Vijana wilayani Lindi wametakiwa kujiunga na vikundi mbalimbali vya uzalishaji mali ili kuweza kujipatia fursa ya kujikwamua kimaisha badala ya kujiingiza kwenye makundi ambayo hayana tija.
Wito huyo umetolewa na mkuu wa wilaya Lindi Dk Nasoro Himidi wakati alipofunga mafunzo ya ujasilimali Kata ya Chiponda jimbo la Mtama yaliyodhaminiwa na mbunge wa jimbo hilo Bernard Membe.
Dk Nassoro alisema wilaya Lindi inavijana wengi wenye uwezo wa kufanya kazi za uzalishaji lakini kinachokosekana ni vijana kutokujitambua, hivyo ni vyema wakajikita kwenye vikundi vya uzalishaji mali ili kuepukana kujiunga na makundi mabaya.
Alisema lengo la viongozi wetu akiwemo mbunge wenu dhamira yake kuwakuza na kuwaendeleza kijasiliamali ili mwisho wa siku muweze kujimudu kimaisha tofauti na ilivyo hivi sasa vijana wengi ujiingiza katika makundi mabaya na wengine wakiishi vijiweni.
Akizungumza kwa niaba ya washiriki wa mafunzo hayo Zuwena Yusuph alisema kuwa wajasiliamali 97 wanawake 45 na wanaume 52 kutoka vikundi 9 vya ujenzi, kilimo,useremala,ufugajikuku na nyuki mama Lishe na ufyatuaji wa matofali.
Zuwena alisema wanavikundi hao wanaojiusisha na uzalishaji wamepata elimu ya ujasiliamali ikiwemo ya utunzaji wa vitabu vya hesabu kuwa mafunzo waliyopata yatasaidia kuwaongeza uelewa jinsi ya kuendesha biashara, kutafuta masoko ,kutunza mitaji pamoja na ushindani wa soko.
0 comments:
Post a Comment