwa kimerudi kawaida kabisa sasa kutokana na mtababu aliyopata mpaka jumamosi ya tar 25 anaweza kuwa tayari kuvamia jukwaa kwa muda mrefu kidogo kwa ajili ya kuwaonyesha show mashabiki
na kutokana na kupata mdhamini anatarijiwa kurekodi mega mix ya nyimbo alizowahi kutunga kipindi cha nyuma ikiwe elimu ya mjinga,mtaji wa masikini,mtu pesa, na nyingine nyingi zilizowahi kutamba katika kipindi cha nyuma

                                    LE GENERALY BANZA STONE
 Banza stone ni mmoja ya wanamuziki walioweza kusimamisha mziki wa dansi na kutamba sana na mpaka akweza kuchukua tuzo mbali mbali ikiwemo ile ya bbc ambayo ailiipata kupitia wimbo wa mtu pesa wakati yupo twanga pepeta na pia alikwishachukua best male vocalist katika kilimanjaro music award

Monday, January 13, 2014

MAFAHARI WATATU MBIONI KUTOA ALBUM YAO BINAFSI NI ALLY CHOKI,BANZA STONE,NA MUUMINI MWINJUMA WASEMA WAMESHAPATA MDHAMINI WANATAKA KURUDISHA ENZI

Akiongea kwa niaba ya wenzake mkurugenzi wa extra bongo le kamarade ally choki amefunguka na kuweka wazi baada ya kufanya show kanda ya ziwa kama mafahari watatu yaani banza stone,muumini mwinjuma pamoja na ally choki na kusema sio show hiyo tu kuwa kuna muendelezo mwingine wa kueza kutoa album yao binafsi baada ya kupata mdhani ambae ni YUSUPHEN na kusema mwaka huu hauwishi lazima wawe wamekwisha toa album hiyo ambayo amesema bado haijajulikana itakua na nyimbo ngapi lakini wapo katika mpango huo lakini wataandaa show maalum kwa ajili ya mafahari hao watatu jijini dar-es-saalaam ili kuwakumbusha watu jinsi dansi ilivyoweza kusimama  kipindi hicho na kusema kwambabado wanauwezo wa kufanya kama zamani tu
                        LE KAMARADE ALLY CHOKI

Tuesday, January 7, 2014

KANAL TOP YUPO VIZURI NA ANAENDELEA NA SHUGHULI ZAKE KAMA KAWAIDA

Nikiongea na Tarsis masela joto ambae ni rais wa akudo impact amesema habari za canal topo kuwa anaweza kuwa amekamatwa china na amehukumiwa kifo ni za uongo kwa kuwa yeye anawasiliana na mke wake ambae kwa mujibu wa masela kuwa wameweza kuwasiliananae hvi karibuni na yupo hai ila amesema watu wanapenda kusambaza habari bila kuwa na uhakika wa kutosha lakini pia katika utafutaji mungu nae ana mipango yake ila kwa swala kuwa canal top amekamatwa china ni habari ambazo hazina uhakika na kusema kuwa canal top anaendelea na biashara zake ambazo tofauti na muziki kama kawaida
KANAL TOP ME AND TARSIS MASELA

Monday, January 6, 2014

RAIS WA SASA WA AKUDO TARISIS MASELA JOTO MKURUGENZI WA FASHION AFUNGUKA KUHUSU MPANGO WA AKUDO IMPACT 2014 ASEMA KWA SASA HAWATOI SINGLE TENA MPAKA PALE UONGOZI UTAKAPOKUBALI KUZINDUA ALBUM KWA KUWASHAPELEKA NYIMBO NYINGI RADIONI PIA ASEMA CHUKI NDIO ZINAUA MUZIKI WA DANSI

Tarsis masela mmoja kati ya wanzilisha wa akudo impact amefunga na kuweka wazi mipango ya akudo impact ambayo wengi wanadhani imezama lakini yeye asema bado wako vizuri na kila wakipiga show wanajaza watu kama kawaida kwa kuwa wana nyimbo nyingi nzuri na za kutosha na nyingi zikiwa zinachezwa kwenye vituo mbalimbali vya radio,lakini amesema kitu kilichokua kinasimamisha kazi za akudo kwenda mbele ni uongozi ambao toka mwaka jana walikuwa wanaahidi kuzindua album hiyo ambayo waliipa jina la historia no change lakini mwisho wa siku hadi mwaka umeisha bila kukamilisha dhamira yao na sasa amesema tayari amekwisha ongea na uongozi wa band kwa sasa hawatatoa single tena mpka pale uogozi utkapokubali kuizindua album hiyo,



mbali ya hilo pia amesema chuki na fitina ni kitu ambacho hakipnendi katika muziki wa bongo na ndio kinachofanya muziki usiende mbele kwa sababu kuwa watu wanatazama kuziua band nyingine lakini sio kutoa ushirikiano wa kuinua muziki mwisho wa siku band nyingi zinakua na uhasama badala ya kuwa na mapenzi mema ya utafutaji katika muziki,

lakini pia amesema kwa sasa show za akudo ziko kama kawaida na wanapiga karibu kila mahali na sasa hvi wanatafuta wadhamani ili waweze kuzunguka mikoani kwa ajili ya kuweza kuzitambulisha nyimbo zao mpya na wanamuziki wao wapya ambao wameongeza nguvu katika safu ya uimbaji

Thursday, January 2, 2014

ABRACADABRAAAA YA KALALA JUNIOR HAKUNAGA AFUNGUKA KUHUSU KITU AKICHUKIACHO AKIWA KATIKA TASNIA YA MUZIKI WA DANSI

Akizingumza na blog hii KALALA JUNIOR a,k.a HAKUNGA aliweza kufunga kitu ambacho wengi hawakijui ni pamoja kuwa ndoto zake kubwa kwa sasa ni kuwa producer wa muziki wa aina zote na ndicho anachopigania sana kwa sasa licha anaendelea kuimba miziki tofauti na akiamia hizo ndoto anaweza kuzitimiza wakati wowote atakapokuwa tayari kuanzia mwaka huu.

2.Kitu ambacho amesema anakichukia saana katika tasnia ya muziki wa dansi ni pamoja na wasanii kutojitambua wao ni kina nani na ndio mwisho wa siku wanafanya mambo ya ajabu ajabu yanayowafanya kudharaulika mbele za jamii nyingine zinazowatazama wao kama kioo cha jamii

3,KALALA juniour anasema kitu ambacho kamwe hawezi kukisahau maisha mwake katika kuelekea mafaniko yake ya muziki ni siku aliweza kurekodi kwa mara ya kwanza na baba yake ni pindi tu Mzee KOMANDO HAMZA KALALA alipokimbiwa na wanamuziki wake kina CHRISTIAN SHEGGY na yeye ndipo alimwambia baba ake hata yeye ni mwanamuziki ataweza kuziba pengo hilo ndipo mzee kalala alipoweza kumruhusu kungia kwenye muziki moja kwa mojan a huku akiikumbuka nyimbo amabyo alianza kuirekodi ni ile ya TANGU LINI NGOZI YA KITI MOTO IKAWAMBWA NGOMA
  KALALA kwa sasa anajipanga kuzindua album yake binafsi ambayo kabla ya kuisha mwaka 20014 atakua maekiwsha izindua.


.

.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...