Kaya zaidi 60 katika kijiji cha Mtama jimbo la Mtama wilaya Lindi zimekosa makazi kufuatia nyumba zao kubomolewa na mvua iliyoambatana na upepo.
Mkazi wa kijiji hicho Zainabu Isa alisema kwamba mvua hiyo ilianza kunyesha zaidi ya masaa saba kuanzia saa 9 alasiri hadi saa 5 usiku na kusababisha hasara ya kuharibu nyumba na chakula ambayo thamani yake haijatambulika hadi sasa,
zainabu alisema wakati mvua hiyo inanyesha maji yalikuwa yakitokea ardhini na kuungana na mvua yaliyokuwa yakitoka juu na kusababisha kubomoa nyumba za wakazi wa kijiji hicho.
Alisema mvua ilipokuwa ikiendelea kunyesha watu walioathiriwa waliweza kuhifadhi kwenye nyumba za majirani mpaka mvua iliponyamaza majira ya saa tano usiku,
Kwa upande wake mtendaji wa kijiji cha Majengo ‘A’ Safu Hamisi alisema kuna kaya 28 ikiwemo 16 za Majengo zimekubwa na maafa hayo ya mafuriko.
Alisema vijiji vilivyokumbwa na mafuriko hayo ni Makonde,Majengo, A , B na Mtama yenyewe na taarifa za kutokea kwa tukio hilo zimefikishwa kwa viongozi wa wilaya akiwemo Mkuu wa wilaya na Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo.
Mkuu wa wilaya hiyo Dk Nadoro Hamidi alikiri kutokea kwa tukio na kueleza kuwa aliwatembea waathiriwa kwa lengo la kuwapa pole na amewaangiza wataalamu wake kufanya tathimini ya hasara iliyotokea ikiwemo kutafuta namna ya kuwapa msaada wa haraka waathirika hao.
0 comments:
Post a Comment