WAY

Tuesday, January 28, 2014

ALIYEKUWA mwanamuziki mahiri wa bendi ya African Stars 'Twanga Pepeta' Soud Mohammed (MCD) amefariki usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya KCMC-Moshi.

Taarifa kutoka ndani ya Twanga Pepeta usiku wa jana, zinasema kuwa MCD alikuwa amelazwa hopsitalini hapo kwa kusumbuliwa na akiwa anasumbuliwa na matatizo ya miguu.
Inaelezwa kuwa mwanamuziki huyo aliyewahi kuwa Bingwa kucheza Disko mkoa wa Kilimanjaro kabla ya kujitosa kwenye muziki wa bendi alifariki majira ya saa saa 2:30 usiku.
Enzi za uhai wake MCD aliwahi kuzipigia bendi ya Diamond Sound 'Wana Ikibinda Nkoy', Twanga Pepeta na hivi karibuni alihamia Mashujaa Band kabla ya kurejea Twanga ambapo aliondoka wiki kadhaa kuelekea kwao Kilimanjaro kujiuguza na kukutwa na mauti hayo.
                                                MASOUD,ME AND MAREHEMU MCD
Safari rado inatoa pole kwa wanafamilia, ndugu na jamaa za mwanamuziki huyo pamoja na kuwapa pole wana Twanga Pepeta na wadau wa muziki wa ujumla.
Mzishi ya msanii huyo yanatarajiwa kufanyika leo mchana mjini Moshi,Mungu aiweke roho ya marehemu Mahali Pema Peponi.
Taarifa kutoka ndani ya Twanga Pepeta usiku wa jana, zinasema kuwa MCD alikuwa amelazwa hopsitalini hapo kwa kusumbuliwa na akiwa anasumbuliwa na matatizo ya miguu.
Inaelezwa kuwa mwanamuziki huyo aliyewahi kuwa Bingwa kucheza Disko mkoa wa Kilimanjaro kabla ya kujitosa kwenye muziki wa bendi alifariki majira ya saa saa 2:30 usiku.
Enzi za uhai wake MCD aliwahi kuzipigia bendi ya Diamond Sound 'Wana Ikibinda Nkoy', Twanga Pepeta na hivi karibuni alihamia Mashujaa Band kabla ya kurejea Twanga ambapo aliondoka wiki kadhaa kuelekea kwao Kilimanjaro kujiuguza na kukutwa na mauti hayo.
Safari rado inatoa pole kwa wanafamilia, ndugu na jamaa za mwanamuziki huyo pamoja na kuwapa pole wana Twanga Pepeta na wadau wa muziki wa ujumla.

Mzishi ya msanii huyo yanatarajiwa kufanyika kesho mchana mjini Moshi,Mungu aiweke roho ya marehemu Mahali Pema Peponi.

0 comments:

Post a Comment

.

.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...