WAY

Monday, January 27, 2014

BAADA YA UZINDUZI WA ALBUM YA NINI YA FM ACADEMIA LAKINI ALBUM YENYEWE HAIONEKANI MITAANI RASI WA FM ACADEMIA NYOSHI ELSAADAT ALITOLEA UFAFANUZI ASEMA WAMEPELEKA NYIMBO ZOTE NJE KUZIFANYIA MASTERING ILI KUEPUKA MAHARAMIA LAKINI PIA NI KATIKA KUWAPA WATU HAMU YA KUITAFUTA ALBUM ILI KIINGIA SOKONI IPAPATIKIWE ASEMA HIYO NDIO STYLE YAO MPYA KATIKA BIASHARA YA MUZIKI

Licha ya tar 21-dec 2013 Kuizindua rasmi album ya CHUKI YA NINI pale mzalendo pub lakini album hiyo hiyo imekua ikiuliziwa na mashabiki kwa kuwa kila wakienda sokoni hawaipati na wala kwenye maonyesho ya fm academia pia hawaipati zaidi ya kupata nyimbo hizo live,kutokana na hili nikaona nimtafute rais wa fm academia NYOSHI EL SADAAT SAUTI YA SIMBA ili aweze kulitolea ufafanuzi suala hili ndipo alipofunguka na kuweka wazi kuwa kwa sasa audio na video za album hiyo wamezipeleka nje kwa ajili ya kufanyiwa mastering ili zisiwezi kuibiwa kirahisi lakini pia amesema kwa kufanya hivyo ni kuongeza soko kwa mashabiki wa band hiyo kwa kuwa watakuwa na hamu sana ya kuitaka album hiyo na pidnipo watakapoiingiza sokoni basi itaweza kupapatikiwa sana kwa sababu kila mtu atakuwa na hamu nayo ila uzinduzi walioufanya ni kwamba kuanza sikuh hiyo itakua rasmi wanapiga nyimbo za kwenye album mpya na kuwazoesha mashabiki na huku akisema soon wakae tayari kuweza kupata wimbo mpya wa OTILIA ambao utakua katika album hiyo,

                                               NYOSHI, ME AND KING BLAISE
AIDHA amewataka mashabiki wa fm academia wasichoke kusubiri album hiyo ya chuki ya nini ambayo imesheheni nyimbo nzuri nyingi zinazovutia zaidi na tafauti na miaka yote kwa kuwa walikaa kimya muda mrefu kwa ajili ya kuweza kutoa album itafunika hata zile vuta nikutvute na hata duniak kigeugeu

0 comments:

Post a Comment

.

.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...